Uzuri hili swali nalo nimelijibu katika maelezo yangu hapo juu na nikauliza swali na kukupa muongozo. Unasema wakristo wanaongozwa na Roho Mtakatifu, ili kujua ukweli ea jambo hilo lazima turudi katika machimbo ya mafundisho ya Ukristo, kwamba ni nani ameyasema hayo. Kama Yesu hakuyasema na hajatoa ishara itabidi watuambie wameyapata wapi. Uongo unaanza kujulikana hapo. Haya mambo marahisi sana.Lakini hapo chini umejibu mfano wangu ambao ulikuwa unaonesha protocols za wakristo kuisoma biblia.
Wewe umedai kuwa hoja ni kua
Shida yenu vijana hamjui kuchimba mambo na kuujua ukweli. Kwanza ili kujua huo ukweli, lazima tujibiwe maswlai kuhusu huyo roho mtakatifu kuwa ni nani na je hiyo kazi kweli anaifanya na kwa mujibu wa nani na hayo mafundisho yametoka wapi ?Sasa hapa ndio tunarudi pale pale je hicho ulichokisoma kwenye biblia kabla ya kukifikiria ni sahihi au lah je ulishushiwa roho mtakatifu wa kukuongoza kusoma hiyo biblia?
Sasa hatukubali tu kuwa kwamba kuna roho mtakatifu, lazima tujue ni kwei yupo na je ni kweli anawatokea watu ?
Tatizo siyo vigezo, tatizo ni misingi iliyo pelekea kuweka hivyo vigezo je nayo misingi hiyo ima kidhi haja ? Marejeo ya misingi hiyo ni wapi ?Lakini endapo utasema hukuhitaji roho mtakatifu basi hapo unakuwa umesha feli kufikia vigezo ambavyo vinapaswa kufuatwa ili kuielewa biblia.
Si kweli hili kwani ukishajua sababu ajabu huondoka. Muujiza ni kimaana ni jambo ambalo limetokea kwa sababu ambazo si za kawaida. Jia hilo. Maana yake tu kwa maana ya dhati ya tamko muujiza ni uhalisia, sasa vipi unautenganisha muujiza na uhalisia ?Kwa mfano jambo lolote ambalo limehusianishwa na muujiza huwa ni ngumu sana kuliweka kwenye uhalisia.
Sasa swali ugumu wa tukio hili ni upi ? Au uongo wa tukio hili unaweza kuuonyesha uko wapi ?Hata wewe kuna habari za Quran zinazosema mtume alipaa angani mpaka mbinguni na farasi aitwaye Buraq (kama nitakuwa sahihi) jambo hilo kwako unaweza ukalirahisha kuwa ni uhalisia kwa dhana ndogo tu ya kusema ni miujiza
Swali la msingi lazima ujue tukio hilo limesimuliwa na nani ? Historia inaongelea vipi tukio hilo, je lilitokea kweli na kama lilitokea kweli uthibitisho uko wapi ? Sasa unaposema ni ngumu hiyo ni ngumu kwako kulingana na ufinyu wa akili yako na maarifa yako ila kiuhalisia si jambo gumu.
Jambo hili halina utata na huwezi kuonyesha utata wa jambo kwa ukweli kama ulivyo, bali akili yako ndogo na maarifa yako juu ya jambo hilo imeshindwa kung'amua jambo hilo, na ndiyo maana jambo hilo lina utata ila kwa hakika halina utata.Lakini leo hii katika ulimwengu swala hilo halielezeki kwa namna yeyote bila kuacha utata na ndio maana muujiza unatumika ku cover gape la kuziba mianya ya maswali magumu kama hayo.
Muujiza ulikuwa unatumika kuwasadikisha watu au kuwafanya watu wasadiki jambo wanalo ambiwa na mitume na manabii wa zama zile, na siyo kwamba muujiza ni kwa ajili ya kucover hayo magap.
Zama hizi miujiza ya Mola haipo tena sababu utume na unabii ushakoma. Kilichobakia zama hizi ni kurejea miujiza iliyo tokea zama za mitume na manabii sababu mambo hayo yamerekodiwa na kuhifadhiwa na yana chain (sanadi).
Kwahiyo hata weww hapo ulipo, mpaka unakufa hutaweza kuonyesha ya kuwa Mtume hakuenda mbinguni, sababu uwezo siyo tu kwamba huna bali huwezi kupingana na uhalisia.