Aidha, tukumbuke kuwa lengo la kuishi siyo kutumia wakati wetu wote katika shughulikia maisha bila kuhakikisha tunaishi kwa furaha, amani na utulivu. Ni dhahiri kuwa tunawajibika kuwa na hali ya kufanikiwa na kufanya kazi kwa juhudi zote, lakini tukifanikiwa kuziliwaza mbongo na kuburudisha miili yetu, tutaweza kuzifanya fikira zetu ziwe makini zaidi na kupata matokeo bora zaidi. Tukijizoeza kupumzika walau kidogo kila siku, tutastaajabu jinsi tutakavyoweza kufanya kazi kwa makini zaidi na kwa kiwango kikubwa bila kuchoka.