Utajuaje kama huyu amefariki kwa mpango wa Mungu au kwa Ushirikina?

Utajuaje kama huyu amefariki kwa mpango wa Mungu au kwa Ushirikina?

Katika jamii zetu, kumekuwa na mijadala ya hapa na pale, kuhusu vifo vya binadamu.

Kuna wengine watasema, huyu amekufa kutokana na mpango wa Mungu, na wengine watasema yule amekufa pasipo mpango wa Mungu (kishirikina).

Sasa wakuu, nataka kujua; Utajuaje kama huyu amefariki kwa mpango wa Mungu au kwa Ushirikina?​
Ushirikina Mara nyingi ni WA kuzuia tu maendeleo, na Wala hauleti maendeleo kwa wanaoufanya, ila hapo kweny kifo Cha Mpango wa Mungu na ushirikina nahic mpaka mtu awe na macho ya Roho ndio anaweza jua
 
Sawa mkuu japo jiulize na wewe kwanini haufanyi sehemu fulani lakini kuna sehemu unafanya kazi tena vizuri mno hapo vipi mkuu

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Kwamba maeneo fulani haufanyi kazi? Ndiyo sababu yule jaji Kanda ya iringa katengua Ile hukumu ya njombe bila mfungwa kukata rufaa.
 
Matukio tu yatakuonyesha

Anaenda hospital anapigwa msako wa ugonjwa mwili mzima hospital zaidi ya moja vipimo vinasoma haumwi chochote, ikifika hatua hio chukua hatua madhubuti soon bundi akaa juu ya paa la nyumba yako
 
Hapo ndipo watu wengi wanakwama sasa... hapo ndipo utaona tofauti kati ya waafrika na wazungu. Wao mgonjwa akipata ugonjwa wasioutambua watafanya uchunguzi mpaka wajue ni ugonjwa gani, na waupatie tiba.

Ila sisi tunawaza kua mtu karogwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matukio tu yatakuonyesha

Anaenda hospital anapigwa msako wa ugonjwa mwili mzima hospital zaidi ya moja vipimo vinasoma haumwi chochote, ikifika hatua hio chukua hatua madhubuti soon bundi akaa juu ya paa la nyumba yako
Ikitokea amefariki, utagunduaje?
 
Ikitokea amefariki, utagunduaje?
Nmekwambia matukio yanayomkabiri utaelewa chanzo cha yote ni nini aidha anapigwa risasi za urogo ghafla anakufa au kwenye mtiririko wa matukio yaan anakufa pole pole kwa ugonjwa usioonekana
 
Ilimradi kafa na kila mtu atakufa hamna haja ya kutafuta sababu maana hutamrudisha..
 
Kifo sio mpango wa Mungu wala hafurahii watu wanapokufa..

Eze 18:32 “‘Mimi sifurahii kifo cha mtu yeyote,’ asema Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova. ‘Kwa hiyo geukeni na kuishi.’”
 
Back
Top Bottom