Uwe makini zaidi unapotaka kununua gari kwa watu hawa

Status
Not open for further replies.
View attachment 2094407
Hawa jamaa wana ofisi zao posta..wanadai wana agiza magari unalipia nusu kisha gari ikifika unamalizia....binafsi nimeagiza gari miezi ya tisa kila nikipiga simu naambiwa boss hayupo nikienda ofisini naambiwa boss katoka nimewaandikia barua wamenijibu kwa kunipa masharti mapya ambayo kwenye mkataba wa awali haukuwepo mwishowe wananiambia niende popote...sasa mimi ntaenda huko popote na nitawaterea mrejesho kutoka huko popote ....sambazieni watu wasije wakapigwa hela ni ngumu kwa sasa
Uje na mrejesho mkuu na kama utawatia ktk 18 zako hakikisha wananuka chupi.
 
Mkuu pole, nadhani ungetoa details kwamba uliagiza gari gani na lini,hiyo pesa ya awali uliwapa kwa njia gani??na mlisainishana wakati unawapa hiyo pesa??una nalala yako ya malipo??kuna wahuni kama hao mwaka jana June walimfanyia hivyo ndugu yangu,baada ya kumzungusha sana akanipa hiyo taarifa,nikamwambia nitumie tu tiketi ya Ndege nije Dar kutoka Dodoma akatuma,tuliwaibukia saa 4 asubuhi ofisini kwao,kuingia ofisini kwa Boss tu nilichomoa mkwaju,nikakoki nikapiga risasi moja chupa kubwa ya Maji ilikuwa mezani pembeni ya huyo jamaa Mkurugenzi, nikamwambia nakuua rudisha pesa ya huyu jamaa hapa,alihamisha pesa palepale kutoka kwenye CRDB yake Account kuja kwa jamaa ndani ya dakika 2, ofisini kulikuwa kuna AC lakini tulitoka pale jamaa shati lote limeloa jasho,wahuni na matapeli kama hao ni ku-deal nao kihuni tu
Safi sana unyama unyama[emoji123][emoji123]
 
View attachment 2094407
Hawa jamaa wana ofisi zao posta..wanadai wana agiza magari unalipia nusu kisha gari ikifika unamalizia....binafsi nimeagiza gari miezi ya tisa kila nikipiga simu naambiwa boss hayupo nikienda ofisini naambiwa boss katoka nimewaandikia barua wamenijibu kwa kunipa masharti mapya ambayo kwenye mkataba wa awali haukuwepo mwishowe wananiambia niende popote...sasa mimi ntaenda huko popote na nitawaterea mrejesho kutoka huko popote ....sambazieni watu wasije wakapigwa hela ni ngumu kwa sasa

Polee mkuu.. fata sheria chako utapata tu
 
Wahi polisi wafungulie kesi, ushahidi unao kwamba uliwalipa mkasainishana
 
Ningesaidia ila mwenye ametoa thread sijawahi kumuamini pia humu ndani. Huyo illegal migrant.
 
Kampuni bora kabisa ya kuagiza magari nchini ni Garnite Co. Ltd - "Better Way and Beyond Standards". Wapo Mwenge Tower ghorofa ya 4 mkabala na Mlimani City.

Ila Mkuu Wanasheria tupo. Una kesi nzuri sana ambayo inaweza kukupatia fidia ya kukuwezesha kupata gari lingine la ziada.

Play your part, it can be done.
Wanasheria wa Bongo mnapenda sana pesa! Kama kweli unaona ana kesi nzuri si uingie mzigoni hadi akishinda kesi ndiyo ulipwe pesa yako yote! Utakubali au utamwambia akulipe kwanza advance!?
 
Maadili ya uwakili hayaruhusu hicho unachokisema..yaani upige kazi halafu utalipwa mteja akishinda. What if akishindwa? Hiyo kwenye rules za ethics inaitwa Contingency fee..ambayo ni prohibited.

Mwanasheria anatakiwa kulipwa before hajatoa huduma za uwakilishi mahakamani regardless kama mteja wake atashinda au atashindwa.
 
Mkuu pole, nadhani ungetoa details kwamba uliagiza gari gani na lini,hiyo pesa ya awali uliwapa kwa njia gani??na mlisainishana wakati unawapa hiyo pesa??una nalala yako ya malipo??kuna wahuni kama hao mwaka jana June walimfanyia hivyo ndugu yangu,baada ya kumzungusha sana akanipa hiyo taarifa,nikamwambia nitumie tu tiketi ya Ndege nije Dar kutoka Dodoma akatuma,tuliwaibukia saa 4 asubuhi ofisini kwao,kuingia ofisini kwa Boss tu nilichomoa mkwaju,nikakoki nikapiga risasi moja chupa kubwa ya Maji ilikuwa mezani pembeni ya huyo jamaa Mkurugenzi, nikamwambia nakuua rudisha pesa ya huyu jamaa hapa,alihamisha pesa palepale kutoka kwenye CRDB yake Account kuja kwa jamaa ndani ya dakika 2, ofisini kulikuwa kuna AC lakini tulitoka pale jamaa shati lote limeloa jasho,wahuni na matapeli kama hao ni ku-deal nao kihuni tu
Kuna siku utaitwa jambazi wakurosti mchana kweupe.
Enzi za ubabe zimrpitwa na wakati.
Rudia hicho ulichofanya nakuhakikishia hutatoboa.
 
Hata kwenye viwanja lipa kwa awamu kampuni moja inaitwa VKP ya Yona kanipiga milioni 6 kawapiga watz 250 jumla ya bilioni 1.200 kesi ipo mahakamani hana hata kumi ya kutulipa sijui pesa alikuwa anapeleka kwa mpalange? Huyu ukimloga utakosea kweli watu wamepigwa milioni 20,30,nk.
Mswahili ajawahi kuwa seriously.
Hii kampuni ya magari tangazo lao linavutia kweli kweli.

Ndugu, yona si bado yuko nyuma ya nondo au ameshatoka? VKP bado inaoperate?

The Monk i hope niliwahi kukwambia hiki kitu, na yule mtu wetu alishawahi kujiassociate na mtajwa hapo.
 
Mwanajf mmoja akiibiwa ni sawa na tumeibiwa wote ngoja kwanza twende kwenye page yao tukakichafue tuone wanatokea wapi
Mimi mwana jf nimeibiwaje mkuu wakati anaagiza gari hakutuambia? Au akipata gari yake Wana jf wote pia tutakuwa temepata magari?
 
Hawajakutana na watu walioaga kwao...

Anyway tujifunze kufanya research na kutumia makampuni ambayo yana reputations tayari
Kutafuta aina ya gari sahihi la kununua na kupata wakala wa kukusaidia kununua gari hilo ni sawa na mwanafunzi wa umahiri kutafuta upenyo wa kisayansi ( scientific gap) kisha anapata upenye wa kimaendeleo ( developmental gap).

Kwa ufupi hii kazi inahitaji utulize kichwa na uache haraka ya kuamini kila kitu na kila mtu. Amini tu kwa kufanya uchunguzi kwanza.
====
Pole kwa usumbufu huu mleta mada.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom