Uwezo wa gari kukimbia angalia RPM sio KMH

Uwezo wa gari kukimbia angalia RPM sio KMH

Unajua vitu ila umekosa kuona vitu vyenyewe halisi hizo gari zinakimbia kweli sio kwamba wanadanganya...

Namletea link hapa benz e class inaachwa jamaa anarekodi hiyo golf inasoma 257 anasema hazifiki 300[emoji23]
 
Video hiyo hapo golf inaila benz
 

Attachments

  • FullSizeRender.MOV
    31.2 MB
Namletea link hapa benz e class inaachwa jamaa anarekodi hiyo golf inasoma 257 anasema hazifiki 300[emoji23]
Hizo Golf Gti na R series wezi wa SA walikua wanazitumia sana maana kukamatwa ilikua tatizo baada ya hapo walikua wanatumia Ford Focus baada Serikali ya kaburu kujua hivyo na wao polisi wakapewa hizo R series mpaka Golf 10 wanazo hao Crime prevention zimewekwa Antenna juu zinakimbia balaa wao kuwakamata wezi huko freeway dk chache tuu huku wakitumia chopa kuelekeza...
 
1.9TDI kwenye Audi au VW ina horsepower 130.

Inatoboa 260kph bila shida.

Hizo golf zinazofika 320kph hata hazifiki 300hp.
130hp then ufike 260Kph..!!!?
Sio rahisi aisee.. Actually Haiwezekani..
Kumbuka IST ina 150hp..

Dashboards zinabandikwa tuu..
518i
520i
525i
530i
535i
540i
Zote dashboard inasoma 260kph..ila hazina uwezo sawa..!
 
Hizo Golf gti na R series wezi wa SA walikua wanazitumia sana maana kukamatwa ilikua tatizo baada ya hapo walikua wanatumia Ford Focus baada Serikali ya kaburu kujua hivyo na wao polisi wakapewa hizo R series zimewekwa Antenna juu zinakimbia balaa...

[emoji23][emoji23] hivo vidude ni motooo
 
130hp then ufike 260Kph..!!!?
Sio rahisi aisee.. Actually Haiwezekani..
Kumbuka IST ina 150hp..

Dashboards zinabandikwa tuu..
518i
520i
525i
530i
535i
540i
Zote dashboard inasoma 260kph..ila hazina uwezo sawa..!
Video za 1.9tdi zimejaa mtandaoni mkuu. Halafu hii ni diesel.

Maana ni engine common sana ya Audi na VW.
 
Nilichogundua kwenye huu uzi ni mashindano ya kila mtu kuonekana anaijua gari vizuri wakati wengi ni weupe tu.

Hakuna aliyemrekebisha mleta mada kwa fact, zaidi ya kila mtu kutaka kujionyesha anaijua gari kuliko mleta mada.
 
Kuna kitu kinaita Horse power mnaweza kuwa sawa Speed bt mwenzio ana horse power kubwa automatical atakupita tuh.
E.G. Ist atembee 80km/r then Altezza atembee speed 80km/r na wote waanze pamoja eneo moja. Unafkir nani atakae mpita mwenzie[emoji1][emoji2][emoji3]
Hivi unajua kuwa speed ni unit? Ukiona gari imeipita nyingine ni matokeo ya kuwa hiyo gari inatembea speed zaidi ya nyingine. Au ndio yale ya kilo moja ya chuma ni nzito kuliko kilo moja ya pamba?
 
Kuna kitu kinaita Horse power mnaweza kuwa sawa Speed bt mwenzio ana horse power kubwa automatical atakupita tuh.
E.G. Ist atembee 80km/r then Altezza atembee speed 80km/r na wote waanze pamoja eneo moja. Unafkir nani atakae mpita mwenzie[emoji1][emoji2][emoji3]
kilo moja ya pamba na mchanga mi ipi nzito zaidi??

majibu ni rahisi sana. 80 kwa 80 jibu ni =
 
Ninacho jua gari ambayo inaspidi rpm inaweza kuwa kwenye 3 na spidi ikawa kubwa zaidi naambayo haina spid rpm inaweza kuwa kwenye 4 na spidi ikawa ya kawaida na kupitwa mwendo na ambayo iko kwenye rpm 3.
 
Rpm haimaanishi Speed aise, Rpm ni uwezo wa gari kuchanganya speed yake kwa sekunde. Sijui kwa lugha nyepes nisemaje ila mfano kuna gari ili ifike speed ya km 80 Itatumia dak 1 wakat nyingine Itatumia dk 2. Lakin gar hizo zote zikifika speed ya km 80 zitakua ktk mwendo sawa hakuna wakumpita mwenzake wala nin ila kumbuka mmoja kufika speed ya km 80 aliwah dk moja kabla hivo atakuuwa yupo mbele.
 
Rpm ni mzunguko wa injini.
Kph ni umbali kwa muda

Yaani umbali flani kwa muda gani hivi vitu 2 havina uhusiano kabisa kinachofanya rpm kupishanapishana ni gia box. .
Mnaweza kutembea wote 50kph mkatofautiana rpm kulingana na aina ya injini na gia iliopo..

Kama ushaona pikipiki inatoa mlio wa kulalama alafu hata aikimbii kama mlio unavyo dai ila kuna nyingine mlio wa kawaida ila inatembea sana.

Rpm inabadilishwa na pedo ya mafuta na kph inabadilishwa na spid ya injini na gia pamoja eneo.

Rpm inaweza kua 0 ila 100kph hapo imefeli kwenye mteremko.

Rpm inaweza kua 6000 ila 0kph hapo ipo gereji wanajaribu carburetor

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Yaani niwe 80km/hr na wewe 80km/hr unipite? Hii Sayansi umesomea wapi ndugu yetu, mtaalamu.
 
Wengi wetu utasikia ile gari inakimbia sana, ni kweli gari lazima kukimbia ila ushawai kujiuliza mnaweza kuwa spidi sawa ila ukashangaa anakupita bila kutegemea.

Utengenezaji wa magari kuna vitu vingi vinaangaliwa ili kufanya gari kukimbia ila kinachowezesha ni injini.

Injini kila siku zinavozidi kutengenezwa zinasumbukiwa RPM ili wewe kukusaidia gari lako kwenda vizuri.

Nini maana ya RPM(Revolutions per minute):
is a unit of rotational speed or rotational frequency for rotating machines.

Wajuzi wa magari na mafundi nataka mtueleze

View attachment 2521539

Mimi sio mtaalamu wa magari ila ninajua kwa mujibu wa uzoefu na u bush lawyer wangu

Speed ni constant yaani ni moja tu iwe baiskeli bajaji virtz v8 boieng au jet
Ndio maana kitochi cha trafiki kinasoma magari yooote

RPM siijui kitaalam ila naijua kwa mtazamo wangu ninapotumia gari(i stand to be corrected)
RPM naiona kama ni namna unavyo kanyaga mafuta kuipa nguvu injini kuzunguka
Unapokua kwenye gia ndogo na unataka gari iongeze speed ukikanyagana mafuta RPM itapanda na ukiachia mafuta na kupunguza mwendo itashuka
Ukiwa kwenye mlima na ukakanyaga mafuta RPM itapanda

Binafsi huwa naitumia sana kujaribu ku control ulaji wa mafuta haswa kama nakwenda safari ndefu

Gari yangu kwenye screen ya radio huwa inaonyesha average ya speed na ulaji wa mafuta km/liter
RPM inapokua chini inakula mafuta kidogo kuliko inapokua juu inakula mengi
Nikitembe na wastani wa RPM ikiwa inacheza kwenye 3+ huwa napata wastani wa 8.5 kilometers per liter
Lakini niki control RPM iwe inacheza chini ya 3 napata 10 hadi 11 kilometer per liter

Kazi kubwa huwa ni kupata timing ya acceleration ili upate soeed unayoitaka lakini RPM iwe chini
Unaweza kuwa speed 120 lakini RPm ikawa juu pia

Inawezekana ni zaidi ya nijuavyo lakini kwangu mimi ni kipimo kizuri cha kucontrol ulaji mafuta
 
Back
Top Bottom