Ushuhuda: Nilishinda njaa siku 3, nikaanza kuokota vyakula barabarani, nikashikwa kwa uzururaji

Ushuhuda: Nilishinda njaa siku 3, nikaanza kuokota vyakula barabarani, nikashikwa kwa uzururaji

Angalia huo uhai wako usikutie kiburi
Hapana pot uhai haunipi kiburi nitakuja hapo getini kukuomba na kukusihi uirejee imani ya haki ukifeli sitasita kutimiza wajibu na sharia isemavyo .

Alafu siku nyingine usieleze kuwa unapata mshahara around one million ni chenji za watu tena wengi waliokuwa nduguzo katika imani ulipokimbia ni mambo ya kawaida sana.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Niliwahi kushuhudia binti mmoja wa kiislam alikuwa akiitwa Mwanaidi asee alianza kwanza kupenda nyimbo za kwaya, mara akahamia kwenye kusoma bible akawa mkristo ndani ya familia ya kiislam bila mzee wake kujua thou mama yake alikua anajua. Baadae akaita kikao cha familia na kuwaambia msimamo wake kuhusu imani. Doo palitokea msala wa kufa raia ,familia yote ikamtenga, wakawa wanaletwa mpak masheikh wa kisomali kumsomea vsom na kumshauri lkn holaa, wakamtimua home baba yake akamwambia mm sio baba yako tena na hii sio familia yako na ndugu wote wakamtenga ila sasa dada ameolewa na anafamilia na maisha mazuri sanaa. Kaka yake alipata tatizo shingoni alikula nyama yenye adrax pelekwa hospital hawaoni ugonjwa. Alipofanyiwa upasuaji shingo yote pamoja na pua ni usaa tu ,cha kushangaza tunaenda msalimia hospital yupo na mafuta makubwaa ya mtumishi flan ivi anapakwa shingn na amepona kabsa na makofi siku hiz anapiga.
 
Ndo tatizo la waislamu ukiacha tu dini na undugu umekufa utatengwa hata na mende wa nyumbani.
Tofaut na Wakristo wapo hadi mashehe familia Yao wote ni Wakristo na Wala hapana mwenye habari nae Kama halijatokea jambo na undugu wao haukomi kisa dini
 
Ulikuwa hujaiona misikiti, au huzijuwi nyumba za Waislam?

Hakuna msikiti au Muislam atakunyima kula, siku nyingine ukisikia njaa, jitose msikitini tu uwaambie Waislam shida yako, utakula mpaka ukitazame macho chakula.

Hivi unaishi Tanzania au wapi?
Huko si ndio ndugu zake walipomtosha.
Mnaweza toa msaada kwa asie Muislamu?
 
Murtard ni hatari kwa sana kwa jamii ni kitendo cha unafiki mkubwa hustahili kuishi diniani tena. Nakushauri fanye toubah nasihi urudi kwenye uasilia wako kabla mabaya zaidi hajakukuta.
Acha kumtisha mwenzako wew. Tuna watu wengi duniani wanaishi maisha mazuri mno na sio waislam wala waikristo, achen vitisho vya kipumbavu nyie
 
Hapana pot uhai haunipi kiburi nitakuja hapo getini kukuomba na kukusihi uirejee imani ya haki ukifeli sitasita kutimiza wajibu na sharia isemavyo .

Alafu siku nyingine usieleze kuwa unapata mshahara around one million ni chenji za watu tena wengi waliokuwa nduguzo katika imani ulipokimbia ni mambo ya kawaida sana.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Ni ndogo lakini kwa mtu ambaye sikupata sapoti ya wazazi na ndugu ni nyingi.
 
Wala simtishi na staki ni mtishe nampa tu ushauri, nayeye mwenyewe ni shuhuda hawezi kupata Amani bila maelewano na wazazi wake.
Ukimsoma vizuri jamaa anatamani arudi japo nyumbani kumsalimia mzee wake na inaonekana mshua ndo hataki salam yake wala hamtaki tena mpaka arudi kwenye imani ya baba yake. Sasa hapo nani ana makosa au nani alaumiwe?
 
Niliwahi kushuhudia binti mmoja wa kiislam alikuwa akiitwa Mwanaidi asee alianza kwanza kupenda nyimbo za kwaya, mara akahamia kwenye kusoma bible akawa mkristo ndani ya familia ya kiislam bila mzee wake kujua thou mama yake alikua anajua. Baadae akaita kikao cha familia na kuwaambia msimamo wake kuhusu imani. Doo palitokea msala wa kufa raia ,familia yote ikamtenga, wakawa wanaletwa mpak masheikh wa kisomali kumsomea vsom na kumshauri lkn holaa, wakamtimua home baba yake akamwambia mm sio baba yako tena na hii sio familia yako na ndugu wote wakamtenga ila sasa dada ameolewa na anafamilia na maisha mazuri sanaa. Kaka yake alipata tatizo shingoni alikula nyama yenye adrax pelekwa hospital hawaoni ugonjwa. Alipofanyiwa upasuaji shingo yote pamoja na pua ni usaa tu ,cha kushangaza tunaenda msalimia hospital yupo na mafuta makubwaa ya mtumishi flan ivi anapakwa shingn na amepona kabsa na makofi siku hiz anapiga.
Hallelujah
 
Njia nyepesi ya kupata chakula ugenini zunguka popote ukikuta Pana msiba hapo ndo kwako jibidiishe tu kufanya kazi za kupasua Kuni,kusomba maji,nk.
Peleleza kazi ya marehemu ili uwe na technic ikitokea ukiulizwa unamfahamu vipi unaweza sema nilikua fundi wake,kibarua wake nk.
Hadi msiba uishe utakuwa umeshapata ramani
 
Ahahahay
Yaani ningekuta msiba mahali ningekomaa mpaka arobaini 😳😳😳😳

Njia nyepesi ya kupata chakula ugenini zunguka popote ukikuta Pana msiba hapo ndo kwako jibidiishe tu kufanya kazi za kupasua Kuni,kusomba maji,nk.
Peleleza kazi ya marehemu ili uwe na technic ikitokea ukiulizwa unamfahamu vipi unaweza sema nilikua fundi wake,kibarua wake nk.
Hadi msiba uishe utakuwa umeshapata ramani
 
Ukimsoma vizuri jamaa anatamani arudi japo nyumbani kumsalimia mzee wake na inaonekana mshua ndo hataki salam yake wala hamtaki tena mpaka arudi kwenye imani ya baba yake. Sasa hapo nani ana makosa au nani alaumiwe?
Sio rahisi kujua wake mpaka mwenyewe afunguke, tujue mazingara yake yalio msababisha awe Murtard huo ukaidi wake aliuanza na umri gani? Ndo tutaweza kuhukumu nani mwenye makosa.
 
Ni ndogo lakini kwa mtu ambaye sikupata sapoti ya wazazi na ndugu ni nyingi.
Kaka Sandali Ali mbona sio wewe ninayekujua kwenye mada zingine mbona mpole sana na mwingi wa hekima ?

Sawa kaka hongera kwa kila jambo aisee najisikia vibaya kuendelea kukujibu vibaya maana hekima zako zinanihukumu .

Kwaheri .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Hapana pot uhai haunipi kiburi nitakuja hapo getini kukuomba na kukusihi uirejee imani ya haki ukifeli sitasita kutimiza wajibu na sharia isemavyo .

Alafu siku nyingine usieleze kuwa unapata mshahara around one million ni chenji za watu tena wengi waliokuwa nduguzo katika imani ulipokimbia ni mambo ya kawaida sana.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
Acha kumtisha mwamba wewe .yeye amechagua kuamini uko alipo na wew amini unachoabudu ova. Hakuna cha imani ya haki wala nn, watu duniani wanaishi bila hiyo imani ya haki na wanaishi maisha mazuri mno kuliko ww. Akina president Xi kule na wachina wengi, wajapan, wahindi , mpaka akina kiduku kule north korea hawajui cha mtume wala Yesu na huwaambii kitu na hyo imani yako ya haki. Funga mdomo acha watu waamini wanachotaka
 
Kuna member humu jf kwenye ule uzi wa watu waliowahi kupitia magumu kwenye maisha alisema alikua akihisi njaa anameza mate mengi au anaachama mdomo upepo unaingia tumboni siku zinasonga, alikonda mpaka alikua akimilikwa tochi tumboni mwanga unatokea upande mwingine wa mgongo.

But guess what, God is good👍
 
Hello habari za asubuhi!
Hii story nimewahi kuwasimulia wachache sana.
Ni rahisi kumtia moyo mtu kuwa magumu yatapita, Mungu atakusaidia kipindi uko vizuri na umeshiba. Ila ukipitia kipindi kigumu hata ushauri na courage utasikia kama kelele tu unapigiwa.
Nikihitilafiana na wazazi pamoja na ukoo nzima 2009 kwasababu ya kuingia katika Imani tofauti.
Kwakweli yule baba yangu ana roho mbaya sana, hata sasa hajawahi kunitafuta. Nami natamani kwenda kumsalimia na kumpa msaada lakini msimamo wake ni kwamba niende kwake nikairudie dini yangu ya zamani kitu ambacho Mimi sikiafiki, sitakiafiki na hakitatokea hata kwa kuchinjwa.
Sasa maisha ya kuhangahikia ugali pasi na sapoti ya mtu (mzazi, mlezi, ndugu n.k) nikajiendea mgodini. Nikaenda kupiga kibarua kwa siku elfu 7, nilienda Mgodini November , December mgodini pakawa na mapumziko ya sikukuu hivyo watu wote tulipaswa kuondoka mgodini mpaka January.
Nikiwa na pesa kidogo sijui nifanye nini au niende wapi nikaamua niende Mkoa wa Ruvuma Tunduru.
Safari ya kwenda Tunduru nikitokea Nachingwea (Lindi) ikaanza.
Kwakuwa nilitumia Lori Tunduru tulifika siku ya pili . Nimefika Tunduru mchongo niliouendea ukagoma hivyo nikaunga mpaka Songea. Nafika Tunduru mfukoni nina pesa ndogo sana hata elfu 2 haifiki.
Safari ikaendelea barabara chafu maana ni masika. Njaa inauma Lori likisomama naangalia huku na kule kama kuna mwembe nikaangalie maembe.
Njaa ikaongezeka Songea tulifika kwa kuchelewa, Lori lilibeba nazi hivyo sometimes nilipata nazi zilizovunjika zenyewe na kuanza kula.
Tumefika Songea usiku wa saa 4, sina ndugu, Sina hata mia na ni mgeni huko
Am back.
Basi ile sijui niende wapi, nikaanza kuelekea mahali kwenye kelele nikafika stand kuu sasa pale nina njaa plus usingizi.
Nikajichanganya kwa machokoraa wa stand, Mungu awainue huko waliko, wakanipa andazi moja na chai kikombe kimoja.
Niliwashuru sana, pale stand hapakuwa na lounge ya abiria kipindi hicho. Sijui sasa kukoje.
Nikapita mitaani kuzurura kutafuta mahali nilale nikapata mahali pembezoni mwa mji nikalala kwenye shamba la mahindi.
Asubuhi nikashikwa na polisi nikiwa stand na kupewa kesi ya uzururaji, jumla ya watuhumiwa tulikuwa kama 15-20.
Tukiwa korokoroni gari ya super Feo iliyokuwa ikitoka Songea kwenda Dar es salaam ikapata ajali. Sasa mkuu wa kituo akaamuru tubebwe tupelekwe Central halafu wale maaskari wakaatend ajali.
Ile tunapandishwa kwenye gari tukitokea ndani kituoni kuingia kwenye karandinga mmoja mmoja Mimi nikafichwa na wingu la Mungu hawakuniona wakawasha gari wakaondoka . Polisi si chini ya watano wote hawakuniona ilhali nilisimama mbele yao na wengine niliwagusa.
Next day tena nikarudi stand, nikachujua nguo zangu nzuri nikaziweka mkononi na kujigeuza mmachinga. Nilizunguka manispaa yote, Aisee katika kipindi kigumu kila solution hugeuka kuwa ngumu. Nguo nilianza kutangaza nauza kwa elfu 5 , nikashushe bei ikawa elfu 3 na mwishowe nikawa nauza buku buku lakini hata moja sijaiuza.
Siku ikaisha njaa Kali, nikalala nje.
Kila nikijaribu kuomba kazi yoyote hata kulima au kulishia ng'ombe nilikosa. Watu wanasema hawanijui hivyo hawawezi kuniamini.
Hapo nilikuwa nimeibiwa vitu muhimu ikiwemo daftari la namba za simu, I'd ya kupigia kura na I'd ya skuli maana nilikuwa ndo nimetoka kumaliza form four.
Siku moja nikiwa taabani fundi viatu akanisaidia 500 ila suala la kunisaidia makazi ya kulala hakuweza sijui kwanini . Nikifurahi sana nikaanza kuzungukia migahawa nikaupata mmoja nikapewa ubwabwa wa 500 mwingi sana nikala huku nahemea maana nilikuwa nikikuta chocote kitu barabarani changu iwe muhindi, karanga au hata dagaa namla.
Kwa ufupi sasa niko Da es salaam, nimeajiriwa na Kaisari, nina familia yenye furaha na amani, niko kwenye uchumi wa kati.

Am happy.
YESU ni BWANA
Kumtegemea MUNGU kuna faida.
MUNGU Baba wa Mbinguni azidi kukubariki sana.
Pole kwa yaliyokukuta.
 
Back
Top Bottom