Utapeli miamala ya simu: Usikubali malipo kwa simu toka kwa usiyemjua

... umefafanua vizuri sana. Swali, "Lipa kwa X-Pesa" inaruhusiwa kutokea mbali? Kwa mfano nimesafiri, naweza kumtuma kijana akaenda penye huduma ya "Lipa kwa X-Pesa" nikalipa kutokea mbali tofauti na kutolea kwa wakala ambapo hairuhusiwi kutokea mbali?
 
We maamuma kama ulilipwa kwa kwa line yAko ya kawaida na muamala ukawa reversed ni ujinga wako..wafanyabiashara wanaojitambua wanatumia lipa kwa simu kwa kuwa ina usalama...
 
You know what? At least unakuwa pale pale na namba unaiona. Ukikosea tena kutype namba na kuthibitisha jina huna tofauti na aliyetupa pesa kwa makusudi. In short you're not serious na hakuna namna ya kukusaidia zaidi.
LIPA NAMBA hata uwe mafia ukishalipa huwezi rudisha muamala maana kwanza ile ni namba ya malipo hata ukilipa mia tano lazima mfanyabiashara apigiwe kuulizwa kuna mteja X ametutarifu katoa/kalipa kimakosa je ni kweli ukisema sio kweli mteja X anapigiwa na mnaunganishwa,,,hii ishanitokea dukani mara chache mtu anatoa pesa wengine kweli kimakosa unapigiwa ukithitibish basi kwa sasa hivi voda wanakupa wakala option ya kumrejeshea mtej pesa kwenye menu kuna kipengele 1.RUDISHA MUAMALA(hapa unachagua kama ww ndo umetuma kimakosa) 2.MIAMALA ILIYOTOLEWA KIMAKOSA(hapo unakutana na kama kuna mtu katoa kimakosa) kama kweli katoa unauchagua unathibitisha ndo pesa zirudi
 
Yaah hii popote ulipo unalipaa mkuu.....
 
Inaruhusiwa....
 
Mkuu ulipotea wapi? Tumemiss kichiz threads zako za Corona.

Mkuu ya mashabiki wa nyungu nawaona pia hapa. Sasa hivi wao ni wajanja n hawaoni umuhimu wa walio vulnerable kuelimishwa.

Tunapigania vipi mambo ya uhalisia yakiwamo maisha dhidi ya Corona, demokrasia au katiba ya maana na watu kama hawa?

Nimechagua kuwaangalia tokea pembezoni warevu hao kwa muda kwanza.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Chukua hiii elimu bure hapa....maana mimi elimu yangu inaambatana na matusi
 
We maamuma kama ulilipwa kwa kwa line yAko ya kawaida na muamala ukawa reversed ni ujinga wako..wafanyabiashara wanaojitambua wanatumia lipa kwa simu kwa kuwa ina usalama...

Ninakazia: Maamuma ni wewe. Huna ulichoelewa wala unachoelewa.

NB: Kuelimika ni dhana pana. Tatizo lako liko hapo.

Pole sana kwa kutojua kuwa hujui.
 
Hujaweka na ni nini hao Vodacom walichompa jamaa yako mtapeliwa kama ushauri baada ya kuwajulisha habari za wizi.

Zipo namba special kwa ajili ya kupokea hela kama mtu ni mfanyabiashara hela ikiingia aliyekosea au aliyejifanya kukosea akitaka kurudisha muamala akipiga customer care lazima muunganishwe wote ili haki ipate kutendeka,mwaka 2016 kuna jamaa yangu yeye alipigwa 1.7mill na haikurudi akaishia kutafuta waganga wa kumloga jamaa.

Au atafute Lipa Namba,hizi zipo za Vodacom na Tigo.
 
... shukrani. Wafanyabiashara wanasubiri kuchangamkia huduma hiyo (Lipa kwa X-Pesa)? Ila kama ingewezekana kutokea mtandao mmoja ukalipa mtandao mwingine ingekuwa vizuri sana.
Inawezekana...yani mfano lipa ya voda unaweza pokea kutoka mitandao mingine
 
Ninakazia: Maamuma ni wewe. Huna ulichoelewa wala unachoelewa.

NB: Kuelimika ni dhana pana. Tatizo lako liko hapo.

Pole sana kwa kutojua kuwa hujui.
🤣🤣🤣..dogo majibu nnayokupa mimi na voda watakupa hayohayo...
 
Ana lipanamba ama alilipwa kwa namba za kawaisa? Lipanamba muamala haurudi
 
Hapa wewe unakuwa ulipi kwa Mpesa bali UNATUMA pesa kwa Mpesa kama form ya malipo ya biashara iliyofanyika, hizi ni huduma mbili tofauti, ambapo ukilipa kwa Mpesa hakuna uwezekano wa ku reverse malipo!
Ndugu zangu watanzania. Tujifunze kuandika maneno ya lugha yetu kwa ufasaha. Unaweza kutoa maelezo mazuri lakini herufi moja tu ikaharibu sentensi nzima. ''Ulipi'' ina maana gani? Na hapa sizungumzii typo, kosa ambalo mtu yeyote anaweza kulifanya bali nazungumzia kutojua kuandika maneno!
 
Ulijualo wewe ni lipi ndugu? Yamewakuta wengine. Alert inawekwa hapo kukutahadharisha na wewe ukiwamo kabla ya hatari umekomaa. Kwani ujinga ni nini basi?
Wewe ndiye mjinga, kulipa kwa mpesa au tigopesa mtu aweza rudisha muhamala, ndiyo maana kuna suluisho la lipa namba, sasa huoni kama wewe ni mjinga kutumia mpesa badala ya lipa namba
 
Yaani your alert is too obvious. Ni sawa na kuwaambia watu kuwa dawa ya kupaka usiinywe. Nani asiyejua
 
Option ya kurudisha muhamala ni feature nzuri na wala siyo mapungufu. Malipo lipa kwa lipa namba. Pesa tuma kwa mpesa. Period
 
Kwamba unaita uongo bila ya kuwa na ufahamu wowote wa kadhia hii?

Vodacom amekiri tatizo hili ni rampant?

No wonder kuna Tanzania ya viwanda ikijengwa katika awamu fulani.

Bure kabisa!
Ungesema ametumiwa pesa kawaida lakini siyo kwa mfumo wa lipa kwa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…