Hujafanya tafiti za kutosha ndugu yangu, na pia unanisikitisha sana ambavyo unajiona duni mbele ya jamii nyingine. Huwa nikiwasoma watu wengi kama ninyi, huwa ndiyo napata kufahamu kwamba mzungu alifanikiwa kwa asilimia 100% kumtawala mtu mweusi, kwasababu ameshikilia fikra zetu. Kiufupi mimi nakukubali sana Nankumene japo katika hili naomba niendelee kukukusoa na kama kuna kitu nakosea naomba niambie nifahamu. Niko tayari kujifunza vitu vipya:
Mosi, bila ubishi wowote ule Misri ya kale (Kemet) ilikuwa ni dola la watu weusi. Ushahidi wa kutosha wa hili ninalosema uko kwenye The Egyptian Hieroglyphs. Nafurahi sana kuona umemzungumzia mwana-mahesabu wa Kigiriki Pythagoras. Hivi unafahamu kwamba Pythagoras kama Plato aliwahi kusoma elimu yake ya juu kule Misri ya kale ??? Kiufupi mpaka kufika vita ya Kalkemish (The Battle of Carchemish), vita baina ya Misri na Babeli, Misri ilikuwa inatawaliwa na mafarao waliotoka Sudan (Nubia). Farao Necho II alikuwa ni mnubi wa Sudan. Hili nalo utataka kulipinga ndugu yangu ???
Pili, narudia tena kuhusu Berbers (The Amazigh People). Hii jamii ya kiafrika ndiyo walikuwa wanajeshi wa muhimu wa kalifeti ya Ummay (The Umayyad Caliphate), ambapo walisaidia kwenye uvamizi wa Uhispania. Hata neno GILBRALTAR limetokana na neno la kiarabu Jabal Tarid (The Mountain of Tariq), ambapo walimuenzi kamanda wa kiislamu aliyeongoza uvamizi huo aliyeitwa Tariq Ibn Ziyad. Hawa waafrika (Berbers) ndiyo waliotengeneza falme imara kama Numidia ambazo zilishirikiana na ufalme wa Karthago (Carthage) katika kupambana na Rumi kwa miaka zaidi ya 100 (The Punic Wars).
Baada ya Warumi kumshinda Hannibal mwaka 146 BCE (The Third Punic War), Scipio Africanus aliamuru dola la Karthago lichomwe moto lote na watu wake kuuzwa utumwani. Walifanya sawa na kile ambacho Mongols chini ya Monghke Khan walikifanya kule Baghdad mwaka 1258 (The Siege of Baghdad) ambako kulikuwa na maktaba kubwa na vyuo bora kabisa duniani kwa wakati huo. Leo hii historia ya haya madola hazipo. Lakini, hata kama hazipo, basi tuseme kwamba waafrika wana akili ndogo kuliko jamii nyingine ???
Tatu na mwisho kabisa, waafrika wana historia ambayo haijazungumzwa na kufanyiwa tafiti vilivyo. Wenzetu wazungu wamefanikiwa sana katika kuaminisha weusi kwamba hawana historia. Wengi wetu hili tumelibeba kama lilivyo bila kulipa tafakuri za kina. Naomba nikupe mifano ya mwisho: Kipindi Roma iko chini ya Kaisari Augustus, vilitokea vita vikubwa baina ya Ethiopia (Nubia) na dola la Mrumi mwaka 24 BCE ambapo waliishia kufanya makubaliano ya amani. Hivi mtu mjinga asiye na akili anaweza kuingia kwenye makubaliano ya kidiplomasia na taifa kama Roma kweli ???
Haya, wazungu wamefika zimbabwe (The Great Zimbabwe), wakaandika kwamba ule mji ulijengwa na wazungu kwasababu weusi wasingeweza kufanya hivyo. Kuna watu wanaamini mpaka leo hii kwamba The Great Zimbabwe haukujengwa na watu weusi. Mara ya kwanza Vasco Da Gama anaona rangi iliyopakwa ukutani (Colour Paint) ilikuwa ni kule Kilwa (The Kingdom of Kilwa), hapa nchini kwetu. Ifahamike kwamba Kilwa ilitengeneza hadi sarafu yake ambayo ipo kwenye makumbusho yake, lakini pia ilianzisha mahusiano ya kidiplomasia na Uchina (The Ming Dynasty) mnamo karne ya 14. Hivi watu wasio na akili wanaweza kutengeneza sarafu yao kweli, pamoja na kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia ???
Aidha kuna kitu kimefichika, au waafrika mnajiona ni mapanzi kama ambavyo wapelelezi wa kihebrani walimwambia Nabii Mussa baada ya kutoka kule Kaanani.....Yote, tisa mzungu kafanikiwa sana kushika akili za mwafrika. Katika hili, alifanikiwa mno....