Uteuzi na Utenguzi: Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ndalichako aondolewa uwaziri

Uteuzi na Utenguzi: Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ndalichako aondolewa uwaziri

Ameshushwa cheo na pia amewekwa Arusha kimkakati.
Inawezekana ni kimkakati kweli lakini ajashuhwa cheo wala kupanda ila kaingia serikalini maana katika mfumo wa utawala wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa ni mwakilishi wa Rais katika mkoa na anatekeleza majukumu ya serikali katika ngazi ya mkoa kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Majukumu ya Mkuu wa Mkoa ni pamoja na kuhakikisha utulivu na usalama, kusimamia utekelezaji wa sera za serikali, na kutoa mwelekeo wa juhudi za maendeleo katika mkoa. Ana mamlaka ya kiutawala na kisheria yanayomwezesha kutekeleza majukumu haya.

Tofauti na Mkuu wa Mkoa, Katibu Mwenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa ni kiongozi wa chama ambaye anahusika na kueneza itikadi na sera za chama. Uteuzi wa Makonda kama Mkuu wa Mkoa unamaanisha ameingia moja kwa moja katika uongozi wa serikali, tofauti na wajibu wa Katibu Mwenezi ambaye anahusika zaidi na mambo ya chama.
 
Inawezekana ni kimkakati kweli lakini ajashuhwa cheo wala kupanda ila kaingia serikalini maana katika mfumo wa utawala wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa ni mwakilishi wa Rais katika mkoa na anatekeleza majukumu ya serikali katika ngazi ya mkoa kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Majukumu ya Mkuu wa Mkoa ni pamoja na kuhakikisha utulivu na usalama, kusimamia utekelezaji wa sera za serikali, na kutoa mwelekeo wa juhudi za maendeleo katika mkoa. Ana mamlaka ya kiutawala na kisheria yanayomwezesha kutekeleza majukumu haya.

Tofauti na Mkuu wa Mkoa, Katibu Mwenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa ni kiongozi wa chama ambaye anahusika na kueneza itikadi na sera za chama. Uteuzi wa Makonda kama Mkuu wa Mkoa unamaanisha ameingia moja kwa moja katika uongozi wa serikali, tofauti na wajibu wa Katibu Mwenezi ambaye anahusika zaidi na mambo ya chama.
Kashushwa cheo acha ukujipa moyo.sahivi anaenda kupigwa biti na kamati ya siasa ya mkoa na atakua anapeleka taarifa za utekelezaji wa ilani kila robo mwaka.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanyau teuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:

i) Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe.Ndejembi anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

ii) Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Anachukua nafasi ya Mhe.John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.

iii) Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

iv) Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.

v) Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.

vi) Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhe. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.

vii) Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

viii) Amemhamisha Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb.) kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.

ix) Amemteua Bw. Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

x) Amemteua Bw. Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.

xi) Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

xii) Amemhamisha Bi. Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).

xiii) Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bi. Agnes Kisaka Meena ambaye
amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.

xiv) Amemteua Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

Dkt. Serera anachukua nafasi ya Bw. Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.

xv) Amemteua Bw. Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

xvi) Amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya
Mipango.

Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuuu tafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

View attachment 2949540
View attachment 2949541
Arusha atakuwa amemtenganisha na DSM, pia watu wa Arusha na morani. Ndali ni kutofautiana na viongozi kuhusu
mitaala Mipya
 
Safi sana Makonda nakuomba ukaokoe vijana wa Arusha, nidhamu ya wale vijana imeharibiwa na madawa ya kulevya hasa mirungi na bangi halafu wao wanaona huo ndio ujanja, naamini hili utaliweza hujawahi shindwa jambo.
 
Hizi nafasi ulinganisho wake hutegemea na seniority yako... kwamba unatoka wapi unakwenda wapi!

Huwezi kutoka U RC ukapewa U DC ila unaweza ukawa Naibu waziri ukatupwa kwa U DC!

Hizi nafasi za kisiasa huwa hazina sana formality of seniority unless unaeteuliwa uwe unajitambua... kuna siku Batilda Buriani aliyewahi kuwa waziri alipewa U RAS!!!

Yule Christina mndeme alifikia ngazi kubwa sana CCM kuwa N/katibu mkuu akitokea kwenue U RC then akarudishwa kwa u RC tena kapewa unaibu katibu mkuu wa wizara!!

Afrika hakuna seriousness katika kupanga majukumu na malengo na watekelezaji. Watu wanatafutiwa kichochoro tu chakuendelea kula ugali.
haha hasa tz huwa nacheka mambo yanavyoendeshwa. nchi haiko serious ni mzaha tu. ningezaliwa mzungu ningebagua sana watu weusi
 
Acheni kujitoa ufahamu. Katibu wa Itikadi siasa na uenezi aliyepita kabla ya Bashite aliishia kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya. Ila yeye kawekwa mkuu wa mkoa wa Arusha kimkakati. Je yeye na Chongolo ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama wana tofauti gani? Tena yeye kapewa jiji lenye ngome ya upinzani!?

Hapo ni siasa za CCM za kutafuta kuungwa mkono kaskazini. Kuitoa CCM haitowezekana kwa miaka 30 ijayo. Huo ndio ukweli mchungu. Kwa akili za upinzani kudemka inaonesha hawaijui siasa na watapigwa bao tena.

CCM ni dubwana kubwa sana.
dubwana wapi wanatumia vyombo vya dola. bila hizo apparatus hawana lolote
 
wazee wa tamaa za vyeo na madaraka.
huko sijui ni kuumia au kuteseka 🐒

wewe unatumwa kwenda kutumikia wananchi, jamaa flani lenye uchu na tamaa ya madaraka limekaa mahali, linatathimini hii nafasi aliyopewa fulani ni ya juu au chini, ndogo au kubwa 🐒

utumishi ni utumishi tu,
ukitumwa popote unakwenda kwa moyo wote kufanya kazi ya wananchi. Weledi, bidii, maarifa na uchapakazi wako ndicho kifanye wewe kua ni mkubwa au mdogo 🐒
 
Back
Top Bottom