Utajiri wa Diamond Platinumz wafikia Billion 8.6 za Kitanzania

Utajiri wa Diamond Platinumz wafikia Billion 8.6 za Kitanzania

Huo utajiri una manufaa gani kwenye nchi iliyo top five ya nchi maskini duniani????
Samahani blaza hizo takwimu umezipata wapi.? Punguza Porojo blaza

Below is the List of Poorest Countries in Africa
1. Mali- GDP Per Capita: $715

2. Sierra Leone- GDP Per Capita:$679

3. Togo- GDP Per Capita: $636

4. Eritrea- GDP Per Capita: $544
5. Ethiopia- GDP Per Capita: $505

6. Madagascar- GDP Per Capita: $463

7. Democratic Republic of Congo – GDP Per Capita: $484

8. Liberia- GDP Per Capita: $454

9. 4 . Niger- GDP Per Capita: $415

10. Central African Republic- GDP Per Capita: $333

11. Burundi- GDP Per Capita:$267

12. Malawi- GDP Per Capita: $226
 
Ingawa mziki wetu haujawa structured kuonyesha jinsi msanii anavyoingiza ela lkn kwa diamond platnumz naweza amini, alafu kile kituo nikituo kikubwa ukiona hivyo wamefanya mpaka research, mmesahau juzi juzi tu Forbes Kuna dada mmoja mtz atatengeneza vipodozi asilia Forbes kwanza wanaamini ni bilionea alafu wanamkadiria baada ya miaka 20 ataingiza dola 200m kwa hiyo yote yanawezekana "ombeni mtapewa, tafuteni mtapata". Alafu Kuna wengine huku wanaponda ukiwafuatilia kutwa kukaa vijiweni kula kulala kwa shemeji tena kwenye vyumba virefu (ukumbini) , tubadirike vijana tuache chuki, kijana umewajaza watu unaowachukia mioyoni, hata ukiomba nn mungu hawezi kukusaidia kwani MUNGU NI PENDO tuache uvivu, Wivu wa kijinga na tufight alafu utaona output yake vijana tunazidiwa mpaka na wazee kutwa kupiga majungu plus fitina kumuona mtu hafai.
 
Wewe unayempinga ndio utuambie sisi,kwa jinsi unavyovijua anavyomiliki ndio sababu unapinga lakini kumbe wewe unapinga bila kuwa na ushahidi wa unachokipinga ????
hivi unaijua pesa inayo ongelewa hapa au unataka kubishana
 
Hivi unaweza kutuambia sababu ya kuongea maneno makali kiasi hiko ni ipi, hii ya bil 8 au ........ hapa tunalumbana kwa hoja si matusi.



Maneno makali ndo yapi??

Huyo mnaemuita domo hana ujanja wa kuwa hata na mil 1

Labda izo bilioni 8.6 za kuchapisha tandale
 
Umetajataja mi-namba kibao lakini hoja ziro, kwa jinsi ulivyoandika inaonyesha kuwa unadhani anamiliki bil 8 basi zipo cash benki/nyumbani na pia kwa jinsi unavyoonyesha uelewa wako ni kuwa hazifanyii kitu zipo tu anazichungulia hakuna alichowekeza si ndio ............. halafu hapo kwenye gari kutembelea miaka mitatu ndio ungejiuliza kwenye hiyo mi-namba yako ulizoziorodhesha kazifanyia nini kama gari anaitumia kwa miaka mitatu sasa ?????



Dada mbona unatokwa povu jingi sana kwa maisha ya mtu mwingine??
 
Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani.

Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6.

Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber.

Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo ya mirabaha kutoka nchi za jirani kama Kenya bila kusahau biashara za mtandaoni zikiwemo Youtube.

Uwekezaji wake kwenye label ya WCB ni kitu kingine kikubwa ambacho kitaanza kumuingizia fedha nyingi siku za usoni. Hadi sasa amesaini wasanii wanne wakiwemo Rich Mavoko, Raymond, Harmonize na dada yake Queen Darleen.

Lakini pia staa huyo anafahamika kwa kuwekeza zaidi fedha kwenye ardhi na nyumba huku akidaiwa kumiliki maeneo mengi jijini Dar es Salaam.



Wala sio mda mrefu ata anza kupitisha bakuli la kwenda India kwenye matibabu
 
Kama ni habari za kweli huo ni utajiri wake, sio wa Watanzania jamani mbona wagumu kuelewa?
Kwa hiyo ukiwa wake nchi/ hainufaiki???

Kuna haja gani ya kuwa na billions of money wakati mzazi wako akiwa mgonjwa humkumbuki????
 
Nimepitia posts za watu wengi humu jamii, lakini kijana umebarikiwa roho mbaya kupita kiasi. Inaonyesha hufurahishwi hata kidogo na maendeleo ya nduguzo wa damu kwa hoja hizo hizo.

Hakika wewe ni mtu mbaya sana.
Hahahaha mkuu maneno makali sana
 
Back
Top Bottom