Ushawahi kwenda sehemu, baada ya kukuona wakakuchukulia poa, baadaye wakajua wewe ni mtu wa aina gani, wakaanza kukuonea aibu?

Mheshimiwa Hakimu 😂😂😂
 
Aise japo naona kama chai

Ngoja niseme tu

Mwaka 2019 kama sikosei nlikiwa nafanya kazi sehemu nchi jirani kwa boss mmoja yeye ni maarufu na anahela kweli

Aliniagiza niende makao makuu ya benk moja nchi jirani kuna jambo nifuatilie

Nilipofika nikakutana na warembo kweli , si unajua staff wa bank wanavopendeza

Mimi huwa ni simple sana japo sipendi kuwa hivo , sasa nikawaambia nahitaji huduma fulani nianzie ofisi gani?
Aise waliniangalia hovyo na kutokunkzingatia hadi nikaamua sasa niwaambie naomba nionane na fulani,maana sikutaka wafanye wajibu wao kisa fulani naenda kwake ,nilitaka wanipe maelezo ndio niingie

Baada ya kutaja naomba kumuona fulani na huyo mtu kushuka hadi floor ya chini walihaha sana , hawakuamini 😀

Sometimes tuwe humble tu , mimi sijawah mkandamiza mtu kisa ninauwezo wakufanya hicho
Mfano hata nikienda sehemu kunahuduma naweza ipata kwa haraka kisa namjua boss wa hilo eneo situmii hio advantage


PILI
Kunamda nilikuwa naonekana mimi ni dereva tu maana sieleweki, jamani tujiweke sawa

Tunaweza pishana na wawekezaji au watu muhimu kwa kutuchukulia poa


Ngoja tunitahidi tujimwambafai na kutafuta magari ya hadhi ya juu😀

Maoni tu
 
Mimi hapa aisee
Hakuna nunda haijakukuta

Mimi kuna kipindi nilienda mlimani city bookshop pale , nilikutana na mzee mmoja very simple

Nilivomuona akawa ananiongelesha namjibu kawaida kabisa na kutozingatia mengine anayoniambia, alitaka nizoea haraka sana nikachukulia poa wakati hata namba tungebadilishana

Sasa kwa njia zangu za haraka haraka wakati wa kulipia kitabu nikakuta kachukua vitabu kama 10+ sasa alilipa akaondoka

Baadae nikaambiwa huyu ni fulani ambaye ni mtu mzito sana na muhimu kwenye network za mjini

Kumbe ningemzingatia sana ningepata connection lakini nilimchukia poa sana nikawa simzingatii

Be active , connect with people bila ku assume tu
 
Kabisa first impression inaweza fukuza watu wa muhimu
 
Aisee
 
Ungesubiri wakuombe lift kwanza ndo uwape..by the way hukuamua kuwaletea ukauzu
 
Mzee wewe sio masikini...vichenchi unavyo
 
Yes, niliunganishwa na senior wangu kazi moja hivi ambayo alialikwa akaifanye yeye, na kwa namna ilivyokuwa nilikuwa naimudu vizuri sababu nishawahi kufanya zaidi ya hiyo

Sasa baada ya kufika yule jamaa kugundua mwamba kanituma mimi akaanza kuongea maneno ambayo hayakuwa mazuri kwamba ameletewa mtu ambae hajui kazi hivyo nitaharibu

niliifanya ile kazi kwa huzuni kidogo sababu mwamba hakunichangamkia hata kidogo na hata ule ushirikiano wa kawaida sikupewa kivile

nilimaliza kile kimeo kikawa fresh na wateja wake (yeye alikuwa kama cordinator) wakatumiwa ile kazi na wakaifurahia, sijui kama yeye aliiona au la

Fast forward miaka kadhaa mbeleni nikaapply Mchongo kwenye kampuni yao na nikapata kwenye kada tofauti na yake ila Mungu si athumani kumbe kile kitengo mkiwa na project mnakuwa wasimamizi halafu wale wengine wanakuwa watekelezaji

Siku ya kwanza tunapishana korido nilimsalimia akauchubua (sa sijui alijua dogo kaja kutafuta ajira au hata intern maana taasisi ilikuwa kubwa sio poa)

Mara ya pili hivyo hivyo

Siku alipagawa tunakutana kwenye fingerprint anabonyeza nami nabonyeza
Hajakaa vizuri tunakutana kwenye ofisi ambayo wanaingia wafanyakazi peke yao halafu na mimi nimo

Sijui aliuliza huko akaambiwa ajira mpya huyo tupo nae hapa, maana ilikuwa full aibu alinikazia for no reason na bado akaleta mikunjo

Mpaka kesho jamaa hajawahi kuwa na amani tunapokuwa pamoja hata tukipiga stori za kiofisi na staff wengine maana anajua siku niki-raise tu ile stori wana watamwona mchawi sana
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…