tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Ijapokuwa Rais Samia atamtumia Rais Trump salamu za pongezi kinafiki, ushindi wa Trump ni mwiba mkali kwa serikali ya Tanzania na CCM.
Sote tunafahamu kuwa serikali ya CCM inapenda misaada na mikopo kutoka Marekani na nchi nyingine tajiri za dunia na kisha kuitumia misaada hiyo kwa manufaa ya machawa na wachumiatumbo wachache.
Sasa kwa kuwa Trump kaingia madarakani, CCM na serikali yake pamoja na machawa wanaopenda pesa za ubwete, wajiandae kufa njaa. Kwa kawaida Trump hashughuliki na ustawi wa nchi nyingine, hasa nchi za Afrika zinazonuka rushwa, ufisadi na uchawa.
MAONI YANGU
Nawapongeza sana wamarekani kwa kumrejesha Trump madarakani ili asaidie kuwanyoosha hawa akina Matonya wanaotandaranda huko na huko kutafuta misaada ili kujaza matumbo yao mapana yasiyoshiba. Sasa tutaelewana tu. Trump endelea kukaza hivyo hivyo hadi kieleweke. Maji mtayaita mma nyie ombaomba msiokuwa na haya. Trump mwaga mboga tukose wote. Machawa wote mnaotusumbua nchi hii, kiyama chenu kimewadia.