Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

my dear, this kind of articles are for people with very high intellect, came back again, hope you will understand just a bit if not all
I am among the intellectuals just let you know! I have been here long enough! I can read and understand what is blue green or red!

I am not stupid!
 
The irony is JPM happens to be a devout Catholic himself. Otherwise, it's a brilliantly written scholarly article.
 
Pascal Mayalla,

Paschal,

Umeandika vizuri. Vikwazo vya uhuru wa Tume haviko kwenye sheria ya uchaguzi pekee. Katiba ya nchi nayo inavyo vikwazo vya uhuru wa Tume. Kwa mfano, inamruhusu Raia kuwa Mwenyekiti wa chama tawala. Matatizo mengi yanaanzia hapo. Tunaweza kujadiliana sana. Lakini, hebu soma kwa makini maelezo haya kuhusu tofauti kati ya uhuru na utumwa wa Tume, halafu tuone kama tutaongea lugha moja...

Tofauti kati ya uhuru na utumwa

Tamko kwamba, “Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania inapaswa kuongezewa uhuru ili iweze kutekeleza kazi zake kwa kasi na ufanisi stahiki,” haliwezi kutetewa au kupingwa kwa ufanisi kama hatujakubaliana kuhusu maana ya “uhuru” inaotakiwa kuongezwa.

Napendekeza kwamba, fasili nzuri ya neno “uhuru” ambalo ni kinyume cha neno “utumwa,” ni ile iliyotolewa mwaka 1967 na Profesa Gerald C. MacCallum (1925-1987) wa Marekani.

Kupitia makala yenye kichwa cha maneno, " Negative and Positive Freedom," iliyochapishwa katika Jarida la “The Philosophical Review,” toleo namba 76.3, ukurasa wa 312 hadi 334, mwaka 1967, MacCallum aliwakosoa kwa ufanisi wanafilosofia wanaopenda kuugawanya uhuru katika makundi mawili ya “uhuru hasi” na “uhuru chanya.”

Badala yake, MacCallum (1967) alipendekeza kwamba, “…freedom is thus always of something (an agent), from something (constraint), to do, not do, become, or not become something (goal); it is a triadic relation.” (uk. 314)

Ndio kusema kuwa, “uhuru ni mahusiano kati ya vitu vitatu kwa mpigo, kwani mara zote tunapoongelea uhuru tunamaanisha uhuru wa MTENDAJI, dhidi ya VIKWAZO vinavyoweza kumkabili mtendaji huyo, katika azma yake ya ama kufanya/kutofanya kitendo fulani, au kuwa/kutokuwa katika hali fulani, hili la mwisho likiwa ni LENGO lake.” (Tafsiri yangu).

Katika fasili hii, MacCallum (1967) anasema mambo mawili kwa mpigo, moja likihusu maana ya “uhuru” na jingine likihusu maana ya “utumwa.”

Kuhusu “uhuru,” MacCallum (1967) anasema kuwa, madai yoyote kuhusu kuwepo kwa “uhuru” katika mazingira fulani, ni madai yanayoambatana na uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama MTENDAJI, uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama KIKWAZO dhidi ya uamuzi wa mtendaji, na uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama LENGO la mtendaji, ambapo, kwa sababu ya kutobanwa na vikwazo, mtendaji yuko huru kuyafukuzia malengo yake kwa ufanisi.

Na kuhusu “utumwa” MacCallum (1967) anasema kuwa, madai yoyote kuhusu kuwepo kwa “utumwa” katika mazingira fulani, ni madai yanayoambatana na uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama MTENDAJI, uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama KIKWAZO dhidi ya uamuzi wa mtendaji, na uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama LENGO la mtendaji, ambapo, kwa sababu ya kubanwa na vikwazo, mtendaji anashindwa kuyafukuzia malengo yake kwa ufanisi.

Kama hii ndio tofauti kati ya “uhuru” na “utumwa” swali linafuata: Je, katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania kuna uhuru kiasi gani na kuna utumwa kiasi gani?
 
Niliposoma na nikakuta limetumika neno maaskofu walidai badala ya maaaskofu wamesema/ walisema nikajikuta napoteza interest ya kuendelea kusoma

Ni suala la lugha tu.

Kudai/kusema, kutoa madai, kusema rai, nk ni maneno yenye maana ile ile.

Katika usanifu wa hoja kwa kuzingatia fomati ya Stephen Toulmin tunayo hoja yenye vipengele hivi:

  • claim/hypothesis/proposal (Madai, rai, pendekezo)
  • ground (ushahidi wa daraja la kwanza)
  • warrant (ushahidi wa daraja la pili)
  • backing (ushahidi wa daraja la tatu)
  • objection (pingamizi/mkingamo)
  • rebuttal (kibutuzi)
Hapo vipi?
 
Makala nzuri ila wavivu wa kusoma hawatajikita kwa kilicho andikwa.Ndio maana sishangai kuona wengi wakimjibu P na kuacha kujadili yaliyomo kwenye makala.

MALG, naelewa hiyo changamoto. Lakini, hoja iliyokamilika haiwezi kujengwa kwa mtindo wa meseji za twitter. Tunahitaji nafasi ya kuweka bayana haya: claim, ground, warrant, backing, objections, rebuttals. Bila hivyo, hoja ya Tume huru, kama nilivyoijadili, haiwezi kuandikika. Naamini walengwa wakuu wanao uwezo wa kusoma makala yote. Ni maneno 3,000 pekee.
 
Nimesoma paragraph moja nikaona mnanichanganya
Mambo mengi....
Nitarudi

Pole Pakawa. Lakini, hoja ninayoijenga hapa haiwezi kujengwa kwa kutumia characters 140 za twitter.
Nafasi inahitajika kwa ajili ya mambo haya: claim, ground, warrant, backing, objection, rebuttals and qualifiers. Kwa hiyo, tuvumiliane.
 
sijaona wapi PM amekosea kwenye point yake ..kweli watanzania ni waoga kila mtu anakimbiza ubawa wake...na kwa kielelezo hicho CCM inaweza kutawala milele...kumbuka CCM ni taasisi na taasisi huwa hazifi ila wale viongozi hufa ..na hata viongozi wakifa wanachaguliwa wengine..that why today we dont have Mwalimu,kawawa..sokoine..bibi titi..Karume but CCM bado ipo imara na inaendelea kushikilia dola.......

jaribu kufikiria in that perspective you will see his point....

Paschal Mayala anakosea kusema kuwa Tume ya Uchaguzi ni Huru lakini sheria ya uchaguzi ndio mbaya. Anashindwa kuelewa maana ya uhuru unaoongelewa. Katiba ya nchi na sheria mbaya ni baadhi ya vikwazo vinavyopunguza uhuru wa Tume.
 
Hongera kwa uchambuzi.. Naomba kujua machache, mosi, hivi kweli KANU iliondolewa madarakani kwa waraka? Pili, naomba kujua kimantiki sababu zilizopelekea Uhuru Kenyatta akiwa KANU aonekane hafai ila akaonekana anafaa akiwa Jubilee! Tatu, je kubadilisha jina la chama kuna manufaa hata kama watu watabaki wale wale?

Majibu:

- KANU iliondolewa na waumini waliovuviwa na waraka.

- Sababu zilizopelekea Uhuru Kenyatta akiwa KANU aonekane hafai ila akaonekana anafaa akiwa Jubilee ni hizi: itikadi, sera, matendo ya chama cha KANU yalikuwa tofauti na tikadi, sera, matendo ya 'chama' cha JUBILEE.

- Umeuliza: je kubadilisha jina la chama kuna manufaa hata kama watu watabaki wale wale? Nami nikuulize: je kubadilisha jina la kampuni kuna manufaa hata kama watendaji wake watabaki wale wale? Jawabu ni ndio. Pitia matini yako ya somo la "rebranding."
 
Mama Amon bandiko lako limelenga uhuru wa kitaasisi ambao kimsing ni zao la sheria zinazounda taasisi husika.

Swali langu ni dogo tu.
Je uhuru wa kifikra kwa watendaji wa taasisi husika upo ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama Amon bandiko lako limelenga uhuru wa kitaasisi ambao kimsing ni zao la sheria zinazounda taasisi husika. Swali langu ni dogo tu: Je uhuru wa kifikra kwa watendaji wa taasisi husika upo ?

Sijaelewa kwa nini unatofautisha uhuru wa kitaasisi na uhuru wa mtu mmoja mmoja ndani ya taasisi. Kwa maoni yangu taasisi ni watu. Uhuru wao una vikwazo vya ndani, kwa upande mmoja, na vikwazo vilivyo nje ya miili yao, kwa upande mwingine. Sheria mbaya ni vikwazo vya nje ya miili yao. Ujinga wao, hofu zao, mashaka yao, imani zao za kisiasa, etc ni vikwazvo vya ndani ya miili yao. Aina zote mbili za vikwazo zinaikwaza Tume kama taasisi.

Kwa ufafanuzi zaidi, soma maelezo haya.....

Tofauti kati ya uhuru na utumwa

Tamko kwamba, “Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania inapaswa kuongezewa uhuru ili iweze kutekeleza kazi zake kwa kasi na ufanisi stahiki,” haliwezi kutetewa au kupingwa kwa ufanisi kama hatujakubaliana kuhusu maana ya “uhuru” inaotakiwa kuongezwa.

Napendekeza kwamba, fasili nzuri ya neno “uhuru” ambalo ni kinyume cha neno “utumwa,” ni ile iliyotolewa mwaka 1967 na Profesa Gerald C. MacCallum (1925-1987) wa Marekani.

Kupitia makala yenye kichwa cha maneno, " Negative and Positive Freedom," iliyochapishwa katika Jarida la “The Philosophical Review,” toleo namba 76.3, ukurasa wa 312 hadi 334, mwaka 1967, MacCallum aliwakosoa kwa ufanisi wanafilosofia wanaopenda kuugawanya uhuru katika makundi mawili ya “uhuru hasi” na “uhuru chanya.”

Badala yake, MacCallum (1967) alipendekeza kwamba, “…freedom is thus always of something (an agent), from something (constraint), to do, not do, become, or not become something (goal); it is a triadic relation.” (uk. 314)

Ndio kusema kuwa, “uhuru ni mahusiano kati ya vitu vitatu kwa mpigo, kwani mara zote tunapoongelea uhuru tunamaanisha uhuru wa MTENDAJI, dhidi ya VIKWAZO vinavyoweza kumkabili mtendaji huyo, katika azma yake ya ama kufanya/kutofanya kitendo fulani, au kuwa/kutokuwa katika hali fulani, hili la mwisho likiwa ni LENGO lake.” (Tafsiri yangu).

Katika fasili hii, MacCallum (1967) anasema mambo mawili kwa mpigo, moja likihusu maana ya “uhuru” na jingine likihusu maana ya “utumwa.”

Kuhusu “uhuru,” MacCallum (1967) anasema kuwa, madai yoyote kuhusu kuwepo kwa “uhuru” katika mazingira fulani, ni madai yanayoambatana na uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama MTENDAJI, uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama KIKWAZO dhidi ya uamuzi wa mtendaji, na uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama LENGO la mtendaji, ambapo, kwa sababu ya kutobanwa na vikwazo, mtendaji yuko huru kuyafukuzia malengo yake kwa ufanisi.

Na kuhusu “utumwa” MacCallum (1967) anasema kuwa, madai yoyote kuhusu kuwepo kwa “utumwa” katika mazingira fulani, ni madai yanayoambatana na uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama MTENDAJI, uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama KIKWAZO dhidi ya uamuzi wa mtendaji, na uwepo wa kitu kinachotambuliwa kama LENGO la mtendaji, ambapo, kwa sababu ya kubanwa na vikwazo, mtendaji anashindwa kuyafukuzia malengo yake kwa ufanisi.

MacCallum (1967) anafananua kuwa, vikwazo vya uhuru vinaweza kuwa nje au ndani ya mwili wa mtendaji.

Kikwazo cha uhuru kilicho nje ya mwili wa mtendaji, ni kitu kama vile mtu mwingine, kikwazo asilia kama vile mafuriko yaliyoziba barabara, minyororo uliofungwa mguuni mwa mtu, pingu zilizofungwa mikononi mwa mtu, ukosefu wa ajira, mdororo wa uchumi unaosababisha mzunguko hafifu wa fedha, na kadhalika.

Hivyo, kwa kuzingatia vikwazo vya nje, mtu atakuwa sio huru endapo mfumo au watu wengine wanamzuia kufanya anachotaka kukifanya, wanamkataza kwenda anakotaka kwa kumfungia chumbani, anataka kwenda mahali lakini anaogopa kufika huko kwa kuwa kuna mbwa mkali, au anataka kwenda mahali lakini hana nauli ya kumwezesha kusafiri hadi huko.

Na vikwazo vya uhuru vilivyo ndani ya mwili wa mtendaji, vinaweza kuwa ni vikwazo vya kisaikolojia kama vile ni ujinga, woga (phobia); hisia kama vile hasira, chuki, wivu, upendo; upumbavu, yaani urazini hafifu; ugonjwa wa kijenetiki, kama vile ugonjwa wa kutoweza kuona rangi za aina fulani; vikwazo vya kiafya kama vile upofu, ukiziwi, na homa ya malaria inayokufanya ushindwe kwenda kazini.

Kusudi tuelewane, hebu tutumie mifano ya wavuta sigara wawili wanaoendesha magari kwenda kununua sigara kutoka madukani, kila mmoja akiwa anaendesha gari lake.

Katika mfano wa kwanza, tuseme kwamba dereva mmoja yuko huru, tukiwa tunamaanisha kuwa, dereva yuko huru dhidi ya vikwazo vilivyo nje ya mwili wake, kama vile trafiki au alama za barabarani zinazoweka ukomo wa kasi ya gari, kufanya anachotaka au kwenda anakotaka kufika.

Katika mfano wa pili, tuseme kwamba dereva mwingine hayuko huru, tukiwa tunamaanisha kuwa, dereva hayuko huru dhidi ya vikwazo vilivyo ndani ya mwili wake, yaani ujinga unaomzuia kujua kwa ufasaha ni duka gani linauza aina ya sigara anayoitaka.

Kwa upande mmoja, mifano hii miwili inafanana katika jambo moja kubwa. Yaani, katika kila mfano kuna kipengele cha uhuru chanya na kipengele cha uhuru hasi. Uhuru chanya ni uhuru wa mtendaji dhidi ya vikwazo na uhuru hasi ni uhuru wa mtendaji kuwa anavyotaka au kufanya anachotaka.

Na kwa upande mwingine, mifano hii miwili inatofautiana katika jambo moja kubwa. Jambo hilo linahusu mahali viliko vikwazo vilivyombana mtendaji.

Katika mfano wa kwanza, kuna vikwazo vya uhuru vilivyo nje ya mwili wa mtendaji, wakati katika mfano wa pili kuna vikwazo vilivyo ndani ya mwili wa mtendaji.

Nje ya mwili wa dereva kuna binadamu ambaye ni trafiki, vitu kama vile alama za usalama zinazotamka ukomo wa kasi ya gari au makorongo. Kwa ujumla, vikwazo vya uhuru vilivyo nje ya mwili wa mtendaji vinaweza kuwa ni maamuzi na matendo ya watu baki kama vile trafiki, vitu vilivyotengenezwa na binadamu kama vile alama za barabarani, na vitu asilia kama vile makorongo na mafuriko.

Na kwa upande mwingine, ndani ya mwili wa dereva, kuna kikwazo cha ujinga wake, ambalo ni tatizo la kisaikolojia.

Kama hii ndio tofauti kati ya “uhuru” na “utumwa” swali linafuata: Je, katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania kuna uuru kiasi gani na kuna utumwa kiasi gani?
 
Mkuu Kitaturu, hili la CCM kutawala milele, sii langu, wala sio mimi nimejiinua na kusema CCM itatawala milele ambayo ni kama kumkufuru Mwenyezi Mungu.
Naomba jipe muda ukanisome hapa uone ni nani aliyeyasema hayo, mimi kosa langu labda liwe ni kuwaripotia tuu humu kuwa CCM itatawala milele.

Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.

Paschal, tatizo ninaloliona katika maandiko yako ni utata wa kimaana unaoambatana na misamiati yako. Mfano mzuri ni maneno "umilele" na "ukweli." Mahali fulani umeandika hivi:

"Jee Milele ni Muda Gani?. Kuna aina mbili za milele, milele ya kwanza ni milele ya kiroho, eternal ambayo inaongozwa na Mungu, na hata sisi binadamu, tutaishi milele, hivyo hapa duniani tuko tuu safarini kuelekea kwenye ama uzima wa milele mbinguni au peponi kwa Mungu kwa watenda wema, au kwenye jehanum ya ziwa la moto wa milele kwa shetani kwa watenda maovu."

"Milele ya pili ni life span ya kudumu mpaka mwisho. Hii ni milele ya kidunia, ukizaliwa ukaishi, siku utakapokufa hiyo ndio milele yako na hapo ndipo mwisho wako. Life span zinatofautiana, mtoto akizaliwa na kuishi siku moja, hiyo siku moja, ndio milele yake, na mtu mwingine ukiishi miaka 100, hiyo ndio milele yake, kama ilivyo nyumba, ukizaliwa na kuvikuta vitu fulani, ukaishi navyo mpaka ulipokufa na kuviacha, vitu hivi vitasemwa vimeishi milele. Hivyo kwa wale wote walioishuhudia CCM ikizaliwa, kisha wao ndio wamekufa na kuiacha CCM, kwao CCM imedumu milele. Hivyo hata hawa waliopo sasa, ambao wamezaliwa na kuikuta CCM, na watakufa na kuiacha CCM, kwao CCM ni chama cha milele."


Neno "umilele" halina maana hizo mbili kama ambavyo unasema. Ukitaka kunyoosha hoja zako google kidogo maneno haya "philosophy of time." Ukishakusoma na kuelewa rudi uhariri threads zako... Vinginevyo naona unachanganya maembe na viazi na kutuaminisha kuwa yote ni matunda.
 
Gutierrez (1988) anasema kuwa "To know God is to do Justice".
(Tazama kitabu chake nimeambatanisha)
Yaani, Kumpenda Mungu ni kutenda haki.
Kama JPM anatenda haki, basi anampenda Mungu.
Na kinyume chake ni kweli.
Je, wewe unafikiri nini?
Huo ni mtazamo mmoja, unaweza kuwa sahihi, lakini haumzuii muumini kuwa Mcha Mungu. Nikirudia ile cliché, hakuna binadamu aliyekamilika.
 
Erythrocyte,
Waafrika kwa misiba!
Yani hapo ndio tunapokwamia, suhulu ya matatizo ya kisiasa utegemee kususuia misiba ni uzembe wa hali ya juu.

Tunakoenda misiba haitakuwa na uzito kihivyo, tukisusa watu wanalipia gharama kampuni ya mazishi kisha marehemu anazikwa na kampuni huku wakihudhuria ndugu na rafiki wa karibu bila kuwasahau kada wenzie wa chama.

Matatizo ya kisiasa hujibiwa kwa mbinu na fitina za kisiasa. Komaeni na serikali ilete usawa(tume huru, sheria bora ya uchaguzi) kwenye mambo ya kisiasa na mengineyo.

Hilo la kuzikana hatujaona maiti ya mtu inazagaa na kuliwa na kunguru au na mbwa mitaani kisa watu walisusa kumzika marehemu kwa sababu yeyote ile.
 
Back
Top Bottom