Utapeli wa kuagiza gari Japan


Una deposit slip uliyotumia kuweka pesa CRDB ?

Haiwezi kuishia hapo kizembe namna hiyo.

Una pa kuanzia
 

Ndio nilichomaanisha akiweka taarifa za miamala, itamsaidia kupata pa kuanzia.

Mfano ile nakala ya kuweka pesa kwenye hiyo akaunti hapo CRDB. Hiyo ni uthibitisho na ushahidi muhimu sana.
 
Watu wana nguvu sanaa, mimi ningekuja humuu baada ya mwaka.
Oya mwacheni mshakji, akiona notifications za huu uzi ni kama mnamtonesha..
Watu wa Dar Mtafteni mshkaji Mpeni Bia.
 
NASHUKURU MUNGU SANA NIMEZUNGUMZA NA MKE WANGU NIMEMWAMBIA KILA KITU KILICHOTOKEA AMENIFARIJI SANA TUNAMUOMBA MUNGU ATUPE KUSAMEHE NA WEPESI WA KUBEBA HILI JAMBO,NALICHUKULIA KAMA KUTOA SADAKA MAISHA LAZIMA YAENDELEE.MUNGU AWABARIKI SANA NDUGU ZANGU HUMU JUKWAANI MMENIFARIJI PIA NA NIMEJIFUNZA MAKOSA NI MWALIMU MUNGU ATUBARIKI SOTE.
 
Kama kampuni imesajiliwa brela usikubali matokeo kirahisi hivi. Cha mwanaume hakipotei tu hivi hivi pambana nenda polisi fungua kesi.
 
Hata biblia inakataza huu msimamo inapokuja swala la haki yako.

Kafungue kesi. Askari wagewe authority ya kuona taarifa za aliyefungua akaunt CRDB waone wanampataje.

Ila email ya kibiashara kua na domain gmail au yahoo hiyo siyo kweli. Siku nyingine achana nayo
 
Wawezajwe acha 9M iende kwa mtindo huo? Wengi tupo humu muda huu hatuna 50K na utatuangusha sana ukisema 9M ni sadaka.

This is unfair to us and to your unborn children and your grandchildren
 
Kama umeamua kuiacha...tafuta mtu mwambie aifatilie akiipata 40percnt achikua 60 akurudishie. Unaipata hyo hela..nenda polisi kesi nyepesi hyo
 
Ni kweli kabisa nilifanya uzembe sana,naombeni mnisamehe kwa hilo Mniombee nipite salama kwenye hili pito langu.
Pole sana chief ndo kijifunza hela zinatafutwa.! Tunajifunza kutokana na makosa. 9M sio mbaya sana, utapata zaidi ya hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…