Makubaliano ni kuwa kwa kuwa Sarpong na Fiston wanasemwa sana leo wapate nafasi ya kufunga. Wote au mmoja wapo hatakosa kuondoka na Goal.
Ila kubwa na la msingi ni kuwa iwe mvua liwe jua leo lazima Yanga tushinde. Match iliisha jana. Meck Mexime au Wanakagera Sugar hawana ugomvi na Yanga. Hawana haja ya kucheza kwa kukamia. Mpira ni starehe wanapaswa wacheze kwa ku relax.
Wanayanga popote mlipo leo muwe na amani na furaha. Achaneni na match ya Mbeya wale wanyak wapuuzi walijifanya wanaume sana.
Leo tupo na Wahaya. Hawa hatuna shida nao tunawafahamu. Hawana moyo Mgumu. Points tatu muhimu. Kocha wa Kagera Sugar anafahamu umuhimu wa sisi kupata points 3.