Uchaguzi 2020 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam: Yaliyojiri mkutano wa kampeni wa Dkt. John Pombe Magufuli

Mgombea wa Kigamboni kasema wao pekee ndiyo wamepewa hospitali mbili za wilaya na Magufuli kwa mkoa mzima wa Dar. Bahati mbaya akaja wa Kigamboni naye akasema hivyo hivyo yani eti Mbagala pekee ndiyo wamepewa hospitali mbili za wilaya kwa Dar. Hadi mtu unabaki kushangaa.

Nimeshangaa Gwajima yeye kataja maendeleo lukuki jimbo la Kawe huku anamsifia Magufuli. Mbaya zaidi akiwa jimboni anasema hakuna kilichofanyika na mbaya zaidi na zaidi ukisoma kitabu cha Mdee cha utekelezaji yote aliyotaja leo Gwajima yameandikwa kwenye hicho kitabu.
Yani wagombea wa CCM hawajiamini kabisa.
 
Baada ya kupumzika kwa siku kadhaa, mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli anaendelea na kampeni leo katika mkoa wa Dar es Salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Up dates;
HI NA LEO PIA MC ATAKUA ADAMU MCHOMVU? SABABU NATAKA KUSHUHUDIA PIA SHOW YAKE YA MITAMA.
 
Mbona mnaonekana mmepungua sana awamu hii ukifananisha na wakati wa Jakaya mmejitoa sana muhanga awamu hii au?
 
Katika uchaguzi kuwa upande wa ushindi ni raha sana. Asanteni Dar kwa kumwelewa Mhe Magufuli. CCM na watu kibao. Chama fulani kinajifariji kuwa wameletwa, malaki hayo ya watu wataletwa na mabasi mangapi na lori ngapi kwa hesabu tu ya kawaida.

Basi barabara zote za Dar hadi Morogoro ingejaa foleni ya mabasi hayo na malori hayo. Kubalini ukweli kuwa Mheshimiwa Magufuli anapendwa na watanzania na atashinda kwa kura za mafuriko. CCM oyeee...
 
Tanzania inakwenda kuweka historia...jamaa anaondoka aisee!!
Hakuna mwenye ubavu wa kumuondoa Magufuli, narudia tena kwa herufi kubwa HAKUNA MWENYE UBAVU WA KUMUONDOA MAGUFULI.
Wakumuondoa Magufuli na CCM yake hajazaliwa bado na hatazaliwa.
 
Endeleeni kujipa matumaini fake
 
Hakuna mwenye ubavu wa kumuondoa Magufuli, narudia tena kwa herufi kubwa HAKUNA MWENYE UBAVU WA KUMUONDOA MAGUFULI.
Wakumuondoa Magufuli na CCM yake hajazaliwa bado na hatazaliwa.
Wananchi hawamtaki...ndiyo maana anasomba watu kwa mabasi na kuweka wasanii kwa mikutano yake ili kuvuta watu wakati hiyo ni rushwa.
 
Mkuu tupo uwanjani tunaona live ujue. Kinachoendelea hapa ni aibu na uwanja hauna watu kabisa. Yaani Bora tungeenda Mbagala Zakhem
 
Nilikua taifa kwa ofisi ya DMO,ajabu eti huduma zote hakuna staff wameenda kwenye kampeni.

Magari ya TRH yamebeba hadi vitoto aibu sana
Wengi wameletwa na mabasi ya Abood kutoka Morogoro, JWTZ wamevalishwa tshirt za CCM n.k
 

Hahahahaaaa mmezodoka
 
Wananchi hawamtaki...ndiyo maana anasomba watu kwa mabasi na kuweka wasanii kwa mikutano yake ili kuvuta watu wakati hiyo ni rushwa.
Sema wewe humtaki usiwasemee wanachi, hao wanaosombwa kwenye magari kwenye watasombwa hivyo hadi kupiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…