SIMULIZI YA MFALME MTATA NA MCHAMUNGU. Baada ya salaam na mazungumzo mafupi Mchamungu akafunguka. "Bwa mfalme nimekuja kwako kwakuwa nimepatwa na mtihani, mtihani wangu hasa unahitaji fedha, baada ya kutafakari kwa kina nikaona nije kwako maana uwezo wa kunikopesha au kunisaidia unao, hata hivyo ikitokea kwamba nawe huna ninachohitaji, hakuna shida, hivyo sina kinyongo. Maana naamini mwenyezi mungu aliyenipa mtihani, pia ana uwezo kuniondolea mtihani huu kwa jinsi anavyoona inafaa". Mfalme akajibu, "Mchamungu una shida, halafu unajifanya mungu atatatua shida zako, mimi ningeweza kukupatia hicho unachotaka, lakini hata nikikupa utajifanya ni uwezo mungu wako. kwakifupi nenda ukaseme na mungu wako umalize shida zako kwa jinsi unavyojua mwenyewe". Mchamungu akajibu, hata hilo pia nashukuru maana Mungu ninayemuamini hashindwi kutatua changamoto nilizonazo, maana ana nguvu na uwezo. kwamba aweza kukufanya dhalili hata wewe mfalme mwenye nguvu, akakushusha. Kauli hii ilizidi kumkera Mfalme. akasema. Ufalme huu nimerithi kwa vizazi na vizazi nyuma, kufikiria Mungu anishushe kwa kupoteza cheo nilichonacho na mali nilizonazo ni ndoto zako tu bw Mchamungu" Kwahiyo naomba uondoke. Mchamungu akaenda zake