Mtemi mpambalioto
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 3,436
- 7,955
system
Watu wanabahati sana Dr Mhede amefeli TRA akafeli DART tena kapewa kazi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu wanabahati sana Dr Mhede amefeli TRA akafeli DART tena kapewa kazi?
Amemteua Lucas Mwashambwa kuwa chawa kiongozi jamiiforums.
Anyway tukiacha utani, Bashite kuna namna amegusa pasipogusika, na soon anaweza akarudi bench aendelee kuwa best loser!!
Watu awaelewi tu, ila ndo kashaingia serikalini ivyo.Kashushwa cheo au analetwa serikalini mdogo mdogo.?
Inawezekana ni kimkakati kweli lakini ajashuhwa cheo wala kupanda ila kaingia serikalini maana katika mfumo wa utawala wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa ni mwakilishi wa Rais katika mkoa na anatekeleza majukumu ya serikali katika ngazi ya mkoa kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.Ameshushwa cheo na pia amewekwa Arusha kimkakati.
Ndio kazi pekee amayoimudu ukiachilia mbali ile ya kuzurula kimataifaHuyu Rais huwa anatengua na kuteua usiku tu?!!!
Kashushwa cheo acha ukujipa moyo.sahivi anaenda kupigwa biti na kamati ya siasa ya mkoa na atakua anapeleka taarifa za utekelezaji wa ilani kila robo mwaka.Inawezekana ni kimkakati kweli lakini ajashuhwa cheo wala kupanda ila kaingia serikalini maana katika mfumo wa utawala wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa ni mwakilishi wa Rais katika mkoa na anatekeleza majukumu ya serikali katika ngazi ya mkoa kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Majukumu ya Mkuu wa Mkoa ni pamoja na kuhakikisha utulivu na usalama, kusimamia utekelezaji wa sera za serikali, na kutoa mwelekeo wa juhudi za maendeleo katika mkoa. Ana mamlaka ya kiutawala na kisheria yanayomwezesha kutekeleza majukumu haya.
Tofauti na Mkuu wa Mkoa, Katibu Mwenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa ni kiongozi wa chama ambaye anahusika na kueneza itikadi na sera za chama. Uteuzi wa Makonda kama Mkuu wa Mkoa unamaanisha ameingia moja kwa moja katika uongozi wa serikali, tofauti na wajibu wa Katibu Mwenezi ambaye anahusika zaidi na mambo ya chama.
Nami nimeshtuka kweli aiseeMakonda kashushwa Cheo
Kama kuna kasoro uteuzi ni huyu bwana. Everything he touches becomes not gold.Watu wanabahati sana Dr Mhede amefeli TRA akafeli DART tena kapewa kazi?
Amebadilishiwa kutoka majukumu ya chama na sasa anamajukumu ya kiserikaliKashushwa cheo acha ukujipa moyo.sahivi anaenda kupigwa biti na kamati ya siasa ya mkoa na atakua anapeleka taarifa za utekelezaji wa ilani kila robo mwaka.
Arusha atakuwa amemtenganisha na DSM, pia watu wa Arusha na morani. Ndali ni kutofautiana na viongozi kuhusuTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanyau teuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:
i) Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe.Ndejembi anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
ii) Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Anachukua nafasi ya Mhe.John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.
iii) Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
iv) Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.
v) Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.
vi) Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mhe. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.
vii) Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
viii) Amemhamisha Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb.) kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.
ix) Amemteua Bw. Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
x) Amemteua Bw. Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.
xi) Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
xii) Amemhamisha Bi. Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
xiii) Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bi. Agnes Kisaka Meena ambaye
amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.
xiv) Amemteua Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Dkt. Serera anachukua nafasi ya Bw. Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.
xv) Amemteua Bw. Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
xvi) Amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya
Mipango.
Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuuu tafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
View attachment 2949540
View attachment 2949541
Anaondolewa ki aina kwenye mfumoKashushwa cheo au analetwa serikalini mdogo mdogo.?
haha hasa tz huwa nacheka mambo yanavyoendeshwa. nchi haiko serious ni mzaha tu. ningezaliwa mzungu ningebagua sana watu weusiHizi nafasi ulinganisho wake hutegemea na seniority yako... kwamba unatoka wapi unakwenda wapi!
Huwezi kutoka U RC ukapewa U DC ila unaweza ukawa Naibu waziri ukatupwa kwa U DC!
Hizi nafasi za kisiasa huwa hazina sana formality of seniority unless unaeteuliwa uwe unajitambua... kuna siku Batilda Buriani aliyewahi kuwa waziri alipewa U RAS!!!
Yule Christina mndeme alifikia ngazi kubwa sana CCM kuwa N/katibu mkuu akitokea kwenue U RC then akarudishwa kwa u RC tena kapewa unaibu katibu mkuu wa wizara!!
Afrika hakuna seriousness katika kupanga majukumu na malengo na watekelezaji. Watu wanatafutiwa kichochoro tu chakuendelea kula ugali.
dubwana wapi wanatumia vyombo vya dola. bila hizo apparatus hawana loloteAcheni kujitoa ufahamu. Katibu wa Itikadi siasa na uenezi aliyepita kabla ya Bashite aliishia kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya. Ila yeye kawekwa mkuu wa mkoa wa Arusha kimkakati. Je yeye na Chongolo ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama wana tofauti gani? Tena yeye kapewa jiji lenye ngome ya upinzani!?
Hapo ni siasa za CCM za kutafuta kuungwa mkono kaskazini. Kuitoa CCM haitowezekana kwa miaka 30 ijayo. Huo ndio ukweli mchungu. Kwa akili za upinzani kudemka inaonesha hawaijui siasa na watapigwa bao tena.
CCM ni dubwana kubwa sana.
Mm nilijua kaletwa nchimbi basi atafagia mitaka taka yooote.katibu hana kelele ni mtu wa mipango zaidi.niliota ndoto flan naikumbuka mpaka kesho.inakribia kutimiaNchimbi kafagia benchi zima la Lumumba sasa ni zamu ya kujipanga kimkakati kwa mbinu mpya na si porojo .
Makubwa gani wewe embu tuache tule pasakaKuna makubwa Makonda atafanya nchi hii. Msimchukulie poa
wazee wa tamaa za vyeo na madaraka.mno !