UVCCM yaomba radhi vijana, yaahidi kumpa ushirikiano Rais Samia Suluhu Hassan

Unapoamua kuomba radhi ni marufuku kwenye matamshi yako kutuwekea neno "KAMA/IWAPO NIMEKUKOSEA".. Mpaka unaamua kuomba radhi ni tayari umeshajifanyia tathimini na kujua kuwa ulikosea na kuteleza.
Kujitambua ni jambo moja ila kumiliki kiburi ni jambo jingine!!!
 
Wewe ni mgeni hapa jamvini, hiyo kauli aliitoa na kuna uzi wake upo humu.

Bila kumsahau yule DC wa Arusha Kennan Kihongosi aliwahi kusema wapinzani wanatakiwa wauwawe, aliyasema hayo akiwa mwenyekiti wa uvccm Iringa

Nyuzi zao na videos zipo humuhumu ngoja wafukua makaburi wataziweka hapa muda si mrefu.
Moja wapi hiyo

They will be crawling out of every hole now with conciliatory statements.
 
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umeomba radhi iwapo kuna mahali walitofautiana kimtazamo na makundi mengine na kutaka vijana wengi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika majukumu yake ya kuiongoza nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Jumapili Machi 28, 2021 na mwenyekiti wa umoja huyo Taifa, Kheri James wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma akibainisha kuwa huu ni wakati wa kusamehe ya nyuma na kufungua ukurasa mpya wenye mambo yatakayokuwa na tija kwa Taifa.

“Inawezekana katika siasa zetu na hekaheka za kutofautiana kimitazamo yapo mambo ambayo huko nyuma yalipelekea umoja wetu ukatetereka, sisi kama umoja wa vijana hatuoni aibu kusema tunaomba radhi kwa hayo kama tuliyatenda na tupo tayari kuyarekebisha ili kutengeneza jukwaa safi kwa rais wetu kuanza upya akiwa na watu walioshikamana ili nchi yetu iweze kwenda mbele.”

“Vijana wa nchi hii ndio watakuwa wanufaika wa kwanza Serikali ikiwa imara na vijana wa nchi hii ndio watakaokuwa wahanga wakubwa nchi ikiwa dhaifu.”

“Kwa hiyo ninasisitiza vijana tunahakikisha maneno na matendo yetu yanafanana na dhamira ya rais wetu ili kumrahisishia kazi yake mpya aliyopewa ya kutuongoza kama mkuu wa nchi ili sisi tuwe ni nguzo ya umoja, mshikamano na maendeleo ya nchi yetu,” amesema James.

Kweli maisha yanaenda kasi sana, Kheri James leo anaongea maneno kama kanyeshewa na mvua.
Mimi sio Chadema lakini huyu kijana aliniudhi aliposema "Safari hii hatutumii bunduki tutatumia sindano shwaaaaaaa....." Huu ulikuwa ujinga wa hali ya juu kwa sababu aliyeumizwa ni binadamu sio mnyama. Hata angekuwa nyama chama cha kuwatetea wangekuja juu.
 
Kazi ya technology ni kutunza historia,ayakane maneno yake.
Laana na baraka ya maisha yako imo ndani ya ulimi wako.Kila mmoja uandika historia ya maisha yake atakayo na mwisho wa mtu uanza na mwanzo wa mtu.Ogopa Sana kuhukumiwa na Jamii kupitia matendo yako.Dunia Bado haijawahi shindwa kufunza.
 
Attachments

  • VID-20210329-WA0017.mp4
    13.4 MB
  • VID-20210329-WA0022.mp4
    776.1 KB
  • VID-20210329-WA0021.mp4
    806.9 KB
  • VID-20210329-WA0020.mp4
    1.6 MB
  • VID-20210329-WA0019.mp4
    315.9 KB
Agiza Novida na karanga mkuu. point uliyoongea zinatolewaga MISIKITINI na MAKANISANI
 
TUNAYAKUMBUKA MANENO YAKE NA MATENDO YAKE.... HATUKUSAMEHI AFE KIPA AU BEKI
 
Halafu jamaa kumbe yupo vizuri katika kuongea na kupanga hoja,kumbe alikuwa anajitoa ufahamu.
Hahahhahaaha akilizao zimeanza kurudi japo itachukua muda kukaa sawasawa kwani babayao alikua anawependa watu wenye akili ndogo na rohombaya
 
Huyu Kheri kachanganyikiwa! Kwahiyo sasa marehemu ndio atwishwa zigo kiaina? Hivi mnafikiri mtaaminiwa na hao viongozi walio hai huku wakishuhudia matendo yenu?

Nafikiri yapo yanaendelea huko nyuma ya pazia ...
Mkuu
Kiongozi mzuri anayezaliwa automatically Ana Kariba za uongozi ....na Ni wachache Sana.....hiki Ni shihele
 
Unajua tatizo ni kuwa, kama wangevaa barakoa ingeleta picha kuwa pengine chuma kiliyeyushwa na deportivo...kitu ambacho kingekuwa ni kama kukivua nguo chuma cha pua.
Kwa hiyo ni mwendo kutembea mapua wazi huku unasali kimoyomoyo.
Hataree na Nusu.
 
Bulembo alikuwa anajisemesha tu, kama kumuua Zitto si angemtumia tu bintie Halima ambae alikiri kuwa huwa anafokonyolewa Vichakan na Zitto
Kuna mmoja alisema Lisu afe.

Mwingine akasema Zitto auawe

Bulembo naye tena ni alhaj skasema Zitto Kabwe afanywe nini sijui!!!

All in all kuomba msamaha ni jambo jema na Ijumaa Kuu wakafanye kitubio hao wakristo wawili!
 
Ahahahahahaha afu ukute mama hata hspokei simu yake au SMS maana kitakuwa kimempongeza kwa ushindi lakini hajibu!

Huyu mama kavu sana aisee
Uislam then mixer ni mwanamke..dharau na vichambo wavitegemee ..hauaa anaonekana anajua kunyali balaa .safiii mama
 
Huyu jamaa aangaliwe sana. Watu wa namna hii hapo alipo ndio inatakiwa iwe sehem yake ya mwisho kushika madaraka, warudishwe kwenye mashina huko wapewe deskjob. Kiburi na majigambo ya namna hii ndio yale waswahili wanasema "Pata pesa tujue tabia yako", hii sio tabia ya kujifunza ndani ya miaka kadhaa this is inborn and inbred hatred. Eti mtoto akidekezwa atakojoa kwenye kikombe cha babu? WTF

Huu msamaha it seems amelazimishwa kuomba sio akili yake, ukiangalia body expression wakati anaongea it shows arrogance na ile fikra ya "Kwani mtanifanya nini", yaani Hakuna unyenyekevu wa kufanya hisia za binadamu yeyote hata kichaa akapata feeling ya kutoa msamaha.
 
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umeomba radhi iwapo kuna mahali walitofautiana kimtazamo na makundi mengine na kutaka vijana wengi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika majukumu yake ya kuiongoza nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Jumapili Machi 28, 2021 na mwenyekiti wa umoja huyo Taifa, Kheri James wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma akibainisha kuwa huu ni wakati wa kusamehe ya nyuma na kufungua ukurasa mpya wenye mambo yatakayokuwa na tija kwa Taifa.

“Inawezekana katika siasa zetu na hekaheka za kutofautiana kimitazamo yapo mambo ambayo huko nyuma yalipelekea umoja wetu ukatetereka, sisi kama umoja wa vijana hatuoni aibu kusema tunaomba radhi kwa hayo kama tuliyatenda na tupo tayari kuyarekebisha ili kutengeneza jukwaa safi kwa rais wetu kuanza upya akiwa na watu walioshikamana ili nchi yetu iweze kwenda mbele.”

“Vijana wa nchi hii ndio watakuwa wanufaika wa kwanza Serikali ikiwa imara na vijana wa nchi hii ndio watakaokuwa wahanga wakubwa nchi ikiwa dhaifu.”

“Kwa hiyo ninasisitiza vijana tunahakikisha maneno na matendo yetu yanafanana na dhamira ya rais wetu ili kumrahisishia kazi yake mpya aliyopewa ya kutuongoza kama mkuu wa nchi ili sisi tuwe ni nguzo ya umoja, mshikamano na maendeleo ya nchi yetu,” amesema James.

Kweli maisha yanaenda kasi sana, Kheri James leo anaongea maneno kama kanyeshewa na mvua.
Huyo jamaa wa

Jamaa huyo alikuwa kiburi sana alishindwa kufaham kila jambo lina mwisho wake tutamsamehe akijiuzulu na vyombo vya dola vifanye uchunguzi kam kuna mabaya aliyaafanya sheria ichukue mkondo wake
 
Si ndie alikuwa akijinasibu kuua?
Si kijana wa 'hayati'
Huyu anatakiwa kuungana na bashite kujibu tuhuma za 'kudhulumu' maisha ya watu.
Mungu ni mwema. Atazidi kuwapigania wanaokandamizwa. Madhalimu na washirika wao wote, watajibu tu hizo dhulma. Wale waliojisahau na kudhani kuwa Jiwe ataishi na kutawala milele sasa hawana pa kukimbilia.
 
Hili ndo gape la upinzani kujijenga kichama na kisera,muda wa kuchukua nchi umewadia,mchwa wameanza kutafunana wenyewe,mlivyo vilaza mtaendelea na harakati zenu za kukosoa utawala uliopita badala ya kutumia huu mwanya kujijenga!
 
Back
Top Bottom