hoja nzuri!
ila nadhani sio kuwa tumepunjwa akili. kwa bahati mbaya mifumo yetu ya zama za kale, sio utawala sio uchumi, yote imeuliwa na mkoloni.
cheki
hii video, inaweka shida zote tulizonazo kama waafrika sehemu moja! kwa bahati mbaya, hatuna ujanja kukwepa pia, hio ndio shida kubwa!
kiukweli sisi Waafrika tupo vizuri na wabunifu sana sema kwa muda mrefu utawala wa kikoloni umeturudisha nyuma mno! na katika mifumo mipya, baadhi ya waafrika wenzetu wanaendeleza mifumo ya kikoloni na bahati mbaya zaidi, pesa ilipoingizwa kwenye mfumo wa malipo duniani ndio kabisa waafrika wamepotea kwenye chati. ila siri kubwa ya mafanikio ya mwaafrika ni kwenye kilimo. sisi ndio wenye ardhi ambayo tunawezalisha dunia lakini vipingamizi ni vingi hasa lugha na sayansi inayotumika katika uboreshaji ni chenga sana.
kuna mambo mengi Waafrika wamegundua alafu sifa zinaenda kwa mtu mweupe! bahati mbaya kwenye michezo hamna jinsi ya kumpokonya Mwafrika sifa na juhudi zake kwani zinaonekana na ndio maana sehemu kubwa hapo kwenye michezo tuna shine sana!
swala la maendeleo, uongozi yote hayo ni mifumo iliyowekwa na mkoloni. mkoloni akiona kuna mweusi anakipaji kuliko wenzake basi sifa nyingi na kumpelekea dada/kaka yetu kuleta dharau. iwe kwenye elimu ama kipato...
kiufupi, mkoloni ilibidi akae chini afikiria njia nyingine ya kututawala ambapo kaneno "uhuru" katatumika. ni wachache waliogundua na ndio kama tunavyojua, hao hua hatukai nao muda mrefu (naongelea janga linalokumba bara la Afrika hapa)!
tumepotea SANA ila ipo siku atatokea
MTU ambaye atajaribu kufanya mageuzi "
at a great cost" kama wenzake ila atasikika ulimwengu mzima!