Utajuaje kama huyu amefariki kwa mpango wa Mungu au kwa Ushirikina?

Utajuaje kama huyu amefariki kwa mpango wa Mungu au kwa Ushirikina?

Sijajua, kama kufanyiwa uchunguzi hospitali, kwa macho yetu haya ya nyama, tunaweza kutoa majibu tofauti.
Mkuu Hospital ndio bora zaidi ila wengi wanaofia nyumbani huwa hatujui kama wamekufa vifo vya kawaida au wametolewa roho kwa nguvu

Kuna wakati jamaa yetu alifariki ghafla akiwa amekaa na wenzake huko uarabuni
Wakaita ambulance (lazima) Dr akatoka baada ya kumuona marehemu na kuwaukiza amepatwa na nini wakasema kaanguka tu
Dr alipiga simu police walikuja wakabebwa wote 6 na kutupwa jela
Walikaa masaa 9 huku wakimlilia marehemu

Baadae majibu yakafika kuwa ilikuwa ni heart attack wakaachiwa huru na kumzika mwenzao

Wenzetu wanajali sana uhalisia na ulweli kuliko kusikia vilio tu
 
Cc: mhandisi uchwara Eng. Zezudu
Eng. Zezudu , hata wazungu zamani walikuwa wanaamini ushirikina, kama ambavyo shinyanga wanaamini mwenye macho mekundu ndio mchawi, wazungu waliamini mwenye pua ndefu iliyopinda ndio mchawi.

Wazungu waliupiga vita kwa dhati ujinga huu, ukapotea. Wazungu wanaoamini ushirikina ni wachache mno.

Sisi huku Afrika, wachache tunaoujua ukweli huu, hatutaki kuwafumbua macho nyie, maana ndipo tunapotajirikia. Ujinga wenu wa kuamini uchawi na kwenda kwa mganga, na kuamini miujiza na kwenda kanisani, ndio mtaji wetu. Endeleeni kuamini hivyo hivyo.
 
Mkuu Hospital ndio bora zaidi ila wengi wanaofia nyumbani huwa hatujui kama wamekufa vifo vya kawaida au wametolewa roho kwa nguvu

Kuna wakati jamaa yetu alifariki ghafla akiwa amekaa na wenzake huko uarabuni
Wakaita ambulance (lazima) Dr akatoka baada ya kumuona marehemu na kuwaukiza amepatwa na nini wakasema kaanguka tu
Dr alipiga simu police walikuja wakabebwa wote 6 na kutupwa jela
Walikaa masaa 9 huku wakimlilia marehemu

Baadae majibu yakafika kuwa ilikuwa ni heart attack wakaachiwa huru na kumzika mwenzao

Wenzetu wanajali sana uhalisia na ulweli kuliko kusikia vilio tu
Nakubaliana nawe mkuu, kama ingekuwa ni ushirikina, ingeonekana nini kwenye uchunguzi?
 
Utakuwa umeshindwa kuelewa hoja.

Hoja ni kuwa ushirikina ni chimbuko la ujinga. Muumini katika ushirikina atakuwa na jina lipi basi la kumwakilisha?

Kushindwa kuliita koleo kwa jina lake hakusaidii kitu ndugu.

Koleo ni koleo siyo kijiko kikubwa.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Sikia wanaokataa hakuna ushirikina ndiyo washirikina wenyewe
 
Hakuna kifo cha ushirikina mkuu...ni basi tu jamii zetu zina baadhi ya mambo zinakumbatia hayana maana...mi binafsi siamini kama uchawi upo.
Kusema uchawi haupo ni sawa na kusema shetani hayupo. Shetani yupo na watendakazi wake ni hao wachawi na waganga wa kienyeji. Kusema hakuna uchawi ni kujidanganya nafsi yako. Ni jambo ambalo wala halitokusaidia chochote.

Yesu ni Mwokozi
 
Tena hao wanaokataa ndiyo wafuasi wenyewe washetani.
 
mh unajua tatizo lilianza pale tulipo letewa dini na majahazi kutoka pande zote za dunia sasa zile zilizokua imani na dini zetu now zinaitwa uchawi ila zilitumika na zilifanya maajabu makubwa sana
 
Nakubaliana nawe mkuu, kama ingekuwa ni ushirikina, ingeonekana nini kwenye uchunguzi?
Mkuu kwa kweli haliwezi kujulikana ila unaweza kuwa na doubt kama Egyptians na jinsi wanavyoamini na hata wazungu wanaamini kuwa wengine walirogwa
Ila mimi siamini ingawa najua yapo
Nikiamini maana yake naipa nguvu kuliko Mungu that's what I believe
Screenshot_20220914-175029_Chrome.jpg
Screenshot_20220914-175007_Chrome.jpg
 
kwenye Liturgia ya KKKT kuna ibada ya kifo ktk mazingira yasiyo ya kawaida. mfano ushirikina
Screenshot_20220914-202949.png
 
Back
Top Bottom