Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3024.jpg
Hakuna jinsi wala suruali zaidi ya kumuomba Dangote anunue Timu hili amfukuze huyu mtu
 
Moja ya vitendo vya mwili ambavyo viko nje ya uwezo wa mtu kujizuia ni kutetemeka. Wataalamu wanabainisha kuwa, kuna baadhi ya aina za kutetemeka zinazowapata watu ambao wana afya njema na aina zingine hutokea kama athari hasi za matumizi ya dawa aina fulani. Lakini kwa sehemu kubwa, kutetemeka kwa baadhi ya viungo vya mwili, ni moja ya dalili za baadhi ya magonjwa yanayoshambulia mfumo wa fahamu.
 
Sehemu kubwa ya mfumo wa fahamu inatengenezwa na ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu inayosambaa mwili mzima. Mfumo huu ndiyo unaotawala vitendo mbalimbali vya mwili kama vile, vitendo vinavyofanyika kwa utashi wetu na vingine vinavyofanyika nje ya utashi na uwezo wetu wa kuamua au kujizuia.

Wanasayansi wanakadiria kuwa ubongo wa binadamu una seli nyingi kiasi cha bilioni 14 hadi 100.
 
Lakini utafiti wa hivi karibuni, ulioongozwa na Frederico Augusto Casarsa de Azevedo na kuchapishwa mwaka 2009 katika jarida liitwalo ‘The journal of comperative neurology’ toleo la 513(5), unakadiria kuwa ubongo wa binadamu una wastani wa seli bilioni 86.



Zinavyofanya kazi

Dk Suzana Herculano-Houzel katika utafiti wake naye pia alipata matokeo yanayofanana na hayo. Seli hizi zote zina kazi maalumu na zinashirikiana katika utendaji wa ubongo.
 
Seli za ubongo pamoja na majukumu mengine, hupokea taarifa mbalimbali za hisia toka kila sehemu ya mwili na kufanya kazi ya kuzitafsiri. Baada ya hapo, ubongo hutoa mrejesho kuhusu taarifa hizo kupitia katika uti wa mgongo na mishipa ya fahamu iliyoko pembezoni mwa mwili.

Mfumo wa fahamu unaweza kusisimuliwa na kufanya kazi kwa namna isiyokuwa ya kawaida bila seli zake kuathirika kimaumbile.
 
Lakini wakati mwingine seli na tishu za mfumo wa fahamu, zinaweza kuathiriwa na maradhi na kusababisha utendaji usiokuwa wa kawaida.

Katika hali ya namna hii, mfumo wa fahamu unaweza kusisimka kwa kiwango cha juu kuliko kawaida na kuamuru misuli ya mwili kufanya kazi kwa namna isiyokuwa ya kawaida. Jambo hilo husababisha mshtuko wa ghafla, mtetemo wa mwili au kukakamaa kwa misuli.
 
Watafiti wa masuala ya magonjwa ya mfumo wa fahamu wanabainisha kuwa kuna zaidi ya aina 600 za maradhi yanayoshambulia mfumo wa fahamu.

Seli au sehemu za ubongo zinazotawala utendaji wa misuli ya mwili zikishambuliwa na maradhi haya, dalili zinazojionyesha ni kupooza au kutetemeka kwa baadhi ya viungo vya mwili.
 
Back
Top Bottom