PreGE2025 Utapeli wa haki mahakamani: Askari kuvaa mask ni ujambazi wa kisheria!

PreGE2025 Utapeli wa haki mahakamani: Askari kuvaa mask ni ujambazi wa kisheria!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sema yule wa juzi kapata msongo wa mawazo mkali sanaa fikiria siri zake zote za binafsi watu wamezianika kama njugu vile? Mpaka anayemkukula mkewe watu wamemtajia aibu gani ile

Sijaona, wameanika wapi Tena?
 
kwa hiyo kupambana na mtu ambaye amefungwa, yupo kwenye kachumba, ndio ukomandoo? mwachie awe nje alafu upambane naye kama wewe mwanaume. hao nao utawaita makombandoo? makomandoo wa indoors?
Indoors? Hujui kuwa kuna wafungwa hatari wakiwa gerezani gereza laweza vamiwa na watu wenye silaha ili wamtoe mtu wao kwa nguvu na kutoroka naye? Unadhani kazi yao kulinda vyumba tu?
 
Indoors? Hujui kuwa kuna wafungwa hatari wakiwa gerezani gereza laweza vamiwa na watu wenye silaha ili wamtoe mtu wao kwa nguvu na kutoroka naye? Unadhani kazi yao kulinda vyumba tu?
wewe utakuwa mwanamke. na haujui maana ya gereza. ukiwa kule ndani hate uwe mbabe namna gani, unaweza kudhibitiwa na mtu ambaye hajaenda hata depo, kwa sababu upo ndani. nini usichoelewa? ndio ujiite mkakamavu unatishia hadi raia mahakamani kwa indoor mababu?
 
Je kuvaa mask ni sheria ya jeshi la Magereza .

Au tangia yule jamaa aliyesemekana kajibizana na Lissu na baadae watu kumuanika ndo sababu na wakamuanika na mke wake na anayemkula mke wake.!?
WAnatii maagizo ya wakubwa, period
 
Katika historia ya mihimili ya dola, mahakama ndiyo taasisi ya mwisho ya utoaji wa haki—lakini leo tunaishuhudia ikigeuzwa jukwaa la uonevu na maigizo ya kisiasa. Ni jambo la kusikitisha na la kuaibisha kuona askari wa serikali wakivamia mahakama wakiwa wamevalia mask kana kwamba wanakwenda kupambana na magaidi, si kuhifadhi amani.

Kitendo cha askari kuvaa mask ndani ya mahakama si tu ni utovu wa nidhamu, bali pia ni ukiukwaji wa wazi wa Kanuni ya 36 ya The Advocates (Professional Conduct and Etiquette) Regulations, GN No. 118 of 2018, pamoja na miongozo ya Jeshi la Polisi kupitia Police General Orders (PGO). Sheria hizi zinamtaka kila mhudhuriaji wa mahakama, hasa maofisa wa dola, kuonesha heshima kwa mavazi rasmi, kuacha vitisho, na kuonesha uso wao hadharani – ishara ya uwazi mbele ya chombo cha haki.

Lakini leo, haki inatapeliwa mchana kweupe! Serikali hii haijifichi tena – imeamua dhahiri kugeuza vyombo vya sheria kuwa vinywaji vya kisasi kisiasa. Askari waliovaa mask si walinzi wa usalama, bali ni watendaji wa hofu na vitisho. Huu ni ujambazi wa kisheria.

Kinachoendelea dhidi ya Tundu Lissu si kesi, bali ni maigizo ya dhuluma yaliyoandaliwa na mfumo kandamizi. Mtu aliyejaribu kuikosoa serikali, kutetea Katiba na kutafuta haki kwa Watanzania sasa anaandamwa na mifumo ya uonevu kana kwamba ni adui wa taifa.

Haki haipatikani kwa bunduki wala kwa mask mahakamani – inapatikana kwa kuheshimu Katiba, sheria na utu wa binadamu. Serikali hii inaitesa haki, inalipaka tope jina la demokrasia, na kuifanya mahakama kuwa chombo cha utapeli wa kisheria.

Tutazame vizuri: hiki si kioo cha haki. Ni kivuli cha udhalimu.
Mbwembwe za kijinga,hapo mshahara wao 450,000 take home, wanadaiwa kausha damu ,marejesho,vicoba,ada za watoto wao,wana njaaa hao,mfano hamna.
Ni wa kuwaonea sana huruma 😅😅😅🤣🤣
 
Screenshot_20250519_200149_1753937672204.jpg
 
Back
Top Bottom