Utabiri: Ni suala la muda tu kabla Mwigulu hajaondolewa katika nafasi yake kwa kubadilishwa wizara au kuondolewa kabisa katika Baraza la Mawaziri

Kwani huyo Mwigulu asipoondolewa katika nafasi yake huo umma utafanya nini zaidi ya kupiga kelele kwenye mitandao? Hakuna la ziada litakalotokea. Hakuna maandamano ya aina yoyote yatakayofanyika. Na CCM itaendelea kushika dola.
 
Mkuu Kishina cha Mshahara, Salary Slip, kwanza naheshimu mawazo yako, ila natofautiana na wewe. Kwanza nchi haindeshwi kwa utabiri, hivyo endelea tuu kutabiri.

Pili hizi ni kelele tuu za chura kisimani, hazimzuii mnywa maji, au kelele za mlango, hazimkoseshi mwenye nyumba usingizi, endeleeni kupiga kelele mchana, usiku mtalala!.

Sii kweli, hizi kelele za tozo hazumgharimu chochote kisiasa na wapiga kelele baada ya kuona Mama hasikii, sasa wanaanza na kumchomekea na makorokocho ya yuotong!. Haisaidii kitu!.

Kwa by nature, mwanamke ni mvumilivu sana, hivyo Mama ni mvumilivu wa kuvumilia vivu, fitna, husda ndio maana ameweza kuolewa ndoa ya mitala na amevumilia.

Hakuna kitu kama hiki

Uondolewe kwa kosa gani?!. Mtu yoyote akiondolewa na mamlaka ya nidhamu ni lazima liwepo kosa!. Mwigulu ana kosa gani?.
Kwenye hili kuna kitu kinaitwa a scapegoat to cover a political liability, yaani mwanasiasa kufanywa mbuzi wa kafara kufunika makosa ya bosi wake, hili ni kweli hufanyika ila lina gharama kubwa za karma baadae. Tusikubali kumgharimisha Mama kwa karma zisizo za lazima!.

I don't think so!.

DAB hakuwahi kutumbuliwa, aliondoka mwenyewe!.
P
Mwigulu amechemsha,hafai kuwa Waziri,mnataka aharibu zaidi Uchumi wa nchi ndiyo tuje ku-regret!!
1.Poor tax administration system
Kuna tax dispute ambayo kesi yake imeifanya serikali ikose kukusanya mapato ya 20 Trilioni.Lakini Kuna shida ya ukadiliaji wa Kodi,maofisa wa TRA wampewa mamlaka makubwa sana,wewe aliona wapi Duniani huu upuuzi!!

2.Poor Distribution of government resources
Matumizi ya Magari ya kifahari (hapa 558 bilioni kila mwaka). Upuuzi mwingine upo Bungeni kule mambo ya Sitting allowance,mfuko wa Jimbo wa Mbunge ni wa nini?kwani Mbunge ni mtekelezaji wa shughuli za serikali!.nk
3.Poor Management of the economy
Zaidi ya 65% ya Watanzania ni wakulima wa tonge kinywani(Subsistence farming) na wengine kwenye informal sector wengiwao Machinga,sasa unapokuwa na Waziri ambaye anawaza kukusanya hela kwa kundi kama hili la oheahe, unategemea nini juu uhai wa Uchumi wa nchi?najua mtasema haya matatizo kayakuta,lakini swali bado linabaki kuhoji kama anayatambua aaya matatizo na kachukua hatua gani?
Siyo kila mtu anaweza kuwa Waziri, Waziri wa fedha akiboronga ndiyo mwafwa!
"Kipawa cha uongozi siyo makalio kwamba kila mtu anayo"
Mwambieni Mama amuondoe huyo mtu wenu,siyo lazima awe Waziri ata akiwa Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni yake au Timu yake ya mpira inatosha!
 
Kwani maamuzi anayofanya yanaanzia kwa boss wake? If Yes, hakutokuwa na UMUHIMU kumtoa Ili Hali tozo zipo palepale
 
Siku nyingine tuwe tunaomba picha za mtu anayetaka kuwania uongozi kabla hajafanikiwa.

Maana nimechunguza kuwa viongozi wenye background za kimaiskini na hawana exposure wakiingia kwenye nyadhifa wanakuwa na kiburi na wanavimba sana na kujiona wao ni mazimba.

Sasa huyu mchunga mbuzi ona mambo yake.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Huna akili
 
Hata kama Mama anampenda au bado ana imani na Mwigulu, ni vigumu sana kuendelea kumbakiza katika nafasi yake kutokana na reaction ya umma kwani anaonekana kuwa ni waziri anaengoza kwa kulaumiwa na kutuhumia na hivyo anakosa sifa ya kisiasa ya kuendelea kuwa waziri.

Kwa maneno mengine, yeye kuendelea kuwa waziri,. sasa kunamgharimu kisiasa Bosi wake jambo ambalo sidhani kama Mama ataendelea kulivumilia. Hivyo, ni swala la muda tu kabla hajaondolewa na mtihani pekee kwa Mama anamuondoaje au anamuondoa katika mazingira gani.

Katika siasa, hata kama hujatenda kosa lolote, ila ikatokea umma unakuunyoshea kidole au kutajwatajwa mara nyingi kwa mambo yasiyopendeza, basi uwajibikaji wa kisiasa huwa haukwepiki ama kwa kuwajibika mwenyewe kwa kujiuzulu nafasi yako, au kusubiri kuonddolewa na Mamlaka yako ya kinidhamu.

Japo hapa Bongo na Afrika kwa ujumla utamaduni huu haijazoeleka sana, ila tartatibu tunaanza kuzoea na mifano teyari iko mingi na hapa kwetu yameshatokea hivyo Mwigulu is the next whether ana hatia au laa.

Bashite is a good example japo ilichukukuwa muda.

Time will tell.
Unataka kusema mwigulu ndo analeta hizo tozo?

Acheni ujinga wa kumtetea mama enu, ,mwigulu anafata maelekezo tu
 
Hata kama Mama anampenda au bado ana imani na Mwigulu, ni vigumu sana kuendelea kumbakiza katika nafasi yake kutokana na reaction ya umma kwani anaonekana kuwa ni waziri anaengoza kwa kulaumiwa na kutuhumia na hivyo anakosa sifa ya kisiasa ya kuendelea kuwa waziri.

Kwa maneno mengine, yeye kuendelea kuwa waziri,. sasa kunamgharimu kisiasa Bosi wake jambo ambalo sidhani kama Mama ataendelea kulivumilia. Hivyo, ni swala la muda tu kabla hajaondolewa na mtihani pekee kwa Mama anamuondoaje au anamuondoa katika mazingira gani.

Katika siasa, hata kama hujatenda kosa lolote, ila ikatokea umma unakuunyoshea kidole au kutajwatajwa mara nyingi kwa mambo yasiyopendeza, basi uwajibikaji wa kisiasa huwa haukwepiki ama kwa kuwajibika mwenyewe kwa kujiuzulu nafasi yako, au kusubiri kuonddolewa na Mamlaka yako ya kinidhamu.

Japo hapa Bongo na Afrika kwa ujumla utamaduni huu haijazoeleka sana, ila tartatibu tunaanza kuzoea na mifano teyari iko mingi na hapa kwetu yameshatokea hivyo Mwigulu is the next whether ana hatia au laa.

Bashite is a good example japo ilichukukuwa muda.

Time will tell.
Waziri wa Fedha analalamikiwa kwa sababu ya tozo mpya ambazo hupelekwa Bungeni kama mswaada na hupitishwa na Rais kuwa Sheria.
Kwahiyo kama Mh. Rais atamuondolea au kumbadilishia wizara basi itakuwa ni kwa sababu nyingine na sio Tozo za serikali.
 
Na kauli za kuhamia Burundi ni sawa ?
 
Kwa kelele zilivyo nyingi na wala hazikomi,hakika ataondolewa au atabadilishiwa wizara.Makamba na Nnape,kelele dhidi yao,zinaibuka na kupotea,kwahiyo wao wanayo bahati,ila Mwugulu,Mmmh... hatapona,lazima aonje hicho kikombe cha kuondolewa au kubadilishwa.
 
KICHWA CHA HABARI kiko sawa✓
HOJA ZA HABARI haziko sawa×

Mamla yoyote duniani haimuachishi mtu kazi kwa kusemwa Sana na Jamii. Humuachisha kazi mtu kwa kutokuwa na MASILAHI nae.
 
Kwani maamuzi anayofanya yanaanzia kwa boss wake? If Yes, hakutokuwa na UMUHIMU kumtoa Ili Hali tozo zipo palepale
Inashangaza sana mijitu inakomaa na Mwigulu,ambaye anafuata tu maelekezo ya Rais,watu inabid wakomae na samia mwenyewe badala ya Mwigulu..halafu wanatishia eti watamtoa 2025..kwa Tume ipi ya Uchaguzi? Ambayo Rais ndo huwateua watendaji wake?
 
Hata kama Mama anampenda au bado ana imani na Mwigulu, ni vigumu sana kuendelea kumbakiza katika nafasi yake kutokana na reaction ya umma kwani anaonekana kuwa ni waziri anaengoza kwa kulaumiwa na kutuhumia na hivyo anakosa sifa ya kisiasa ya kuendelea kuwa waziri.

Kwa maneno mengine, yeye kuendelea kuwa waziri,. sasa kunamgharimu kisiasa Bosi wake jambo ambalo sidhani kama Mama ataendelea kulivumilia. Hivyo, ni swala la muda tu kabla hajaondolewa na mtihani pekee kwa Mama anamuondoaje au anamuondoa katika mazingira gani.

Katika siasa, hata kama hujatenda kosa lolote, ila ikatokea umma unakuunyoshea kidole au kutajwatajwa mara nyingi kwa mambo yasiyopendeza, basi uwajibikaji wa kisiasa huwa haukwepiki ama kwa kuwajibika mwenyewe kwa kujiuzulu nafasi yako, au kusubiri kuonddolewa na Mamlaka yako ya kinidhamu.

Japo hapa Bongo na Afrika kwa ujumla utamaduni huu haijazoeleka sana, ila tartatibu tunaanza kuzoea na mifano teyari iko mingi na hapa kwetu yameshatokea hivyo Mwigulu is the next whether ana hatia au laa.

Bashite is a good example japo ilichukukuwa muda.

Time will tell.
#achawivu #tafutahela #ageisjustanamba #chapakazi #majungusimtaji
 
Akiondolewa Watanzania watakuwa wametendewa haki sana. Hakuna uongozi kabisa kwa mwiguru nchemba. Kwa rasimali zote hizi tulizonazo,bado mwiguru anajiona mbunifu kuwafanya wananchi ndio chanzo cha mapato
 
Back
Top Bottom