Muwe mnawasaidia muda mwingine hao watoto wa watu. Mwanamke haachwi Kwasababu isipokuwa kwa usaliti na ushirikina/uchawi wa tabia.
Hawa mabinti tunawaonea bure muda mwingine. Majority hawajawa institutionalized enough kuwa Wife kwa wanaume.
Hebu nambie wanapata wapi trainings za kuandaliwa kuwa wake za watu?! Jamii imejiwekeza zaidi kuwapa watoto wa kike elimu ya corporate na kuwaanda watoto wa kike kuwa watendaji wa serikali na mamlaka zake na taasisi za kibiashara ila wamesahau kabisa kuwajenga na kuwafunza skills za kuwa wake za watu na mama wa familia bora.
Ukitazama juu juu unaweza hisi wanafanya kusudi ila ukitazama kwa kina utagundua kuwa hii kitu inakwenda deep kwenye malezi.
Mimi nikikaa na mabinti hawa especially umri wa kuanzia 25 kushuka huwa najitahidi sana kuwapa elimu ingawa najua haitoshi lakini at least nawapa mwangaza wa maisha kwa perspective inayotakikana.
Muwe mnawaelekeza kama haelekei achana nae kama anaelewa basi nenda nae. Akiomba pesa kwa mahitaji ya msingi na akionesha kweli amekwama usisite kumpatia. Ila kama unampenda na unaplan kufanya nae maisha then muelekeze namna ya kushiriki kutafuta. Ajue uchungu wa inavyotafutwa ili akikuomba akuombe kwa akili na asiombe pesa kiboya.
Sent using
Jamii Forums mobile app