Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Kweli expert wangu tushukuru kwa kila jambo,ndio majaliwa yetuMaisha ni kuridhika tu na unachostaili kupata.
Ulishawahi kukosa pesa hata sh 100 ya kula unaishi nyumba ya kupanga na mwisho wa mwezi tayari........View attachment 3377475
Jana nikiwa katika mishe mishe ndani ya Daslamu,kwanza nilipita sehemu nikaona watu bwana wana makazi mazuri sana,yani unapata hamu hata ya kuwahi kurudi home,nyumba kali,garden kali na swimming pool ya kiushikaji.
Jamani kuna watu wanaishi kwenye makazi mazuri na kuna sisi tumejaaliwa kujistiri tupate pakulala na kujihifadhi
Nikiwa njiani ndani ya jiji la Daslamu,nakutana na ndinga kali barabarani,jamani kuna watu wana drive ndinga na wengine tuna usafiri wa kutoka point moja kwenda nyingine
Unajua nini expert wangu? Iko hivi mwisho wa siku tutakufa,kwahiyo take it ize,yani usiwaze kivile,hatupo duniani milele kwamba ukose raha mbona mimi sipo kama wale au similiki mali kama wale
Kifo kiwe liwazo kwako kwamba hayo yote hayatadumu milele,kwahiyo haina haja ya kukosa raha na furaha,mwisho wa siku hapa duniani tunapita tu
Umekosa makazi ya ndoto yako,just chill usikonde
Umekosa ndinga ya ndoto yako,just chill usikonde
Umemkosa umpendaye kwa dhati,just chill usikonde,coz ipo siku ungekufa wewe au yeye
Kwa kila jambo ambalo limekuwa hamu yako kubwa tambua kwamba one day,huu ulimwengu utaisha na maisha halisi yataanza huko akhera,kikubwa tengeneza mazingira ili upate neema za huko akhera
Ni hayo tu!
Imeshawahi kunitokea kipindi fulani huko nyumaUlishawahi kukosa pesa hata sh 100 ya kula unaishi nyumba ya kupanga na mwisho wa mwezi tayari........
Acha tu mkuu, hiyo siku unaweza kutamani walio tangulia mbele ya haki.Imeshawahi kunitokea kipindi fulani huko nyuma
Nimeipenda hii🤣🤣Ni ndoto tu sijui naota kweli, hebu niamke nikapambane hata kama nililala saa tisa.
Expert wangu,hapo ushapambana sana tayar,kwahiyo mwisho wa siku unachagua kuukubali ukweli na hiyo ndio tiba halisiA mindset of a poor man pleasing his heart and colleague's. Pambana weka pembeni excuses. Don't be selfish you're not born for yourself, you're born for others and for thriving generations
Nimeipenda hiiIla kitu ambacho sipaswi kukisahau ni kuwa mimi ni nani na malengo yangu yanapaswa kutimia .
Ni kupambana mkuu kuhakikisha ndoto zinatimia ila ni vyema kutambua sio lazima kila unachokipenda au unachokitaka utakipata kwenye haya maisha.Nimeipenda hii🤣🤣
Hakika MtumishiNi kweli ndinga kali, majumba makali yanapita ila hakikisha yanapitia na kwako pia.