Usiuze kwanza Subiri Mji Ukue hapo pakishachangamka patakulipa sana

embu nipe maana ya kukodisha ardhi kwa muda!
 
wataalamu wa uchumi wataweka sawa juu ya hili
Cc Monetary doctor
We jamaa mmi na uchumi Tena 😂

Kikubwa afanye forecasting vzr , ardhi ndio assets yenyewe Haina expire date wala kuharibika,

Hta ukisikia nyumba imeuzwa million ngp tunathaminisha eneo Hilo ni eneo mahususi kwa ajili ya nn, sio nyumba imeuzwa the actual value ni value ya ardhi.
 
Ni kweli, ila sasa kama kila mtu akishika eneo asiliendeleze akisubiri liendelee litaendeleaje? Hujawahi pita eneo fulani unakuta ni plot miaka na miaka halijengeki? Sababu huwa ni kama hii, wote wamekutana wanasubiri kuendelee.

Lazima kuwe na watu ambao wapo tayari kuachia wageni kwa pesa ndogo. Hawa watu pia ni wadau wa maendeleo la eneo husika maana wasingeuza pasingekuwa hivyo.
 
Mkuu hivi hujui maana ya kukodi au unajitoa ufahamu?
kukodi ni kutumia kwa muda mali/kitu ambayo/ambacho sio yako/chako kwa pesa kulingana na muda mlioelewana na mwenye nayo/nacho.

Kiuhalisia hauwezi kukodisha ardhi never kabisa, fikria wewe una eneo lina thamani ya m100 kisha ukamkodisha jamaa akajenga ghorofa ya thamani ya 1billion akigoma kukulipa hela ya kukukodishia eneo lake utafanyaje? Utabomoa ghorofa lake? Huna uwezo wa kuendesha kesi,hapo utakosa vyote mkuu.

Migogoro ya ardhi haitaisha,na ukimfatilia sana huyo mwenye ghorofa anaweza kukuua ili ajimilikishe kirahsi.
 
Na kukiendelea ndio unakuta wanauza maana alienunua kafika dau kubwa zaidi mfano wewe unasema hili eneo langu nitaliuza kwa million 200 anakuja mtu anakwambia anataka hio eneo kwa million 500 hapo ndipo watu wanapoachia maeneo na ndipo maeneo unapoona yanaendelezwa sababu mtu kauza kwa faida maradufu sio kwa hasara, kuna Mzee mmoja walimfuata hawa watu wanaojenga minara ya simu wakamtaka awauzie eneo lake wajenge Mnara Mzee akawagomea akawaambia anawapa eneo wajenge Mnara ila yeye anachotaka wamlipe mpaka pale watakapouondoa huo Mnara wakaingia makubariano wakasaini Mnara ukajengwa Mzee akaanza kulipwa, akili kubwa pesa aliyolipwa ni zaidi ya ile ambayo angelipwa kwa mkupuo kuwaachia watu wa Mnara wajenge Mnara wao
 
kukodi ni kutumia kwa muda mali/kitu ambayo/ambacho sio yako/chako kwa pesa kulingana na muda mlioelewana na mwenye nayo/nacho.
Ndio hivyo ni km unavyopangishwa km mpangaji kwenye nyumba ya mwenye nyumba wewe unakua umekodi kwa muda ukiisha muda anaweza akakutimua km anataka kufanya kitu kingine kwenye eneo lake na huna cha kumfanya sababu nyumba ni yake na ardhi ni yake
 
Ndio hivyo ni km unavyopangishwa km mpangaji kwenye nyumba ya mwenye nyumba wewe unakua umekodi kwa muda ukiisha muda anaweza akakutimua km anataka kufanya kitu kingine kwenye eneo lake na huna cha kumfanya sababu nyumba ni yake na ardhi ni yake
utamtimuaje mtu ambaye kwanza anakuzidi ukwasi,amejenga nyumba yake ya gharama kwenye eneo lako? Kwanza yeye ndiye atakayekuamrisha kuwa kama unataka usipoteze eneo lako basi kubali akununulie kama unataka upoteze basi usiuze.
Uchaguzi ni wako.
Na tofautisha nyumba ya kupanga na ardhi sawa.
 
Tatizo mkataba na Muumba hatuna.
 
Hapa sijaelewa kua mzee wako alikua na uwezo wa kufanya makubwa kwenye hilo eneo ila yeye akaliuza au hakua na uwezo ndio maana akamuuzia mwenye uwezo huo?
 
Uko sahihi ukiachana trading ya crypto ambayo inanifanya niishii kitajiri biashara nyingine ambayo naipenda sana na huwa inanipa mpunga mrefu ni Real Estate, Mashamba weka miti ya matunda, viwanja weka apartments za Airbnb, Mengine weka mifugo na kilimo cha biashara hutokaa ujutie.
 
Ukiwa na hoja yenye misingi ya Economics, nipo hapa nakusubiri. My offer stands, boy!

View attachment 3401399
mkuu nishamaliza pale juu kuwa hata usubiri kuuza eneo lako mwaka 2070 pesa utakayopewa inaweza kuwa na thamani sawa au ndogo na ungeuza eneo hilohio mwaka 1990. Thamani ya pesa huenda na wakati.
Hao wanaokukazia ni walalahoi hawajui uchumi wala akili ya kuchanganua mambo simple kama haya hawana.
 
Kuna mahali nakubaliana na wewe japo....

Ni nadra kwa ardhi kushuka thamani (depreciation). Ndiyo maana hata ukisubiri ukauza leo, baada ya muda thamani yake utakuta imeongezeka, factoring out inflation. Hata muda huo ukifika ukauza baada ya muda unakuta tena thamani imekwenda juu. Hii inaturudisha kule kule: unapoamua kuuza ardhi jua kwamba hiyo ardhi miaka mitano au kumi huko mbele ya safari itakuwa imeongezeka thamani; na uza tu kama kweli ni lazima ufanye hivyo. Tena hakikisha sehemu ya hiyo hela unaiwekeza mahali ili isipotee bure.

Hakuna mahali utafika useme kwamba hiki ndicho kikomo cha thamani ya ardhi hii; na kwamba huu ndiyo muda sahihi wa kuuza. Labda tu kukiwa na athari zingine za kiuchumi (market fluctuations); na zingine zilizo nje ya uwezo wako.
 
Wewe uza wenzio wana focus ya miaka 100 zaidi ndio maana hawauzi ila wanawekeza kwa malengo ya baadae
 
Hapa umesema vyeema sana mkuu na nahisi tumeelewana nini nilichokimaanisha sio km wengine walivyoelewa juu juu kwamba usiuze tu no angalia future plan yako una malengo gani, mwingine amekumbwa na madeni suluhisho pekee ni kuuza ili alipie madeni ila hana malengo mengine mapya ndio anaishia hapo kuuza kwa hasara basi ila pia mwingine anaingiwa tu na tamaa ya kupata pesa za haraka ila ukiangalia nyuma ya pazia hana malengo yoyote nini atafanyia hio pesa atayoipata baada ya kuuza
 
Exactly mkuu, hilo ndio jambo jema zaidi fanya kitu cha manufaa ya leo na ya baadae zaidi hutojutia
 
Tatizo mkataba na Muumba hatuna.
Mbaya zaidi haujui kwamba anakuchukua lini kwa hio unapofanya maamuzi ya ajabu mwishoni isiwe vile ulitegemea ingekua ndipo unapokaa chini na kujitafakari upya je ulifanya maamuzi sahihi kuhisi kwamba Mungu atakuchukua kesho?
 
Siku moja utanielewa nilikua namaanisha nini leo malizia bia zako hizo nenda kalale
Kuna jamaa mtaani kwetu akimaliza kuvuta bage anakushauri hadi ushauri wa usiende uani ukibanwa na haja. Yani anajikuta mshauri sana kumbe madhala ya bangi. Acha bangi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…