Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ila kwa ndugai anachoMama hana kinyongo na mtu, vipi kuhusu ubunge wake atautumikiaje akiwa ughaibuni au ndiyo umegawiwa kwa Vuai?
Mafuru tayari yupo wizara ya fedha, ni msajiliSababu sio muhimu sana ndugu, ni suala la mkeka kutimia, anafuata Mafuru, genge linatimia! Vuai kuwa mbunge? Alikuwa waziri kiongozi huyu, kuna neno hapa......uzanzibar unaenda kushika hatamu
Huo Ni mtego ili aone Kama atakubali kuchutama, akizingua hakai hata mwaka.Huwezi jua ya Mungu mengi na hujafa hujaumbika...
DuuuRais Samia Suluhu amemteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.
Sambamba na hilo Rais Samia Suluhu amemteua Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia Rais Samia Suluhu amemteua Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL na anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Rubirya ambaye amestaafu kwa umri.
Polepole na Kindamba wanatarajiwa kuapishwa kesho Jumanne tarehe 15 Machi 2022 Ikulu ya Chamwino Dodoma saa 04:00 Asubuhi.
Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu amemteua Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Mchechu ambaye amewahi kuhudumu kwenye wadhifa huo, anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Pia amemteua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (Mstaafu) Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari (Tanzania Port Authority).
Na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Peter Ulanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Ulanga ni Mkurugenzi Mstaafu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).
Na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali John Julius Mbungo, Mkurugenzi Mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Meli Tanzania (MSCL).
View attachment 2150380
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nafikiri sasa ataelewa msemo wa "wahuni sio Watu"
Duh, Hakika tumepotea Njia.Dodoma sasa tunapelekwa Pemba
Mipango mkakati ndugu...Nehemia Mchechu NHC tena? Ni sababu zipi zilipelekea kutumbuliwa? Hazikuwa genuine?Hivi hakuna watanzania wengine?
Muungano? Muungano?Duh, Hakika tumepotea Njia.
Hata kama tutagoma kwenda,,,,,,,Bado tutapelekwa tu.
Safari yenyewe haihitajiki Nauli kufika tunapopelekwa.
...........TUMEIPENDA WENYEWE.......
kabisa mkuu. ubalozi wanafaidi watoto tu ila balozi mwenyewe kama ni siasa anakua amepotezwa kwenye ramani kabisaTeuzi Kama hizi huwa Ni maalum ili kukuondolea umaarufu na kukufilisi kijanja.
Ukishakua nje ya nchi attention yako inakua Ni ndogo mno, pia Kama una vimiradi vyako ulianzisha lazima viyumbe.
Ukija kurudi bongo, unakua Kama ndo unaanza upya.
Mfano mzur muone Dr. Slaa na mabalozi wengine walio wastaafu walio nje ya mfumo, yaan utadhan ndo wanaanza maisha[emoji4]
Haizidi milioni tano, na unaipata kwa kuchelewa tarehe 40, na huko anakuwa exile, asirudishwe tenaUbalozi mshahara shillingi ngapi?
Huyu mchechu amewekwa pale ili akapige vizuri