Usinunue kiwanja au shamba lenye mbuyu mkubwa kama huna uwezo wa kukabiliana na changamoto zake

Mi ndo napenda viwanja vya hivyo.
Niinyooshe michawi vzr
 
Mimi nimenunua kiwanja chenye mbuyu wa tangu enzi na watu wote wa mji walikuwa wanategemea mzimu huo kujitibu na kuangamiza, lengo niliutaka mimi ule mbuyu ikabidi nitumie akili ya kulinunua lile eneo, dunia ina mambo hii.
 
Shida haipo kwenye kumiliki, tatizo ni pale utakapo taka kuukata ndipo utajua kwanini ulianza kama mchicha
 
Mimi nimenunua kiwanja chenye mbuyu wa tangu enzi na watu wote wa mji walikuwa wanategemea mzimu huo kujitibu na kuangamiza, lengo niliutaka mimi ule mbuyu ikabidi nitumie akili ya kulinunua lile eneo, dunia ina mambo hii.
Ilikuaje mkuu mwisho wa siku!?
 
Hii dunia ina mambo sana najua Kuna watu hawawezi kukuelewa kabisa ngoja siku yawakute ndio wataelewa
 
Kuna mzee mmoja tulimwambia huko Kigamboni kwamba asikate kienyeje!
Siku ya kwanza shoka ikavunjika mpini wala haukukatika, akaona aite chain saw!
Akaiwasha ikaunguruma na kusambaratika vipande!
Lakini hakutosheka akachukua nyingine!
Awamu hiyo akafanikiwa kuukata wote lakini ukabaki unaelea hewani!
Asubuhi yake mbuyu ulivyodondoka na yule mzee akafa! Siku ile ile!
 
Sijui kwa nini, ila naukumbuka ule Mbuyu pale Kinondoni Hananasifu (jirani na shule) tangu 1980's. Miaka 10 iliyopita nilifika pale na ulikuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…