Utabiri: Weekend hii Simba na Yanga zote zitafungwa huko katika mechi zao za kimataifa

Utabiri: Weekend hii Simba na Yanga zote zitafungwa huko katika mechi zao za kimataifa

Simba watashinda kwasabau ifuatayo-

Simba walikua na mechi za kujipima nguvu maandalizi ya cafcl timu kubwa tofauti tofauti.View attachment 2511442
,,,,,,,,,,,,👆

wakati huo wapinzani wao Horoya awakua na mechi yoyote tangia walipocheza mechi ya mwisho ya ligi ya Guine tarehe 21 January.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Simba atashinda 1 bila majibu,Yanga atapoteza 2 nunge tunzeni huu utabiri.
Nani atunze utabiri wa ki-zuwena! Vibonde wa kundi Simba Wako njiani tayari wanarudi wamevunjika guu wamepigwa kama Ngoma huko Guinea! Tena Ilitakiwa wale tatu bila lile goli la kichwa walilokosa Horoya na penati yao aliyopangua Manula!

Tunatunza utabiri za maana kuwa Yanga itabeba ndoo ya shirikisho na Musonda ataua waarabu kwao!

Simba haikubeba ubingwa wa ligi eti iko ligi ya klabu bingwa , my foot. Msimu huu Simba mbovu ya kina Boko kapiga nje goli la wazi Zuwena fc watatia aibu sana Africa maana watapigwa mechi zote kama Ngoma!
 
One Day kama Kamsemo ka One Day Yes yaani Mwenyewe Unajionea Huruma kabla Hujahurumiwa
Haya Zuwena fc njoo utuoneshe ushindi wenu dhidi ya Horoya! Makolo Mmepigwa kama Ngoma mnatia huruma mechi nzima mlikaa kimya kwenye vibanda umiza tunaoropoka na kupayuka ni Yanga tu!!

Sisi Yanga ni unbeaten team popote tunapiga boli la kisasa hatuhitaji sijui huruma zako hata sielewi your comment! Huruma my foot!
 
Nashauri msiojua mpira muwe mnakaa kimya
Baada ya Mnyama kukaa mkao WA kuliwa na kupigwa kimoja Cha nguruwe Nimeitafuta sana hii comment yako hadi nikaipata.

Yani mi nitabiri nawewe utabiri huo hautakuwa utabiri Bali ramli!

Mi nakuzidi mbali sana kimpira Mkuu sema hunijui tu. Kuanzia Leo mi nikiwa naongea kuhusu nani atapumuliwa uwe unakaa kimya na kupiga makofi.

That time Uliniboa sana we jamaa kwa comment ya kijinga hadi nikaenda kwa mganga kukucheki kama ni askari au bwana jela mwenyewe kabisa maana Si Kwa amri hiyo!!

Kuanzia Leo nikisema Simba atapasuka ukubali na kutulia dawa na sindano viingie sawia sawa Zuwena?
Wewe ni nani wa kunifunga mdomo. Unatumia mamlaka gani? Maana mwendazake kalala!

Wakati mechi inapigwa Horoya vs Simba nilikuwa nimekaa pale naku-zoom tu nasubiri Simba Zuwena fc wapigwe kama Ngoma niruke ruke na kweli yakatimia! Jamaa wakapiga kimoja tu Cha nguruwe watoto mia nane! Kimoja kinauma asikwambie mtu!!

We jamaa wa Zuwena fc ni mbumbumbu kweli kweli. Yani timu Ina Boko na Kibu mshinde ugenini?

Hivi we jamaa ni WA kunishinda Mimi Mr Zuga akili za kujua mpira kweli?

Kisa tu Mimi ni utopolo?

Ujue Nina uchungu Mi nimebeba viatu vya wachezaji Ili kuingia uwanjani Bure kuiona Yanga ikicheza live nikiwa na miaka sita na Leo hii Nina mvi kwa mbaaali!

Hivi uliona wapi timu mbovu ikashinda?

Hivi we mbwiga Bado tu huukubali mziki wa Yanga ? we jamaa ukapimwe akili. Hivi huoni jinsi Yanga tunapossess ball. Hivi unaJua kama Al Hilal wasingejiangusha dkk 60 nzima tungewaua kwao na kuwepo klabu bingwa na nilitabiri Al Hilal watafungwa mechi zote za makundi na tayari washapigwa mechi moja Jana na Mamelodi Sundown, wale uwezo wao na Zuwena fc hawachekani!!

Jana kocha wa Simba sijui jina lake na Mgunda walitia huruma sana niliona walijikunyata kama vifaranga walionyeshewa mvua Huku mama kuku akiwa ameshachinjwa kitoweo Cha sikukuu ya krismasi. yaani walionesha hawana uwezo kabisa wa kuusoma na kubadili mfumo kama ilivyo kwa Professa Nabi. Ila pia Simba hawana kikosi kipana ni kina Kibu na Boko umemaliza!! Jana Simba wachezaji wengi first eleven walikula Kadi za njano nyingi sana kwa kushindwa mziki wa Horoya sasa mechi zao zijazo za klabu bingwa ni za kina Israel Mwenda na Gadiel Michael! Simba kweli mbovu this time! Hivi Raja wamepiga mtu tano bila wakija Kwa Mkapa Simba asipopasuka mi nahamia Zuwena na kama kawaida nitakuwa nimekaa paleeee nawa-zoom tu Simba na kuwazomea!! Masimba hayo hayajui mpira promo kibaoooo Dunia nzima spika za matangazo kuuuuubwa huku Mpira hamna!!

Chama na Phiri mechi zao kwa Mkapa tu ugenini ni makapi tu! Mabua! Hawana maajabu!!

Sisi utopolo sote tumebukua madarasa ya kutosha umri wa mtu mzima tunatabiri kwa facts sio ushabiki , Yanga haijafungwa mechi nyingi sana hivyo Ina maana ukuta wake ni imara Simba inapigwa pigwa tu kama Ngoma ndo kigezo nilichotumia. Hakuna mwanayanga ambae hajaenda shule!

Halafu mbona kama naona vijana hawavai Tena jezi za Simba mitaani nowadays? Wanaona aibu kuwa mashabiki wa Zuwena fc? Au Mimi ndo sijui Nini kimetokea? Miaka nyuma kidogo 2020 jezi za Simba ilikuwa ndo vazi la taifa ! kweli Nabi kiboko ya Makolo fc!! Jezi za Simba eti Leo zimekuwa mbaya mara zimekuwa nzito na eti ukivaa unasikia joto kali sana hata uwe umejificha ndani ya friza!! Mikia mayowe hayataisha kwa five years ni Yanga tu!!

Haya sasa Zuwena fc mshaharibu timu mbovu kina Kibu na Boko na Zimbwe rudini home kwenu bongo Buza kwa Mpalangers mtulie na mshatia hasara ya kulipa mabilioni ya kambi Dubai! Timu mbovu hata uipe mechi ya kujipima nguvu na Brazil na Real Madrid watapigwa tu. Dubai my foot!!

Leo wanaume Yanga ndo tunacheza huko Kwa waarabu mbumbumbu Zuwena fc wote njooni vibanda umiza muwazomee Aziz Ki na Musonda! Yanga Tunaua mtu Leo sisi sio Zuwena fc Boko Jana Horoya apewe nini yeye na goli kapiga nje njoo huku Sasa Namungo vs Yanga Dida akabutua mpira ukamfikia Aziz Ki, usijisumbue we kaangalie kwenye nyavu tu!
 
Simba atakufa 1-0 wakati Yanga atakufa 3-0.

Huu ndio utabiri wangu kuelekea ufunguzi wa mechi za ligi ya mabingwa pamoja na shirikisho Afrika kwa ngazi ya makundi. Simba na Yanga watapoteza mechi zao za ufunguzi wakiwa ugenini...

Tupia na wako...
Duuuh[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Simba atakufa 1-0 wakati Yanga atakufa 3-0.

Huu ndio utabiri wangu kuelekea ufunguzi wa mechi za ligi ya mabingwa pamoja na shirikisho Afrika kwa ngazi ya makundi. Simba na Yanga watapoteza mechi zao za ufunguzi wakiwa ugenini...

Tupia na wako...
Dah wale wa tunis ,huu uzi watauchukia
 
Simba atakufa 1-0 wakati Yanga atakufa 3-0.

Huu ndio utabiri wangu kuelekea ufunguzi wa mechi za ligi ya mabingwa pamoja na shirikisho Afrika kwa ngazi ya makundi. Simba na Yanga watapoteza mechi zao za ufunguzi wakiwa ugenini...

Tupia na wako...
Duh!...
 
Simba atakufa 1-0 wakati Yanga atakufa 3-0.

Huu ndio utabiri wangu kuelekea ufunguzi wa mechi za ligi ya mabingwa pamoja na shirikisho Afrika kwa ngazi ya makundi. Simba na Yanga watapoteza mechi zao za ufunguzi wakiwa ugenini...

Tupia na wako...
Mpaka dakika hii ya 15 Yanga amekula 2 bila..limebaki 1 tu utabiri utimie
 
Back
Top Bottom