Usinunue kiwanja au shamba lenye mbuyu mkubwa kama huna uwezo wa kukabiliana na changamoto zake

Usinunue kiwanja au shamba lenye mbuyu mkubwa kama huna uwezo wa kukabiliana na changamoto zake

Kwangu nimeuchimba hadi mizizi lile shimo nikaendeleza hapo choo kabisa tena la 17ft lilipitiliza urefu na upana wa 25ft na wachimbaji walikula laki 450,000 tuu

Ulipata shida sana, nunua chumvi kilo kadhaa kutegemea na ukubwa wa mbuyu, uchimbe, weka changanya na oil chafu, njoo wiki tatu utakuta mbuyu umekufa umeoza.. kazi kwisha... nilitumia roughly 120,000/= tu.
 
Kwahiyo akili ni kuamini meli inaelea halafu kupiga kama watu hupaa na ungo?
Usichokijua usiamini hakipo ni suala la muda tu! Endelea kukua!

Meli haielei kwa imani na kila mtu anaona meli ikielea sio story za hearsay.

On the other end, story za ushirikina including hii yako zote ni story za blah blah mara nimesikia, sijui nimeona ukiambiwa thibitisha huwezi mnataka watu waamini bila reasoning whatsoever. Huu ni uzwazwa.

Mwaka jana kuna mtu alileta uzi humu jukwani unaoendana na huu wako, alisema huko Kigoma kuna diwani alifariki na kufufuka kichawi. Kama kawaida mitanganyika ikaamini pasi na shaka kama inavyoamini hapa. Hamna kufikiri kama nyumbu. Niliuliza swali moja tu, naomba jina la huyo diwani ukizingatia diwani ni public office naweza kuverify hiyo taarifa, zaidi niliahidi kutoa laki 5 kwa mtu yeyote yule atayenipa jina la huyo diwani, chenga nilizopigwa sijawahi kuona hadi leo jina sijapata. Ukiweza wasaidie wenzio ujipatie laki5 kwa kutaja jina tu. Link ya uzi hii hapa:

Ulipata shida sana, nunua chumvi kilo kadhaa kutegemea na ukubwa wa mbuyu, uchimbe, weka changanya na oil chafu, njoo wiki tatu utakuta mbuyu umekufa umeoza.. kazi kwisha... nilitumia roughly 120,000/= tu.
Unauchimba mbuyu wenyewe au chin kwenye mizizi
 
Pengine hilo lenyewe ndilo lishirikina likuu la vilinge vya hiyo mibuyu, so linajitutumua hapa kupumbaza Watu hapa JF [emoji23]

Jamani muelewe hata hapa JF pia tunachati na mawakala wa shetani (mizimu, mapepo, majini, wanga/wachawi/washirikina na waganga wa kienyeji) maana shetani ni roho mchafu awezaye kuingia popote pale pasipo na uwepo wa Mcha Mungu haswaa [emoji16]

Basi hamna wacha Mungu humu ndo maana majini tumeingia 🤣 🤣 miafrika tunasafari ndefu sana.
 
Ulipata shida sana, nunua chumvi kilo kadhaa kutegemea na ukubwa wa mbuyu, uchimbe, weka changanya na oil chafu, njoo wiki tatu utakuta mbuyu umekufa umeoza.. kazi kwisha... nilitumia roughly 120,000/= tu.
Huo mbuyu kadri utakavyokuwa unanyauka na kuoza na wewe unaoza na kukonda taratibu!
Wachawi huona nia njema na ovu! Ukienda kwa nia ya kuharibu na wao watakuharibu
 
Watu tunakata iwe mibuyu au miembe na hakuna shida.
Yaani niache kununua shamba/kiwanja kisa imani za kingese za uchawi?
Mm najua namna ya kuwashikisha kaa la moto.
 
Watu tunakata iwe mibuyu au miembe na hakuna shida.
Yaani niache kununua shamba/kiwanja kisa imani za kingese za uchawi?
Mm najua namna ya kuwashikisha kaa la moto.
Hujaambiwa uache, Uzi umesema wazi endapo huna uwezo kushindana acha!
 
Habari wadau

Ukataji wa mibuyu au miti mikubwa umekuwa ikiambatana na changamoto nyingi sana kwa wamiliki na hata kwetu mafundi!

Ushauri huu tunautoa kwenu tukitambulika kama (SAMICO) ambao ni jopo la mafundi wazoefu katika sekita ya ujenzi, Umeme na gesi asilia! Unaweza kutufuatilia katika kurasa zetu Instagram kwa jina la @samico_tanzania

Kutokana na uzoefu katika fani hii ya ufundi, tunashauri kama mtu huna uwezo mkubwa wa kiuchumi au kiimani!

Usinunue kiwanja au shamba ambalo lina Mbuyu mkubwa au miti mikubwa ya kihistoria ili kuepusha migongano ya kimaslahi inayoweza kujitokeza wakati wa ukataji miti hiyo kwa ajili ujenzi!

Miti hii kwa sehemu kubwa huwa ni (viwanja, bar au kumbi za washirikina) Tulioko site muda mrefu tunajua changamoto zake! Ni kisanga sana ingawa tiba yake tunayo!

View attachment 2286292
Wewe una imani haba
Mbuyu ni mti kama mti mwingine.
Mimi nina mibuyu miwili katika plot yangu kubwa, alikuja jamaa tapeli, ati mganga, akaweka vitambaa vyekundu!
Nikavichomoa na kuvipiga kiberiti.
Nikamwita huyo jamaa , na nikammwambia aache chokochoko, akapotelea mbali huku akiugua akifikiri mie nina "fundi" mkali.
Nikawaambia tu majirani, imani yangu iko vizuri, siamini mambo yasiyo na tija.
 
Hamna kitu ukiwekea imani ya uchawi hapo unaupata kweli ila ukitoa hela vijan wa kazi wanachimba hadi mizizi yote na hakuna kizuizi chochote cha kichawi
Mh wakati nipo mdogo shule tukifagia tulikuwa tunakuta mibuyu imeota asa mm nilikuwa naing'oa nikaambiwa ukifanya ivyo hutopata mtot up now no child I don't know that it's true or not
 
Wewe una imani haba
Mbuyu ni mti kam mti mwingine.
Mimi nina mibuyu miwili katika plot yangu kubwa, alikuja jamaa tapeli . ati mganga aka weka vitambaa vyekundu!
Nikavichomoa na kuvipiga kiberiti.
Nikamwita huyo jamaa , na nikammwambia aache chokochoko, akapotelea mbali huku kiugua akifikiri mie nina "fundi" kali.
Nikawaambia tu majirani, imani yangu iko vizuri, siamini mambo yasiyo na tija.
Lete namba mkuu ...ukakate mbuyu mmoja sehemu upo! Tusiandikie mate na wino upo! Nauli na kila kitu bosi atalipa! Yeye anataka mbuyu utoke!
Lete namba nikupe hilo dili ni hapo pwani wala siyo mbali! Posho utapewa
 
Niliyo kuambia ni ploti yangu mwenyewe, tena iko Pwani.
Sifanyi biashara ya kukata miti.
Ukikubali moyo na roho yako ididimizwe na washirikina, hiyo ni hiyari yko
 
Pale Yombo Dovya kuna mibuyu miwili ilikatwa Shule na Chama aisee mpaka wanataka ilibidi watu wa kitabu waje, nakumbuka ilikua 2011 barabara inajengwa
 
Back
Top Bottom