Maana naona kasi ya kutumia hili neno inaongezeka, Mtu ukipingana mawazo na Raisi au Waziri wewe sio mzarendo, Ukihoji kitu kuhusu Nchi yako ambacho kiongozi hataki kijulikane wewe so mzarendo, sasa uzarendo ni nini?
Nimemwona Mwakyembe akiwaasa Viongozi wa kidini kuwafundisha waumini wao uzarendo, sijajua alikuwa anataka Viongozi wa Dini wawaeleze Waumini wao kukubaliana na Mawazo ya Viongozi? au alikuwa na maana gani,
Watu wote waliohoji vitu fulani fulani Serikalini wameitwa sio wazarendo,
Ndege imezuiliwa Canada, Tundu lissu kahoji kaitwa Sio mzarendo, Zitto kahoji kuhusu Uchumu kaitwa sio mzarendo, sasa uzarendo maana yake nini?