Utafiti Wangu: Watoto wengi hupenda zaidi ndugu upande wa mama kuliko upande wa baba

Wanaume kubambikiwa mtoto ni a million times common kuliko mama kubadilishiwa mtoto wake.!!
Hakuna mwanaume anayebambikiziwa mtoto. Watoto wote wanaozaliwa na mwanamke uliyemlipia mahari hao ni watoto wako.
 
Kichwa kigumu bro. mtoto wa dada yako ni mpwa wako, hawezi tokea mtoto wa kumzaa wa dada yako asiwe wake.
Alichokiandika umekielewa lakini?

Hii mada haihusu wapwa inahusu upande wa baba na wa mama. Yeye kasema upande wa baba unaweza kuta baba wakubwa au wadogo wana watoto ila sio wao kiuhalisia hivyo wasiwe ndugu zako wa damu moja. Ndio nikamuuliza huko kwa mama una uhakika gani kuwa watoto wa wajomba ni wao?
 
Mtoto wa mjomba sio sawa na mtoto wa mamdogo/mkubwa.
Mtoto wa mjomba sawa na wa kaka/bamdogo.
Inaweza kuwa mbuzi kwenye gunia tu
Kama ni hivyo, kwa baba kuna mashangazi, ambao pia watoto wao ni damu ya babu yako..
 
Ila kweli..hata sisi tupo na ukaribu mkubwa Sana na ndugu wa upande wa mama kuliko wa baba.
 
Upande wa mume siku zote wana gubu..mashangazi, baba wadogo.
 
Upande wa mama lazima upendwe kwasababu upande wa mama huwa una uhakika wa damu yao mtoto ni wao sababu binti yao ndie amemleta mtoto.

Ila upande wa kiume huwa ni ngumu kuwakubali watoto sababu kuna kesi za kubambikiwa ujauzito na hiyo inaleta utata......

Huwa inawachukua muda sana familia ya mwanaume kukubali kijana wao ndie baba halisi wa mtoto aliyezaliwa.

Mimi mwenyewe watoto wa dada yangu na mdogo wangu nipo nao karibu zaidi kuliko watoto wa kaka zangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mwanamke ulimlipia mahari, basi watoto wote atakaowazaa hao ni wako mzee baba.
 
Kama umeoa msichana, kazi kwako.
Lakini Kama umeoa mke, huyo unaedai kaweka mbegu, ameweka lini.
Na Nani ana ujasiri wa kujitangaza kwamba yeye Ni mwizi.
Je, unafahamu kuwa Ni kosa la jinai kutembea na mke wa mtu?
Kama hujui Basi zaa na mke wa mtu halafu dai mtoto..utauona Moto wake..
 
Aliyelipa mahari ya mwanamke ndio baba wa mtoto/watoto wote. U-baba ni malezi mkuu na sio kumpa mwanamke mimba pekee. Unajuaje kama huyo unayemuita baba tangia udogoni ndio baba yako mzazi?...
 
Mbona hili swali umelikwepa kujibu.

Unajuaje kama huyo unayemuita baba tangia udogoni ndio baba yako mzazi?
 
We Ni mjinga Kama mke wa Ayubu.
Wewe mwenyewe na Kila mtu hapa amekiri kwamba hakuna uhakika kwamba watoto ni halali kwa baba zao, Kama jinsi ilivyo kwamba wewe si halali kwa baba
Yako.
Pamoja na ukweli wote huo ambao hata wewe unaukubali, Bado watoto Hawa wanaendelea kulelewa na hao mababa wasioaminika kuwa wao mpaka wanatenganishwa na kifo.
Baba zao wa DNA wapo wapi?
Kwanini wasiende kuwachukua?
Kwanini baba yako halali haji kukuchukuwa?
Umeshasikia mara ngapi mtu kaenda kudai mtoto kwenye ndoa ya watu?
Niseme tu kwamba , ubaba Ni zaidi ya DNA, au kumlipia mahali mama.
Ubaba Ni responsibilities.
Responsibilities ndizo zinamfanya mtoto akutambue kuwa wewe Ni baba.
Katika Hali yoyote, Kama mtoto hajakutambua wewe kuwa Ni baba yake, huna lako hapo.
Utaitwa tu kuwa wewe Ni baba yake lakini moyoni mwake haumo, hakusikilizi , hakutii, hakuheshimu, hata ukiwa na shida au ukizeeka , Hana muda na wewe.
Endelea kulilia DNA , wenzako tunawajibika kwa watoto hata wa ku adapt, na wanakuwa wetu.
Tuna wa menta wanakuwa vile tunavyotaka wawe.
Ni furaha ilioje, kuliko kuwa na litoto la kibaolojia ambalo Kila siku linakuhuzunisha na kukutia uchungu.
 
Good
 
Daaah umefunguka sana mzee baba. Umemchana huyo mtoto mdogo asiyejua nini maana ya maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…