Uzalendo ni nini?

Uzalendo ni nini?

Wadau nisaidieni uzalendo ni nini maana wamshabikiao jpm wanasema ni uzalendo waoneshao uozo wanaonekana si wazalendo je uzalendo ni nini?
Hakuna philosophical thinker anayeweza kuweka definition yake, sana sana ni mapovu ya Lumumba.
 
uzalend n kupenda na kutetea chama tawala, hata kikfanya maov au kikikurupuka n kukitii kukiheshem na kukisifia. Yahata kama kna2peleka shmon n kukubal tu
 
Kuna watu wana jiuliza uzalendo ni nini baada ya kuona mahakama ya mafisadi haijawahi kufunga hata mtu mmoja wakati kuna wanasiasa wanapigwa risasi mchana!!

Uzalendo ni kupenda nchi yako kwa moyo wako wote na kupongeza serikali pale inapofanya vizuri na kukosoa pale inapofanya vibaya.
 
Kuna watu wana jiuliza uzalendo ni nini baada ya kuona mahakama ya mafisadi haijawahi kufunga hata mtu mmoja wakati kuna wanasiasa wanapigwa risasi mchana!!

Uzalendo ni kupenda nchi yako kwa moyo wako wote na kupongeza serikali pale inapofanya vizuri na kukosoa pale inapofanya vibaya.
Unatakiwa kuwa Ndiyo Mzee.
 
Maana naona kasi ya kutumia hili neno inaongezeka, Mtu ukipingana mawazo na Raisi au Waziri wewe sio mzarendo, Ukihoji kitu kuhusu Nchi yako ambacho kiongozi hataki kijulikane wewe so mzarendo, sasa uzarendo ni nini?

Nimemwona Mwakyembe akiwaasa Viongozi wa kidini kuwafundisha waumini wao uzarendo, sijajua alikuwa anataka Viongozi wa Dini wawaeleze Waumini wao kukubaliana na Mawazo ya Viongozi? au alikuwa na maana gani,

Watu wote waliohoji vitu fulani fulani Serikalini wameitwa sio wazarendo,

Ndege imezuiliwa Canada, Tundu lissu kahoji kaitwa Sio mzarendo, Zitto kahoji kuhusu Uchumu kaitwa sio mzarendo, sasa uzarendo maana yake nini?
 
uzalendo ni kutetea rasilimali za Taifa zisiibiwe na wazungu.........CHADEMA wanatetea wazungu watuibie
 
Uzalendo na sio uzarendo
Huko shule ulienda kusomea ujinga?
Ndio matatizo ya yenu, yaana mna mambo ya ajabu sana, hoja umeielewa, kosa la herufi limekufanya usijibu hoja, haya wewe mzalendo.
 
Salam,nimekuwa nikijiuliza neno"UZALENDO"huwa linamaana gani kwa wana ccm walio wengi?
Kila mtu atakaetoa mawazoyake kwenye kadamnasi anahesabiwa si mzalendo,mtu anaetumia haki ya kikatiba kufanya chochote tofauti na mtazamo wao anaitwa"si mzalendo".
Mawazo wanayoyakataa siku zote, akijitokeza mtu akafanya lile lililokataliwajana,na mtu akahoji kwanini lilikataliwa jana,anakuwa si mzalendo.
Naomba kujulishwa,kwa tafsiri ya CCM hasa wafuasi,uzalendo kwao UNA MAANA GANI?.
 
Nimetoka kuangalia kipindi cha Clouds 360 na kukutana na chagizo iliyotamalaki ya " uzalendo ni kupeana dili". Niwaulize tu wadau, je ni kweli kwamba uzalendo ni kupeana dili? Source Clouds 360!
 
Kwa tanzania ya sasa ni kuwa Uzalendo ni kutoikosoa serikali hadharani!
 
kaAatika ccm uzalendo nikuhakikisha unaipigania ccm hadi kufa
 
Inaweza kuwa sijaelweka kwenye kichwa habari kuhusu swali langu.
Swali langu ni rahisi sana na linamaanisha hivi...kwa sisi Watanzania, tafsiri ya neno 'uzalendo' ni nini?

1. Je, kukosoa pale tunapoona mambo hayako sawa, ili kuepukana na kuharibikiwa kama taifa (pasipokujali itikadi za kisiasa)?. ama,

2. Kupongeza na kushangilia kila jambo hata kama ni la kipuuzi (na hii ni kwa sababu tu aliyeongea na kuamua jambo ni mtu wa chama B kwa wanachama B?

Vilevile unaruhusiwa kuja na tafsiri yako ya neno 'uzalendo' ili na wengine waelewe vizuri kama navyotaka kuelewa vizuri.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom