Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

uteuzi wa kimkakati sana huu [emoji16][emoji16]
 

Maprofesa wa chuo kikuu cha Dar es salaam ninaomba mnieleweshe hili jambo:-​

Kuna watu waliteuliwa na JK akiwa Rais, alipoingia JPM watu hao walifukuzwa wote, sasa ameangia Samia anawarudisha wote waliofukuzwa na JPM ila walikuwa wameteuliwa na JK kabla.​

Swali la msingi ni nani anamshauri Samia kuteua tena waliokuwa wameteuliwa na JK ila walifukuzwa na JPM?​

 
Sawa Nahodha hapo atapewa Wizara, hongera kwa Mchechu kurudishwa NHC kwani alilihudumia vyema shirika, Polepole Malawi akatatue mgogoro wa ziwa Nyasa [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Huwezi jua ya Mungu mengi na hujafa hujaumbika...
Huo Ni mtego ili aone Kama atakubali kuchutama, akizingua hakai hata mwaka.

Anakua kama mwenzie nchimbi kule brazil[emoji4]
 
Duuu
Wameamua kumficha mfichua wahuni ili asiendelee kuwafichua wahuni
 
Pole wameshindwa kumthibiti nchini wameamua kumtoa nje ya nchi
 
kabisa mkuu. ubalozi wanafaidi watoto tu ila balozi mwenyewe kama ni siasa anakua amepotezwa kwenye ramani kabisa
 
Acha Kukariri

Performance za Nehemia pale NHC ni sawa na ya Dau pale NSSF au ya Dr Kimei pale CRDB …hazijawahi kufikiwa kabla na baada yao wamepigiwa kelele weeeeee za kila aina lakin baada ya kuondoka hakuna lolote la maana

Awamu ya nne Ndege ya Mzee kila ikiruka kwenda ng'ambo kwny mambo ya Uchumi, fedha na uwekezaji basi mmoja kati ya hao mapacha watatu lazima awepo
Huyu mchechu amewekwa pale ili akapige vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…