Utafiti wangu: Watoto wa kati kati katika uzao wamejaa matukio sana

Hilo lipo na kumewahi kuwapo na nadharia nyingi (oral narratives) kwamba watoto wa katikati huwa tangu kuzaliwa kwao ni kwa mapambano. e.g.
1. Mtoto wa pili anapambana na mtoto wa kwanza (First born) ili aweze kupata haki yake ya kunyonya maziwa ya mama yake. Kumbuka inavyokuwa changamoto kumwachisha mtoto ziwa. Kwa mantiki hiyo mtoto wa pili anajitahidi kumfurusha First born kutoka kifuani mwa mama. Mama anakuwa kwenye dilema ya kuonesha upendo sawa kwa wote wawili anaegemea upande wa Kipya kinyemi. Lakini wakati huo-huo First born naye anataka atambulike uwepo wake. Unaweza kuliona hilo pale First born anapomng'ata Second Born.
2. Katika uzao wa mama huyo, uzazi wa kwanza i.e. First born mama huyo alikuwa na muhemko sana kuuona uzazi wake na pengine kuonesha jamii kwamba yy ni mama. Wamama wengine hufikia hatua na kutaka waitwe kwa jina la mtoto e.g. mama Y. ilhali jina lake halisi la huyo mama ni Letiaeli.
3. Mtoto wa kwanza huwa anapata upendo mkubwa sana mara tu baada ya kuzaliwa na katika malezi siku za mwanzo-lakini anapokuja mtoto wa pili pupendo huo hupungua na huhamia kwa yule wa pili. Mtoto wa pili hureact kwa kulia, kujizaragaza na kukasirika sana na wakati mwingine kung'ata ziwa la mama yake kama vile kutoa adhabu. Hawa wanakuwaga washari sana.
4. Watoto wa mwisho (Vitinda mimba) hupata upendo uliobaki kwa mama mzazi kwani wamama wengi wanajijua wakifika mwisho wa uwezo wa kuzaa. Kwa mantiki hiyo watoto vitinda mimba wanakombeleza ile albaki yote ya upendo kutoka kwa mama. Hawa kwa kupata aina maalum ya upendo huwa wanadeka sana, wanapenda kupetiwa-petiwa. Ni wenye viburi na wanajiona ni special zaidi.
 
Kama Kuna ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…