Utajiri wa Diamond Platinumz wafikia Billion 8.6 za Kitanzania

Utajiri wa Diamond Platinumz wafikia Billion 8.6 za Kitanzania

Huo utajiri una manufaa gani kwenye nchi iliyo top five ya nchi maskini duniani????
Umaskini wa nchi unamhusu nini,yeye ni mojawapo ya raia wachache wanaopambana na umaskini kwa dhati,wakati waliobaki wanapoteza muda kupambana nae!
 

Diamond anakadiriwa kuwa na utajiri wa dola milioni 4 mpaka sasa ambayo n sawa na shilingi bilioni 8.6 za kitanzania
 
kuna mada zinaendelea hapa jukwaan kuhusu utajir wa mwanamuziki Diamond ni Tshs bil 8. Sina nia ya kupinga ila tujadili kwa facts kama Great Thinker.
...........
Kumekuwepo na tetesi nyingi kuhusu utajiri wa Diamond umefikia kiasi gani. Hilo ni swali ambalo hajawahi kulijibu kwa uhakika zaidi ya kutoa tu hints na kuwaacha wanaouliza kubaki na majibu yao wenyewe vichwani.
Lakini kupitia kipindi maalum cha kituo cha runinga cha E!TV, E Vip kilichorushwa Jumapili ya June 26, tunaweza kusema walau kwa uhakika staa huyo ana utajiri mkubwa kiasi gani. Diamond ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani ambao kwa shilingi ya Tanzania ni zaidi ya bilioni 8.6.

Si kitu kinachoshangaza tena kwa Diamond kutokana na hatua aliyofikia akiwa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi Tanzania kwa sasa. Fedha zake nyingi zinatokana na show zake zisizokauka za ndani na nje ya nchi, mikataba ya ubalozi na matangazo kutoka makampuni kama Vodacom, Cocacola, DSTV na Red Gold. Hivi karibuni alipata deal jingine la kutangaza huduma ya taxi ya Uber.

Pia amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia biashara ya nyimbo zake hasa miito ya simu, malipo ya mirabaha kutoka nchi za jirani kama Kenya bila kusahau biashara za mtandaoni zikiwemo Youtube.

Uwekezaji wake kwenye label ya WCB ni kitu kingine kikubwa ambacho kitaanza kumuingizia fedha nyingi siku za usoni. Hadi sasa amesaini wasanii wanne wakiwemo Rich Mavoko, Raymond, Harmonize na dada yake Queen Darleen.

Lakini pia staa huyo anafahamika kwa kuwekeza zaidi fedha kwenye ardhi na nyumba huku akidaiwa kumiliki maeneo mengi jijini Dar es Salaam.
............
baadhi ya michango ya wadau

1.Kuna watu wanadhani billioni ni kitu rahisi sana kuwa nacho achana na hiyo billion 8 wanayodanganya nayo....Show moja Diamond akiwa nje ya nchi analipwa Million 50.. Tufanye anafanya show nje ya nchi week zote 52 za mwaka, hiyo ni Billion 2.5 kwa mwaka, tufanye kafanya hizo show miaka miwili mfululizo inatupa Billion 5..

Anasema Vodacom walimpa Million 800, DSTV nao tufanye Million 100, Uber Million 100, Tomato Million 100, Caller tunes Billion 1.. Hapo Jumla tunapata Billion 7.1.. Na hapo hatujaweka matumizi yoyote.. Sasa hizo billion 8.6 katolea wapi.. Billion kuimiliki msifikiri mchezo.. Angekuwa anamiliki Billion 8 asingetembelea kile kigari kwa miaka mitatu sasa

2.Sio kila mtu anayekupinga anakuchukia.. Mjifunze hilo kwanza, Billion 8 bakini mkiziongelea ila hiyo pesa huyo dogo hana.. Billion 8 angekaa kwenye nyumba kama ile uko porini?? Umeona nyumba na magari wanayopush yule dogo mnaija wa 5 star music?? Mtu ana ki BMW hajakibadilisha mwaka wa tatu huu na nyumba ya kawaida kabisa inaitwa Ikulu alafu mnadanganya ana Billion 8.

3.Kwa asie jua pesa ana dhani billion ni pesa ya masihara lkn swali linakuja je, mziki unalipa kiasi hicho? ana assets zipi japo za billion 2?

4 kama mziki unalipa kwa nn kuna utofauti Mkubwa sana wa kimapato kati yake na wanamziki wengine?maana hakuna mwanamziki mwingine aliyefikisha bil 2.

5. kwa pesa hizo asingekaa huko porini Madale angetafuta mjengo masaki, mikocheni, mbezi beach au sinza( hapa naongelea msanii)

....Wadau kutiririke
 
Kwa hiyo ukiwa na pesa ni lazima ukae mbezi beach,masaki na mikocheni? We jamaa Una arguments za hovyo kweli kweli...[emoji57]

simpo logic huwezi kuwa na hela ukakaa porini, what is good for him angalau anakaa hom kwake tofauti na wale magumash wengine wanaopanga afu wanasema kwao
 
Kwa hiyo ukiwa na pesa ni lazima ukae mbezi beach,masaki na mikocheni? We jamaa Una arguments za hovyo kweli kweli...[emoji57]
simply wasanii wanapenda show off.. kama kweli anahela asingekaa madale !!! cha kimpongeza ni kuwa anamklkki nyumba ila la bil 8 tupa kule
 
Umaskini wa nchi unamhusu nini,yeye ni mojawapo ya raia wachache wanaopambana na umaskini kwa dhati,wakati waliobaki wanapoteza muda kupambana nae!
Ina maana hautuhusu si ndio? kama hautuhusu hii habari imefwata nini hapa?
 
We nae sijui wa wapi...Yani uwe ata na a billion alafu unakaa tandale kwa Tumbe si utakua hamnazo.Hewa yenyewe pale ya kugombania kama mpira wa kona..
ahahahah kama una bil 8 ina maana unaweza kununia nyumba ya mil 300 maeneo mazuri ukizingatia yeye ni msanii!!!! sio madale
 
Back
Top Bottom