As long as Mwigulu bado yupo kwenye Baraza, naweza kusema hii haitoshi.
Halafu hawa kina Makamba ndio watu pekee wa kuwa mawaziri? Ni kweli wanawazidi wenzao uwezo au ni influence tu za wazazi wao ndio zinawafanya wapate kipaumbele?
Kama si hivyo, basi ni wazi CCM kuna ombwe kubwa la watu wanaofaa kuwa viongozi katika hii nchi.
Watanzania tuendelee kudai Katiba mpya tupate watu wapya kuongoza hii nchi kwani hata hawa walioenguliwa bado kesho wanaweza kurudi tena katika Baraza la Mawaziri.
Chama kilekile, watu walewale (wanaachiana tu viti) na matokeo yake maisha ya watanzania yanabaki kuwa yale yale miaka nenda, miaka rudi.
Pathetic!