Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-08-17-09-32-12.png
 
Maji yanasaidia nywele
Kwa wale wadau wa masuala ya urembo hasa kina dada zaidi ya kuritubisha ngozi maji husaidia kung’arisha nywele . Kuosha nywele kwa maji ambayo hayajachemshwa kwa kutumia virutubisho vya nywele vya kutengeneza kama vile shampoo na mafuta maalum aina ya conditioner yanazifanya nywele kuwa thabiti zaidi na kuondoa uwezekano wa kung'oka hovyo hovyo huku zikiwa na mn’gao.
 
Ngozi ya mwili husaidiwa sana na maji
Zaidi ya ngozi ya uso maji ni muhimu kwa ngozi ya mwili kwa ujumla . Wakati wa kuoga maji ya moto au vugu vugu hufanya ngozi ya mwili kuwa nyororo na yenye afya zaidi , maji husaidia kuondoa ukavu ambao huondoa mvuto wa asili wa ngozi na kuipa afya kwa ujumla.
 
Maji husaidia kupunguza uzito wa mwili
Kwa wale wenye matatizo ya uzito wa mwili ambao wakati mwingine unaweza kuwa hatari kwa afya, kwa kusababisha matatizo kama Presha, kisukari na magonjwa ya moyo, maji yanaweza kuwa kimbilio lako. Kwa mujibu wa utafiti , watu wazima wanaokunywa glasi nane za maji kwa siku yaani angalau glass mbili kwa kila baada ya saa kadhaa hasa kabla ya na wakati wa kula wanajikuta wakila chakula kidogo na hivyo kufanya mwili wako kupata chakula kile kile kinachohitajika na hivyo kuondoa uwezekano wa mwili wako kulimbikiza chakula kinachofanya uzito wako uendelee.
 
Maji huisaidia akili kufanya kazi vizuri
Mwili unapokosa maji tatizo pekee sio mtu kuhisi kiu wakati mwingine ubongo huhisi kuchoka kirahisi na haraka pale ambapo mtu hajanywa maji muda mrefu . Hisia kama hasira , uchovu wa akili , kuchanganyikiwa humtokea mtu kirahisi wakati akiwa hajanywa maji muda mrefu na wakati mwingine hata kichwa huuuma sana lakini suluhisho la yote haya ni kunywa maji mara kwa mara .
 
Muwasho wa koo
Muwasho wa koo unaotokana na alegi (allergy) au mafua hutibiwa na maji , mtu anapopata tatizo hili suluhisho la haraka ni kusukutua maji yenye chumvi lakini kuepusha tatizo hili ni kuhakikisha koo halikauki kwa muda mrefu.

Maji husaidia kupigana dhidi ya magonjwa

Maji yana msaada mkubwa sana kwenye kupambana na magonjwa mwilini mwako . Ni vizuri kunywa maji mara kwa mara kuepusha mwili wako na magonjwa . Pia ulaji wa matunda husaidia kuupa mwili maji muhimu yanayokuwa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali . Matunda kama mapapai,matikiti maji,matango,machungwa ,ndizi,maembe yanauongezea mwili maji ambayo yanakufanya ukae muda mrefu bila kuugua .
 
Ndiyo madhara ya kuota ndoto mchana, tangu akiwa mvulana ameishi akiwaza urais, amegombea mara kadhaa na sasa amejiaminisha uchaguzi huu lazima atashinda tu. na sasa anaelekea kutoamini kuwa hatakuja kuwa rais tena. Ni kama mtu aliyekata tamaa ya maisha. Subiri tuone

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa siasa za Kenya na ukabila ulivyo Ruo kuongoza Kenya si rahisi
 
Back
Top Bottom