UWATA wamesambaratisha familia yetu

UWATA wamesambaratisha familia yetu

So sad, ukiongezea na ujinga wa watu wengi kushindwa kuhoji baadhi ya hizo imani kwa mfano ipo dhana moja viongozi wengi wa hizi imani huwaaminisha wafuasi wao eti kwamba kuna laana sijui mizimu ya mababu na mabibi au hata shangazi na watu engineo wa karibu inayoweza kukudhuru. Kutwa kucha wanahubiri uchonganishi kwenye nyumba za ibada.

Hebu imagine Bibi yako au babu aliyemzaa mama/baba yako eti alikuwa na maroho mabaya, hivi inaingia akilini kweli? Jiulize, huyu kiongozi ni mganga au mpiga ramli? Anapata wapi ujuzi wa kutambua kuwa bibi/babu yako alikuwa na hao roho wachafu? Huoni hata na wewe wajukuu zako wakija kuaminishwa imani hizi za kishenzi hata na wewe utakuja kuitwa mchawi au mshirikina wakati huo umeshatangulia mbele za haki? Tuwe na Imani lakini vitu vingine ni lazima tuhoji kama vina ukweli wowote ama ni njia ya wajanja kuchukua sadaka
Uko sahihi mkuu
 
Nilipita Soweto Mbeya nikaonyeshwa huyo jamaa aliopoanzia hiyo huduma yake. Lakini ktk kufuatilia kwa uchache nimeona kama ni cult fulani hivi. Sasa sijui ilibadilika baada ya jamaa kufa au tangu mwanzo maana na wewe unasema ulikuwa mdogo. Halafu kila anayesema alitoka, anasema alitoka akiwa mdogo.
Uliona ni cult au ulithibitisha? Kama ulithibitisha kuwa ni cult toa A-Z usiishie kuzungumzia hisia tu ambazo hzina uhakika itakuwa unafanya kupotosha au uongo
 
Nilivyowafahamu mimi UWATA, mtu anaendelea na dhehebu lake kama kawaida kama ni RC, Anglican, KKKT nk ila kuna muda hasa jioni wanakwenda kukutana ili kuabudu kwa mapana zaidi katika sehemu nyengine wanaita hekaluni.
Huyo anaeongoza hiyo ibada mnapokutana ye ndio tatizo,je unaijua madhabahu yake kiundani?
 
Nawafahamu kwa Sehemu, kwa ninavyo wafahamu mengi uliyoongea ni chuki binafsi au chuki na kikundi chao,
Najua wanaumoja sana ila hawavunji ndoa ,kwasababu nawafahamu watu kadhaa wanaosali huko na wana ndoa na watu wa madhehebu mengine,
Kuhusu nguo ni chuki binafsi, wanavaa kiheshima sana kama waisilamu au masista sema hawavai uchungu tu, hawasuki kama wasabato,hawavai heleni na hawana mambo mengi na hata wanaume hawavai vbya,
Ni kikundi cha kilokole ndio na si kanisa

Mwisho
Inawezekana kabla ya huyo kufunga ndoa ndoa ilikuwa na shida, na mahusiano yenu ya familia yapo na shida pia
**Kwani hamuwezi kusali kwenye madhehebu yenu au amuamini kuwa Mungu hayuko kwenye madhebu yenu mpaka kwenye hicho kikundi?
**Je mnajua dhumuni la mwanzilishi wa hicho kikundi?
**Mwisho wakati ni mwalimu mzuri hicho sijui kikundi kitakuja kuwa kanisa (dhehebu)fulani
 
Hicho chama unachokizungumzia ni WAWATA( Wanawake Wakatoliki Tanzania),, ni tofauti na UWATA( am not perfect sure ila nahisi ni Uamsho wa wakristo) kitu kama hicho

Usifananishe WAWATA na UJINGA
WAWATA ni Wanawake Wakatoliki Tanzania iweje mwanaume awe mfuasi wa WAWATA?
 
Yaliyotokea Uganda na juzi kati hapo Kenya watu hamjifunzi?biblia imeeleza kila kitu lkn baadhi hamuelewe anyway inawezekana ni kizazi cha nyoka
 
Tanzania Tuna uhuru wa kuabudu kola mtu afanye anavyoona ni sawa ww kama wa mizimu nenda,wa freemason nenda,sijui kkt,rc ,uwata ,cjui mwamposa nenda ,..... Maana unaujua mwisho wa yote kila mtu ataukumiwa kulingana na Matendo yake na si uliabudu wapi?
Maadamu huvunji sheria,
Pili mtoa Mada katafute hela zako Kwani lazima akupe zake,Tatizo hapo ni hela hamna kingine.
Kuna mambo ya Msingi ya kujadili ya bandari,
 
😂😂😂 hela ndo kitu mnajua. Hujioni ulivyo mjinga 🚮
 
😂😂😂 hela ndo kitu mnajua. Hujioni ulivyo mjinga 🚮
Mjinga ni ww ,tunajua wapi?
Kwani nilishawahi hitaji hela yako ?
Tunajua wapi na nan?
Hujielewi.
Mm sipo huko,ila kwa uelewa wangu kidogo ni kuwa imeandika chuki binafsi,
Familia yenu inamatatizo kaeni chini mtengeneze familia,
Inaonekana wote mnahusudi pesa ya mzee.
Na ili kutafuta wa kumtupia lawama unaenda kumtupia lawama watu usiyo wajua,
Jilaumuni nyie kwa kushinda kuweka umoja wa familia ,uwata ninao wajua mm hawafungishi ndoa na hawavunji ndoa?
Naenda kanisa walilofungia ndoa huyo mzee ndo umlaumu
 
UWATA - Uamsho wa Wakristo Tanzania.
UWATA - Ushirika wa Wahuni Tanzania.

Ogopa neno tata linalokuwa na maana zaidi ya moja.
 
Uliona ni cult au ulithibitisha? Kama ulithibitisha kuwa ni cult toa A-Z usiishie kuzungumzia hisia tu ambazo hzina uhakika itakuwa unafanya kupotosha au uongo
Nimeandika niliona kama ni cult flani kama ile ya Pool of Siloam hivi. Naifatilia usiwe na wasiwasi.
 
Mjinga ni ww ,tunajua wapi?
Kwani nilishawahi hitaji hela yako ?
Tunajua wapi na nan?
Hujielewi.
Mm sipo huko,ila kwa uelewa wangu kidogo ni kuwa imeandika chuki binafsi,
Familia yenu inamatatizo kaeni chini mtengeneze familia,
Inaonekana wote mnahusudi pesa ya mzee.
Na ili kutafuta wa kumtupia lawama unaenda kumtupia lawama watu usiyo wajua,
Jilaumuni nyie kwa kushinda kuweka umoja wa familia ,uwata ninao wajua mm hawafungishi ndoa na hawavunji ndoa?
Naenda kanisa walilofungia ndoa huyo mzee ndo umlaumu
🚮
 
Back
Top Bottom