Usinunue kiwanja au shamba lenye mbuyu mkubwa kama huna uwezo wa kukabiliana na changamoto zake

Usinunue kiwanja au shamba lenye mbuyu mkubwa kama huna uwezo wa kukabiliana na changamoto zake

Habari wadau

Ukataji wa mibuyu au miti mikubwa umekuwa ikiambatana na changamoto nyingi sana kwa wamiliki na hata kwetu mafundi!

Ushauri huu tunautoa kwenu tukitambulika kama (SAMICO) ambao ni jopo la mafundi wazoefu katika sekita ya ujenzi, Umeme na gesi asilia! Unaweza kutufuatilia katika kurasa zetu Instagram kwa jina la @samico_tanzania

Kutokana na uzoefu katika fani hii ya ufundi, tunashauri kama mtu huna uwezo mkubwa wa kiuchumi au kiimani!

Usinunue kiwanja au shamba ambalo lina Mbuyu mkubwa au miti mikubwa ya kihistoria ili kuepusha migongano ya kimaslahi inayoweza kujitokeza wakati wa ukataji miti hiyo kwa ajili ujenzi!
Miti hii kwa sehemu kubwa huwa ni (viwanja, bar au kumbi za washirikina) Tulioko site muda mrefu tunajua changamoto zake! Ni kisanga sana ingawa tiba yake tunayo!
View attachment 2286292
Mi ndo napenda viwanja vya hivyo.
Niinyooshe michawi vzr
 
Mimi nimenunua kiwanja chenye mbuyu wa tangu enzi na watu wote wa mji walikuwa wanategemea mzimu huo kujitibu na kuangamiza, lengo niliutaka mimi ule mbuyu ikabidi nitumie akili ya kulinunua lile eneo, dunia ina mambo hii.
 
Shida haipo kwenye kumiliki, tatizo ni pale utakapo taka kuukata ndipo utajua kwanini ulianza kama mchicha
 
Mimi nimenunua kiwanja chenye mbuyu wa tangu enzi na watu wote wa mji walikuwa wanategemea mzimu huo kujitibu na kuangamiza, lengo niliutaka mimi ule mbuyu ikabidi nitumie akili ya kulinunua lile eneo, dunia ina mambo hii.
Ilikuaje mkuu mwisho wa siku!?
 
Hii dunia ina mambo sana najua Kuna watu hawawezi kukuelewa kabisa ngoja siku yawakute ndio wataelewa
 
Hii dunia ina mambo sana najua Kuna watu hawawezi kukuelewa kabisa ngoja siku yawakute ndio wataelewa
Kuna mzee mmoja tulimwambia huko Kigamboni kwamba asikate kienyeje!
Siku ya kwanza shoka ikavunjika mpini wala haukukatika, akaona aite chain saw!
Akaiwasha ikaunguruma na kusambaratika vipande!
Lakini hakutosheka akachukua nyingine!
Awamu hiyo akafanikiwa kuukata wote lakini ukabaki unaelea hewani!
Asubuhi yake mbuyu ulivyodondoka na yule mzee akafa! Siku ile ile!
 
Sijui kwa nini, ila naukumbuka ule Mbuyu pale Kinondoni Hananasifu (jirani na shule) tangu 1980's. Miaka 10 iliyopita nilifika pale na ulikuwepo.
 
Back
Top Bottom