Ushuhuda: Nilishinda njaa siku 3, nikaanza kuokota vyakula barabarani, nikashikwa kwa uzururaji

Ushuhuda: Nilishinda njaa siku 3, nikaanza kuokota vyakula barabarani, nikashikwa kwa uzururaji

Mkuu kuna tafauti ya Murtadi na muumini wa dini nyingine wakuzaliwa hao ni watu wawili tofauti........Murtadi ni laana kwenye familia lakini imani zingine ni sawa nikiweka jitihada tu warudi penyewe.
"Murtad na muumini wa dini nyingne wa kuzaliwa ni tofaut" sawa naomba nijibu hyo laana inakuathiri vipi wew na familia yako katika ukoo wako???.
 
Njia nyepesi ya kupata chakula ugenini zunguka popote ukikuta Pana msiba hapo ndo kwako jibidiishe tu kufanya kazi za kupasua Kuni,kusomba maji,nk.
Peleleza kazi ya marehemu ili uwe na technic ikitokea ukiulizwa unamfahamu vipi unaweza sema nilikua fundi wake,kibarua wake nk.
Hadi msiba uishe utakuwa umeshapata ramani
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
"Murtad na muumini wa dini nyingne wa kuzaliwa ni tofaut" sawa naomba nijibu hyo laana inakuathiri vipi wew na familia yako katika ukoo wako???.
Laana ni ukosefu wa radhi za mungu katika mambo mengi ya maisha yako, laana sio rahisi kuiona siku moja, ni gradual........
 
Ulikuwa hujaiona misikiti, au huzijuwi nyumba za Waislam?

Hakuna msikiti au Muislam atakunyima kula, siku nyingine ukisikia njaa, jitose msikitini tu uwaambie Waislam shida yako, utakula mpaka ukitazame macho chakula.

Hivi unaishi Tanzania au wapi?
Wewe mama unataka kijana wa watu akaliwe kalio Kwa kisimgizio cha suna?dini ILO aliliama alafu alilrejee kweli?
 
Ulikuwa hujaiona misikiti, au huzijuwi nyumba za Waislam?

Hakuna msikiti au Muislam atakunyima kula, siku nyingine ukisikia njaa, jitose msikitini tu uwaambie Waislam shida yako, utakula mpaka ukitazame macho chakula.

Hivi unaishi Tanzania au wapi?
Tena akienda pale mtoro kariakoo atasaza haswa! Sjui alifeli wapi?

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Ndo utuambie sasa hizo radhi za Mungu wew zinakuathiri vipi kwa yeye kuwa murtad???
Mkuu sasa zitaniathiri je wakati mimi sitoki kwenye familia yake? hilo ungeuliza wana familia yake uwauliza vinavyo wakumba uko tangu ndugu yao aritardi.
 
Hello habari za asubuhi!
Hii story nimewahi kuwasimulia wachache sana.
Ni rahisi kumtia moyo mtu kuwa magumu yatapita, Mungu atakusaidia kipindi uko vizuri na umeshiba. Ila ukipitia kipindi kigumu hata ushauri na courage utasikia kama kelele tu unapigiwa.
Nilihitilafiana na wazazi pamoja na ukoo nzima 2009 kwasababu ya kuingia katika Imani tofauti.
Kwakweli yule baba yangu ana roho mbaya sana, hata sasa hajawahi kunitafuta. Nami natamani kwenda kumsalimia na kumpa msaada lakini msimamo wake ni kwamba niende kwake nikairudie dini yangu ya zamani kitu ambacho Mimi sikiafiki, sitakiafiki na hakitatokea hata kwa kuchinjwa.
Sasa katika maisha ya kuhangahikia ugali pasi na sapoti ya mtu (mzazi, mlezi, ndugu n.k) nikajiendea mgodini. Nikaenda kupiga kibarua kwa siku elfu 7, nilienda Mgodini November , December mgodini pakawa na mapumziko ya sikukuu hivyo watu wote tulipaswa kuondoka mgodini mpaka January.
Nikiwa na pesa kidogo sijui nifanye nini au niende wapi nikaamua niende Mkoa wa Ruvuma Tunduru.
Safari ya kwenda Tunduru nikitokea Nachingwea (Lindi) ikaanza.
Kwakuwa nilitumia Lori Tunduru tulifika siku ya pili . Nimefika Tunduru mchongo niliouendea ukagoma hivyo nikaunga mpaka Songea. Nafika Tunduru mfukoni nina pesa ndogo sana hata elfu 2 haifiki.
Safari ikaendelea barabara chafu maana ni masika. Njaa inauma Lori likisimama naangalia huku na kule kama kuna mwembe nikaangalie maembe.
Njaa ikaongezeka Songea tulifika kwa kuchelewa, Lori lilibeba nazi hivyo sometimes nilipata nazi zilizovunjika zenyewe na kuanza kula.
Tumefika Songea usiku wa saa 4, sina ndugu, Sina hata mia na ni mgeni huko
Am back.
Basi ile sijui niende wapi, nikaanza kuelekea mahali kwenye kelele nikafika stand kuu sasa pale nina njaa plus usingizi.
Nikajichanganya kwa machokoraa wa stand, Mungu awainue huko waliko, wakanipa andazi moja na chai kikombe kimoja.
Niliwashuru sana, pale stand hapakuwa na lounge ya abiria kipindi hicho. Sijui sasa kukoje.
Nikapita mitaani kuzurura kutafuta mahali nilale nikapata mahali pembezoni mwa mji nikalala kwenye shamba la mahindi.
Asubuhi nikashikwa na polisi nikiwa stand na kupewa kesi ya uzururaji, jumla ya watuhumiwa tulikuwa kama 15-20.
Tukiwa korokoroni gari ya super Feo iliyokuwa ikitoka Songea kwenda Dar es salaam ikapata ajali. Sasa mkuu wa kituo akaamuru tubebwe tupelekwe Central halafu wale maaskari wakaatend ajali.
Ile tunapandishwa kwenye gari tukitokea ndani kituoni kuingia kwenye karandinga mmoja mmoja Mimi nikafichwa na wingu la Mungu hawakuniona wakawasha gari wakaondoka . Polisi si chini ya watano wote hawakuniona ilhali nilisimama mbele yao na wengine niliwagusa.
Next day tena nikarudi stand, nikachujua nguo zangu nzuri nikaziweka mkononi na kujigeuza mmachinga. Nilizunguka manispaa yote, Aisee katika kipindi kigumu kila solution hugeuka kuwa ngumu. Nguo nilianza kutangaza nauza kwa elfu 5 , nikashushe bei ikawa elfu 3 na mwishowe nikawa nauza buku buku lakini hata moja sijaiuza.
Siku ikaisha njaa Kali, nikalala nje.
Kila nikijaribu kuomba kazi yoyote hata kulima au kulishia ng'ombe nilikosa. Watu wanasema hawanijui hivyo hawawezi kuniamini.
Hapo nilikuwa nimeibiwa vitu muhimu ikiwemo daftari la namba za simu, I'd ya kupigia kura na I'd ya skuli maana nilikuwa ndo nimetoka kumaliza form four.
Siku moja nikiwa taabani fundi viatu akanisaidia 500 ila suala la kunisaidia makazi ya kulala hakuweza sijui kwanini . Nikifurahi sana nikaanza kuzungukia migahawa nikaupata mmoja nikapewa ubwabwa wa 500 mwingi sana nikala huku nahemea maana nilikuwa nikikuta chocote kitu barabarani changu iwe muhindi, karanga au hata dagaa namla.
Kwa ufupi sasa niko Da es salaam, nimeajiriwa na Kaisari, nina familia yenye furaha na amani, niko kwenye uchumi wa kati.










Am happy.
YESU ni BWANA
Process za Mungu ni ngumu sana kuzielewa! Ila cha msingi ni kiziamin na kizikubali....
 
Ndo utuambie sasa hizo Laana za Mungu wew zinakuathiri vipi kwa yeye kuwa murtad???
Ungekua makini sana, kile kitendo cha kutoelewana na baba ako mzazi ni sehemu ya madhara ya hizo laana, hamna kitu kinacho uma kama kutoelewana na wazazi wako, mkuu bado unauliza laana za murtardi ni zipi?
 
Ndo tatizo la waislamu ukiacha tu dini na undugu umekufa utatengwa hata na mende wa nyumbani.
Tofaut na Wakristo wapo hadi mashehe familia Yao wote ni Wakristo na Wala hapana mwenye habari nae Kama halijatokea jambo na undugu wao haukomi kisa dini
Sio tatizo la waislaam, ndio hukmu ilivyo maana hata akifa kabla hajarudi katika uislam hata kwenye viwanja vya pepo hawatakuwa pamoja

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Ungekua makini sana, kile kitendo cha kutoelewana na baba ako mzazi ni sehemu ya madhara ya hizo laana, hamna kitu kinacho uma kama kutoelewana na wazazi wako, mkuu bado unauliza laana za murtardi ni zipi?
Kwahyo mkuu kuwa na maoni tofauti na mzazi wako ni laana?? Mfan mim mshua akiniambia somea udaktari nika kataa nikamwambia mm nataka kusomea uinjinia, kwahyo hapo tayari laana. Ahhhahh mkuu imani yako ni ipi kwanza tuanzie hapo
 
Back
Top Bottom