Uteuzi na Utenguzi: Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ndalichako aondolewa uwaziri

Ameshushwa cheo na pia amewekwa Arusha kimkakati.
Inawezekana ni kimkakati kweli lakini ajashuhwa cheo wala kupanda ila kaingia serikalini maana katika mfumo wa utawala wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa ni mwakilishi wa Rais katika mkoa na anatekeleza majukumu ya serikali katika ngazi ya mkoa kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Majukumu ya Mkuu wa Mkoa ni pamoja na kuhakikisha utulivu na usalama, kusimamia utekelezaji wa sera za serikali, na kutoa mwelekeo wa juhudi za maendeleo katika mkoa. Ana mamlaka ya kiutawala na kisheria yanayomwezesha kutekeleza majukumu haya.

Tofauti na Mkuu wa Mkoa, Katibu Mwenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa ni kiongozi wa chama ambaye anahusika na kueneza itikadi na sera za chama. Uteuzi wa Makonda kama Mkuu wa Mkoa unamaanisha ameingia moja kwa moja katika uongozi wa serikali, tofauti na wajibu wa Katibu Mwenezi ambaye anahusika zaidi na mambo ya chama.
 
Kashushwa cheo acha ukujipa moyo.sahivi anaenda kupigwa biti na kamati ya siasa ya mkoa na atakua anapeleka taarifa za utekelezaji wa ilani kila robo mwaka.
 
Arusha atakuwa amemtenganisha na DSM, pia watu wa Arusha na morani. Ndali ni kutofautiana na viongozi kuhusu
mitaala Mipya
 
Safi sana Makonda nakuomba ukaokoe vijana wa Arusha, nidhamu ya wale vijana imeharibiwa na madawa ya kulevya hasa mirungi na bangi halafu wao wanaona huo ndio ujanja, naamini hili utaliweza hujawahi shindwa jambo.
 
haha hasa tz huwa nacheka mambo yanavyoendeshwa. nchi haiko serious ni mzaha tu. ningezaliwa mzungu ningebagua sana watu weusi
 
dubwana wapi wanatumia vyombo vya dola. bila hizo apparatus hawana lolote
 
wazee wa tamaa za vyeo na madaraka.
huko sijui ni kuumia au kuteseka πŸ’

wewe unatumwa kwenda kutumikia wananchi, jamaa flani lenye uchu na tamaa ya madaraka limekaa mahali, linatathimini hii nafasi aliyopewa fulani ni ya juu au chini, ndogo au kubwa πŸ’

utumishi ni utumishi tu,
ukitumwa popote unakwenda kwa moyo wote kufanya kazi ya wananchi. Weledi, bidii, maarifa na uchapakazi wako ndicho kifanye wewe kua ni mkubwa au mdogo πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…