RESOLVED HOJA Ushauri wangu: Mabasi ya abiria ya mikoani yaishie Mbezi Magufuli

RESOLVED HOJA Ushauri wangu: Mabasi ya abiria ya mikoani yaishie Mbezi Magufuli

Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Mapato hayapotei maana wafanyabiashara wako hadi shekilango pale. Nadhani ungeshauri stand ya magufuli kwakua ni international, basi iwe kama Airport, ondoa wapigadebe wote ndani, kujaza wapiga debe ndani ya stand na wafanyabiashara imefanya stand kupoteza mvuto.

Dunia ya sasa imejikita kwenye kutatua kero za watu/kuwafanyia urahisi kwa kila jambo. Wewe unatuletea mawazo ya kutesa watu?
Mfano: Kwa mtu anayeishi Gongo la mboto, Kigamboni nk unampeleka Magufuli akafanye nini?
Huwa nasema, tunahitaji mapinduzi ya SAYANSI ili watu wawe na mawazo ya kutafuta suluhu za kurahisishia watu maisha na sio mawazo ya ajabu ajabu......
 
Mbona mabasi yote ni lazima yaingie magufuli na kushushwa shekilango,then yanaelekea ofisini kwao,

Binafsi sishukiagi magufuli,nashukia kariakoo,ulisema lazima abiria wote washuke magufuli mbona tutateseka
Utateseka vipi wakati kuna daladala, mwendokasi, bajaji na bodaboda zote zinakufikisha mpaka katikati ya mji!
 
Isitoshe management ya Magufuli bus stand siyo professional wala haiko customer friendly. SIPENDI SIPENDI na nasema SIPENDI kwenda Magufuli Terminal
Hiyo ndiyo agenda ya msingi.
Majuzi kulikuwa na shida ya maji na vyoo vilifungwa.
Unajiuliza kituo kikubwa kama kile kukosa choo hata saa moja tu hali inakuwaje?
Taarifa kituoni hapo zinasema kuwa meneja wa kituo hicho haruhusiwi kununua hata kitasa.
Kwamba kila kinachoharibika kinatakiwa kijadiliwe na mkurugenzi wa manispaa pamoja na watalaam wake.
Urasimu huu unaongeza changamoto lakini wizi wa watendaji nduyo unaoleta shida zote hizo.
 
Hilo wala sio tatizo,
Tatizo ni mtu mwenye mizigo yake anayeshukia hapo Mbezi Magufuli akiwa na mizigo na watoto atafikaje Ubungo, Kinondoni, Kariakoo, Posta, Kigamboni n.k

Kama walikuwa wanataka Dar iwe na stendi moja tu ya mabasi sehemu ya kuijenga ilifaa iwe Ubungo, Mwenge, Sinza, Shekilango, Kariakoo, Posta au Kigamboni.
Kuwa na mizigo mingi pamoja na kusafiri na watoto nafikiri hilo ni suala binafsi. Msafiri mwenyewe anatakiwa kujipanga
 
Kuwa na mizigo mingi pamoja na kusafiri na watoto nafikiri hilo ni suala binafsi. Msafiri mwenyewe anatakiwa kujipanga
Kama serikali ilikuwa ina shida sana ya kuwa na stendi moja tu Dar yenyewe ndio ilitakiwa ijipange mapeme kuweka hiyo Stendi mwisho wa mji, Posta au Kigamboni, mambo mengi yoyote ya kutaka abiria wote wa Dar kutumia Magufuli ni ujinga usio na mfano.
 
Tukiwafelisha tutatengeza wezi na vibaka , hapo ndo sehemu wanapookoteza riziki zao kwahiyo ni vzr kuwatengenezea mazingira rafiki ya biashara
Siyo kweli, machinga wanaofanya biashara hapo Magufuli pamoja na wapiga debe ndiyo wanaochafua hiyo terminal.
Kwamba wataishije ikiwa wataondolewa mahal hapo hilo siyo jukumu la stendi hiyo.
 
Mwezi mmoja uliopita mkuu wa wilaya wa ubungo alitembelea pale stand ya magufuli , nilitazama kwenye TV namna wafanyabiashara wa Mbezi magufuli wakilalamika baadhi ya mabasi yakitoka mikoani yanapitiliza hayashushi abiria mbezi magufuli

In summation

Dhumuni la kujenga kituo cha Magufuli ni kusogeza mabasi ya mikoani yasifike city centre , kama sio hivo basi sioni umuhimu wa Serikali kujenga stand ya magufuli kila kampuni ya mabasi ingejenga stand yake kiholela
Mkuu lakini stendi binafsi zilikuwepo hata kipindi ambacho stendi kuu ipo pale ubungo. Kama lengo ni kuondoa msongamano serikali ilitakiwa kuzipiga ban hizi stendi ndogo pale pale mwanzo wakati stendi ya magufuli inaanza kutumiaka. Sasa hivi italeta shida, na ukizingatia wabongo tukishazoeshwa kuvunja sheria tunaona ni haki yetu.

Serikali nayo ni shida. Wanasiasa wanawaza zaidi uchaguzi ujao kuliko maendeleo. Unayoyaongea bila shaka yapo kwenye meza ya watendaji, sema sasa ndio wanawaza wakitekeleza hilo maana yake kura zote za wakazi wa huku city center washazikosa
 
Kama serikali ilikuwa ina shida sana ya kuwa na stendi moja tu Dar yenyewe ndio ilitakiwa ijipange mapeme kuweka hiyo Stendi mwisho wa mji, Posta au Kigamboni, mambo mengi yoyote ya kutaka abiria wote wa Dar kutumia Magufuli ni ujinga usio na mfano.
Mkuu mji unapanuka hata wakati stendi ya ubungo inatengenezwa mji ulikua unaishia magomeni kama sikosei. Mshua akishawahi kuniambia miaka ya zamani stendi kuu ilikua mnazi mmoja. Hata hii magufuli kuna kipindi kitafika italazimua isogezwe magari saba au mbele zaidi, kwahiyo hauwezi kusema stendi ijengwe sehemu moja na ibakie hapo hapo mpaka mwisho wa dohari
 
Hao wamachinga wa Mbezi Magufuli warudi kijijini wakalime, kama wameshindwa kufanya biashara zao sehemu nyingine Dar. Kwanza stendi ni kwa ajili ya abiria kushuka, kupanda bus na kujisaidia, hayo mengine ya kula biscuits, crisps na mayai ni ziada tu.
Wanachinga kwa kweli ni lazima wadhibitiwe. Sio stend tu hata kwenye masoko na barabarani pia. Wanasababisha usumbufu na kero.

Kuna hawa wanaitwa mawinga nao washaanza kuwa kero. Huko vituoni na kwenye masoko
 
Mkuu mji unapanuka hata wakati stendi ya ubungo inatengenezwa mji ulikua unaishia magomeni kama sikosei. Mshua akishawahi kuniambia miaka ya zamani stendi kuu ilikua mnazi mmoja. Hata hii magufuli kuna kipindi kitafika italazimua isogezwe magari saba au mbele zaidi, kwahiyo hauwezi kusema stendi ijengwe sehemu moja na ibakie hapo hapo mpaka mwisho wa dohari
Kama kila mji ukipanuka stendi inasogezwa, miaka michache ijayo mtasema mabasi ya Dar yaishie stendi ya Kibaha.
 
Nabisha wewe passport huna kuijua unaijua kupitia TV
Nimekwenda SA kabla wewe hujazaliwa zadi ya mara 20 kuanzia 199 hadi 2015. Nimepita Joburg, PE, Capetown na Pretoria. Joburg naijuwa zaidi na nilikuwa naishi kitongoji cha Bruma Lake karibu na Eastgate
 
Mkuu mji unapanuka hata wakati stendi ya ubungo inatengenezwa mji ulikua unaishia magomeni kama sikosei. Mshua akishawahi kuniambia miaka ya zamani stendi kuu ilikua mnazi mmoja. Hata hii magufuli kuna kipindi kitafika italazimua isogezwe magari saba au mbele zaidi, kwahiyo hauwezi kusema stendi ijengwe sehemu moja na ibakie hapo hapo mpaka mwisho wa dohari
FACT
 
Magufuli alijitahidi Kudhibiti hio hali Lakini Kwa sasa naona Shekilango, Riverside na mazese kote Wamiliki wa mabus wanazidi Kujenga Vituo
 
Una akili za kijinga sana sana Ndugu yangu, Una akili ndogo sana, Mabasi yako mangapi? Most of them yanaondoka na kuingia usiku, huo msongamano unaosema ni upi?<
sidhani km kulikuwa na haja ya kutukana ungemuelewesha vzr tu nadhani labda angeelewa.. pengine ulichoandika ww ndo cha kijinga kbs!
 
Back
Top Bottom