Usioe mwanamke ambaye wazazi wake walishatengana ila bado wanaishi

Usioe mwanamke ambaye wazazi wake walishatengana ila bado wanaishi

Yani mwanamke kaajiriwa mkoani, tumekutana huko ila nisimuoe kisa ameanza maisha anaishi getto. Kwahiyo unataka kila siku atoke songea (kwao) aende iringa (kazini) na kurudi ili tusimuone anaishi getto?
NGOJA NIMUULIZE SWALI HILI PIA NA KAMA HUMU KUNA VOICE NOTE NITAIWEKA
 
Kutana na mwanamke ambaye Kila siku anamtaja "mamangu" na hajawahi kumtaja baba yake hata siku Moja. Nenda kwao ukute mama yake alishashindikana na anakukaribisha kwa bashasha na mapochopocho " karibu mwanangu" halafu unakuta Binti lake zuri kweli kweli la sura. Beba Sasa useme umeoa hakuna rangi ambayo hautaiona ,Kila siku linakuja na syllabus mpya ya kukuthibiti na kukunyanyasa Kila idara, kulitema huwezi na hata akili ya kulitema ilishaisha. Ndugu wote walishatimuliwa hawakanyagi kwako umebaki mwenyewe. Stress ++ ulikuwa bonge la mjanja unaanza kuwa fala hadi kazi i
Hivi mwanaume unanyanyaswaje na mwanamke
 
Daaah kwakweli sio vitu vya kupuuzia hata siku 1, mwanamke akiishi maisha ya shurba huwezi muweka sehemu yenye pamba akalala, atalala ila ataamka kuzitoa pamba zote alalie mbao.

Tuishi kwa akili na tuwachunguze kabla ya kuwaweka maishani mwetu
 
Na pia wawili mnapokutana Kuna ground mna set basi lazima izo principles mzifate sio lazima ziwe kama walizoishi Babu zako, Mana waza generation zijazo mambo yatakuwaje ikiwa tunawaza kila siku mwanamke awe submissive tu nakukandamizwa? Tuna watoto na tunawakuza Kwa vile ulimwengu unavyotaka watakuja Kubwa wafanyabiashara wakubwa, Maceo je mtataka tu wakae na sisi mpaka atoke mtu wa Kumuona?

The World is changing very fast na tunapaswa ku adopt, marriage is a not a prison ukiona mtu hamatch na principle mlizo set let her go

Mambo till do us apart ni Ujinga kufanya Kwa mtu mliekutana na meno 32
Mstari wa mwisho umeongea kwa hisia sana
 
Leo nimepita kijiwe nongwa nikakutana na mzee mmoja aliyekuwa akitoa maoni yake kwa hasira juu ya vijana ambao bado hawajaoa, Alikuwa na mtazamo mkali lakini wa kusisimua kuhusu mahusiano, na alisisitiza kuwa anazungumza kwa msingi wa uzoefu wa maisha na umri alionao

Haya ndiyo aliyoyasema:

  1. Epuka kuoa au kuwa kwenye mahusiano na mwanamke ambaye wazazi wake walishatengana lakini bado wanaishi – anadai mwanamke wa aina hii mara nyingi huwa hana muunganiko wa kihisia na mwanaume, anaweza kuona huna thamani kwake na akaweza kuishi bila wewe
  2. Chagua mwanamke ambaye bado anaishi kwao – yaani yupo chini ya uangalizi wa wazazi wake, si yule anayeishi mwenyewe "ghetto". Anaamini hii husaidia kujua tabia zake za msingi kabla hajaanza maisha ya kujitegemea
  3. Mwanamke anayemheshimu baba yake – mzee huyu alisema, ukiona mwanamke anamthamini na kumheshimu baba yake, ni rahisi sana na wewe kupata heshima kutoka kwake.
  4. Hakikisha unamzidi mambo manne muhimu: kiuchumi, kiakili, kiumri na kimtazamo (uwe na mawazo chanya). Alisema hii itakusaidia kuwa na nafasi ya uongozi wa mahusiano yenye afya na heshima

Huyu mzee kamaliza kwa kusema "Ni mzoefu wa maisha na umri na anaelewa nini anazungumza kwa sisi vijana wadogo na wenye kujitafuta.

NAOMBA KUWASILISHA
Kwani Wazee Wengine Mnasemaje?
 
Back
Top Bottom