Usiombe kuacha kazi kisa Forex. Nilivyofilisika na kukimbilia kijijini Tabora

Usiombe kuacha kazi kisa Forex. Nilivyofilisika na kukimbilia kijijini Tabora

Sehemu ya Pili (2)

Nilipoishia

Niliamua kufungua akaunti yangu ya forex na kutumia akiba yangu kama mtaji wa kuanzia. Safari yangu ya kuelekea uhuru wa kifedha ilikuwa imeanza.

Tuendelee..

Nilitafuta eneo bora pa kufanya biashara yangu ya forex. Nilijitahidi kutafuta mahali ambapo ningeweza kujikita na kuzama kwenye biashara yangu bila ya kuingiliwa na mazingira ya nyumbani. Niliamua kutafuta ofisi ya wazi, na mwishowe, nilipata chimbo karibu na Posta, mitaa ya Samora.

Hapo ndo ikageuka kuwa ofisi yangu. Pale, niliweka kompyuta yangu, chati za forex, na kila kitu ambacho ningehitaji kufanya forex yangu. ningeweza kufanya forex bila kuingiliwa na mazingira ya nyumbani.

'''Kabla sijaendelea niseme tu ukweli, pale nilikutana na wadau wengine bana watu wanapambana na hii forex asikwambie mtu, Nnilikutana na mrembo nakumbuka alisema anasoma Udsm,ni mrembo kwelikweli, hii ilinipa moyo na nikajisemea moyoni kumbe forex ndo mpango mzima, nikajipa moyo !hii si ndo biashara sasa, tena iliyokamilika, hakika sikujutia kuacha kazi, Tena nilianza kuiponda huku nikishangaa nilikuwa wapi Mimi mtoto wa Mwanzibo Kitombo..'''

Hii ni kumbukumbu isiyofutika kwenye moyo wangu hadi kesho.

!!Na yule mdada sikumuacha salama, maana nilikuwa naye karibu kama sufuria na mfuniko!!

Tuendelee

Nilianza kujifunza kwa kina kupitia akaunti ya demo, nikiamini kwamba kama ningeweza kufanya vizuri hapo, ningeweza kufanikiwa kwenye akaunti halisi. Kwa miezi kadhaa, nilijitahidi kufanya forex kwa uangalifu na ujuzi wa kujifunzia kupitia akaunti ya mazoezi. Niliona mafanikio kidogo, na hili lilinipa matumaini kwamba naweza kushinda changamoto zote.

Banabana, nilipoamua kuingia kwenye akaunti halisi na kuweka mtaji mkubwa, hali yangu ilibadilika haraka mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio kama farasi wa mwisho kwenye mashindano ya mbio. Hofu ilinikumba na jasho baridi lilianza kunitiririka. Nilijisikia kama mtu aliyeingia kwenye uwanja wa vita bila ya silaha, nikiwa mgeni katika ulimwengu huu wa forex. Kutoka kuangalia tu chati za forex kwenye skrini ya kompyuta yangu hadi kuingia kwenye soko halisi, ilikuwa ni tofauti kubwa.

Kila bonyeza la mouse lilikuwa na uzito wa dunia kwenye kidole changu. Niliogopa kufanya uamuzi mbaya na kupoteza pesa yangu yote. Kila wakati nilipotazama bei zikibadilika haraka kwenye skrini yangu, hisia za kutokuwa na uhakika ziliniondoa usingizi.

Kila pair, iwe EUR/USD siyo GBP/JPY ilionekana kama mtihani wa ujasiri wangu na ujuzi wangu. Hofu ya kupoteza ilinifanya nipambane na migogoro ya ndani, nikiwa na shauku ya kufanikiwa lakini pia na wasiwasi wa kushindwa.

Siku ya tatu hofu ilipungua kila kitu kilionekana kama vile nilivyotarajia. Niliweka trade zenye faida, na akaunti yangu ilionekana kuimarika.

Lakini ghafla, soko lilibadilika mwelekeo, hii siku sintoisahau ilikuwa Arusha nimeenda kula bats na Toto za (R chuga), nimetoka zangu pinpoint naelekea Njiro Tanesco, ndani ya chuo cha wasibu Nina appointment bidada mmoja, ilikuwa jionijioni hivi mvua ikiwa inanyesha nilifika mahali sipakumbuki vizuri gari langu lilikwama, eebhana her, basi nikaanza piga gia wapi, furukita huku na kule wapi, hapo kumbuka nilikuwa nimeweka trade kabla sija weka PT na SL ndo kikatokea hiko kisanga. Baada ya kupambana kulitoa gari kwenye matope. Nikasahau kama niliwema trade, Bahati nzuri walitokea vijana na sikusita kuwaomba msaada, tulifanikiwa kulitoa japo kwa jasho Mimi mwenyewe nimelowana mwili mzima. Kuwashukuru wale vijana nikaingia mfukoni na kutoa note za elfu kumikumi tank nikawapa wale vijana wagawane.

Sasa kimbembe Kikaanzia pale niliporudi kwenye gari langu, nilishtuka ghafla. Nilikumbuka kwamba nilikuwa nimesahau kuweka stop loss wala take profit kwenye biashara yangu. Mioyo yetu inaweza kuwa na furaha na kisha kuwa na wasiwasi mkubwa zaidi ya mara moja.

Nilijikuta nimeshikwa na mshtuko huku nikifikiria kuhusu hatari ya kuacha biashara yangu bila ulinzi wowote. Nilipochukua simu yangu na kufungua MT5.


Hee bana hee nilihisi kuchanganyikiwa....

(Sehemu inayofuata itaendelea Husikose...)
 
Makosa ni yako ya kutoweka Stop Loss, kwangu mimi forex ni nzuri kupita betting, chanse ya kulose au kuwin ni 50 kwa 50. sio kama betting siku akicheza Man City au Ysnga odds 1.12! inamaanisha chance kuwin ni 12 out of 100! By the way " INVEST WHAT YOU CAN AFFORD TO LOSE"
 
Mkuu nimeanza huo ujinga tangu 2016 mpaka nakuja kukubali kabisa hakuna maisha huko ni mwaka Jana. Katika kipindi chote hicho hakuna rangi sijaona. Sina haja ya kukuhakikishia kwa lolote ila Kama upo na swali lolote kuhusu forex karibu.
Vip unaushuuda wowote wa hizi robort za kutrade automatic kama ya ya huyu jamaa anajiita billionaire fx academy kweny Instagram?
 
Vip unaushuuda wowote wa hizi robort za kutrade automatic kama ya ya huyu jamaa anajiita billionaire fx academy kweny Instagram?
Nilishawahi kumiliki mpaka robort lenyewe mkuu. Kwanza Kuna watu walikuwa wanajiita LZ TRADE walikuwa na marobot yao Kama matatu hivi Kama sikosei. Kila bot lilikuwa na gharama zake za kujiunga kulingana na efficiency ya bot lenyewe. Mwanzo faida ilikuwa inapatikana kwani kwa mtaji wa $1500 kulikuwa na uwezejano wa kuwithdraw atleast $300 per week(kulingana na watu waliojiunga kupitia link yako). But all in all ni utapeli mtupu boss.
 
Back
Top Bottom