Mkuu Kishina cha Mshahara,
Salary Slip, kwanza naheshimu mawazo yako, ila natofautiana na wewe. Kwanza nchi haindeshwi kwa utabiri, hivyo endelea tuu kutabiri.
Pili hizi ni kelele tuu za chura kisimani, hazimzuii mnywa maji, au kelele za mlango, hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi, endeleeni kupiga kelele mchana, usiku mtalala!.
Sii kweli, hizi kelele za tozo hazumgharimu chochote kisiasa na wapiga kelele baada ya kuona Mama hasikii, sasa wanaanza na kumchomekea na makorokocho ya yuotong!. Haisaidii kitu!.
Kwa by nature, mwanamke ni mvumilivu sana, hivyo Mama ni mvumilivu wa kuvumilia vivu, fitna, husda ndio maana ameweza kuolewa ndoa ya mitala na amevumilia.
Hakuna kitu kama hiki
Uondolewe kwa kosa gani?!. Mtu yoyote akiondolewa na mamlaka ya nidhamu ni lazima liwepo kosa!. Mwigulu ana kosa gani?.
Kwenye hili kuna kitu kinaitwa a scapegoat to cover a political liability, yaani mwanasiasa kufanywa mbuzi wa kafara kufunika makosa ya bosi wake, hili ni kweli hufanyika ila lina gharama kubwa za karma baadae. Tusikubali kumgharimisha Mama kwa karma zisizo za lazima!.
I don't think so!.
DAB hakuwahi kutumbuliwa, aliondoka mwenyewe!.
P