UVCCM yaomba radhi vijana, yaahidi kumpa ushirikiano Rais Samia Suluhu Hassan

Kuna mmoja alisema Lisu afe.

Mwingine akasema Zitto auawe

Bulembo naye tena ni alhaj skasema Zitto Kabwe afanywe nini sijui!!!

All in all kuomba msamaha ni jambo jema na Ijumaa Kuu wakafanye kitubio hao wakristo wawili!
 
Huyu hakushinda nafasi hio ya uenyekiti alishinda kwa maagizo ya mjomba.Msamaha pekee ni ajiuzuru nafasi hio.Walijimilikisha chama toka cha wakulima na wafanyakazi ni kuwa mali binafsi ya familia.Mjomba mwenyekiti,mpwa mwenyekiti,maamuzi ni yao kununua wapinzani, kurejea chaguzi,kuvuruga chaguzi,nk.Ni Kati ya watu walioibip the hague.
Uzuri technology utunza historia
 
Tangu Madam ale kiapo taifa lina 'family feeling' ndio maana wale 'machokoraa' wanatafuta namna ya kujirudi.

Tunamuombea huyu Mama atawaliwe na hofu ya Mungu aweze kurejesha mshikamano wa kitaifa, kwa maana tulipofikia ni wazi watu wana majeraha makubwa yaliyo tokana na utawala wa awamu ya 5.
 
Waliomuuwa mawazo wameshahukumiwa.
Tunataka wasiojulikana wote wakajibu mitihani yao.
 
Unapoamua kuomba radhi ni marufuku kwenye matamshi yako kutuwekea neno "KAMA/IWAPO NIMEKUKOSEA".. Mpaka unaamua kuomba radhi ni tayari umeshajifanyia tathimini na kujua kuwa ulikosea na kuteleza.
 
Waliomuuwa mawazo wameshahukumiwa.
Tunataka wasiojulikana wote wakajibu mitihani yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…