Youbettersleep
JF-Expert Member
- May 3, 2019
- 955
- 1,672
Leo nimepita kijiwe nongwa nikakutana na mzee mmoja aliyekuwa akitoa maoni yake kwa hasira juu ya vijana ambao bado hawajaoa, Alikuwa na mtazamo mkali lakini wa kusisimua kuhusu mahusiano, na alisisitiza kuwa anazungumza kwa msingi wa uzoefu wa maisha na umri alionao
Haya ndiyo aliyoyasema:
Huyu mzee kamaliza kwa kusema "Ni mzoefu wa maisha na umri na anaelewa nini anazungumza kwa sisi vijana wadogo na wenye kujitafuta.
NAOMBA KUWASILISHA
Haya ndiyo aliyoyasema:
- Epuka kuoa au kuwa kwenye mahusiano na mwanamke ambaye wazazi wake walishatengana lakini bado wanaishi – anadai mwanamke wa aina hii mara nyingi huwa hana muunganiko wa kihisia na mwanaume, anaweza kuona huna thamani kwake na akaweza kuishi bila wewe
- Chagua mwanamke ambaye bado anaishi kwao – yaani yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake, si yule anayeishi mwenyewe "ghetto". Anaamini hii husaidia kujua tabia zake za msingi kabla hajaanza maisha ya kujitegemea
- Mwanamke anayemheshimu baba yake – mzee huyu alisema, ukiona mwanamke anamthamini na kumheshimu baba yake, ni rahisi sana na wewe kupata heshima kutoka kwake.
- Hakikisha unamzidi mambo manne muhimu: kiuchumi, kiakili, kiumri na kimtazamo (uwe na mawazo chanya). Alisema hii itakusaidia kuwa na nafasi ya uongozi wa mahusiano yenye afya na heshima
Huyu mzee kamaliza kwa kusema "Ni mzoefu wa maisha na umri na anaelewa nini anazungumza kwa sisi vijana wadogo na wenye kujitafuta.
NAOMBA KUWASILISHA