Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Kama Ney wa mitego alitekwa, Dr ulimboka alitekwa na wakamtoa kucha kwanini usiamini na Roma katekwa? Hasa ukizingatia aina ya muziki anaoimba Roma hauwapendezi watawala wa CCM?
Ney alitekwa lini wewe Bawacha?
 
Akili ziro, kama watu binafsi wamemteka, inamaana intellijensia ya vyombo vya ulinzi na usalama ishindwe kujua hao watu na kuwachukulia hatua!.

Tuache ushabiki.
 
Mi nadhan hatupaswi kuegemea upande wowote ule katika kitafuta ukweli wa hili,nadhan kinachotakiwa kufanyika ni juhudi za vyombo vya dola kufanyika kumpata na si tu kufanyika bali zionekane kufanyika.
 
Ni vigumu mtekaji wa kawaida kuicha simu hewani kwani anajua anaweza sakwa kwa kupitia simu!
 
Idd Amin alikuwa kila mwaka anaenda kuhiji na aliitwa Alhaji!!! Lakini alimuua Askofu Mkuu wa Anglikan Janan Luwum!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…